KERO Mwendokasi ni Changamoto zaidi ya inavyozungumzwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
.. Mradi ulianza na wale matapeli wa simon group waliyojidai wamenunu UDA na eti wakaingia ubia na serikali kwenye udart. Hawakuweka hata senti zozote kununua uda au kuingia ubia na serikali isipokua utapeli mtupu. Eti wakajidai wanalipa deni kuingia ubia na udart huku wakitumia mapato ya ubia udart kulipia hisa zao udart. Kichekesho kitupu. Nadhani magufuli kimyakimya akawatimua na kuwatupa gerezani hao kina Robert Kisena wa simon group. Kwa vyovyote jinsi udart wameanza ni vigumu kuendelea vizuri. Mwanzo mapato mengi yaliishia kwa hao matapeli. Tatizo kubwa la udart kwa sasa ni uchache wa mabasi na pengine upotevu wa mapato mkubwa. Wale matapeli wa simon group badala ya kuleta mabasi 400 marefu 'articulate buses' yaliyokua ndio mahitaji wakaweza kuingiza mabasi kiasi cha zaidi mia mengi yakiwa yale ya kawaida 'standard buses' na hata hivyo walishindwa kulipia ushuru mengi yakabakia yamezuiliwa bandarini.
 
Na Bado kwenye Sgr 😆😆

Hiyo BRT ni mradi wa kifisadi pia , gharama inazotumia kujenga hizo njia za zege ingetosha kufungua routes Mpya za Jiji na Msongamano usingekuwepo.
SGR muda si mrefu kutakuwa na maumivu

Ova
 
Idara ya Usalama wa Taifa iamke
 
Wanaotumia huo usafiri on daily basis kazi wanayo tena sio ndogo...last week nilienda posta muda wa kurudi nikasema acha nikapande mwendokasi kivukoni, picha linaanza nafika pale kuna nyomibla kutosha ndani alaf hamna basi hata moja.
Watu wametulia tuli wakioneokana kukosa matumaini! Nikajisemea shida yote ya nini , nikaita bolt tu!
 
Usafiri wa ajabu kabisa huu

Ova
 
Alafu walivyo na upuuzi wakaanzisha root ya kibaha, mjini mabasi hayatoshi wewe unayapeleka kibaha!
 
Kuzorota kwa huduma za UDART - Mwendokasi ni AIBU na FEDHEHA kubwa kwa Mama Samia na Serikali yake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…