kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
.. Mradi ulianza na wale matapeli wa simon group waliyojidai wamenunu UDA na eti wakaingia ubia na serikali kwenye udart. Hawakuweka hata senti zozote kununua uda au kuingia ubia na serikali isipokua utapeli mtupu. Eti wakajidai wanalipa deni kuingia ubia na udart huku wakitumia mapato ya ubia udart kulipia hisa zao udart. Kichekesho kitupu. Nadhani magufuli kimyakimya akawatimua na kuwatupa gerezani hao kina Robert Kisena wa simon group. Kwa vyovyote jinsi udart wameanza ni vigumu kuendelea vizuri. Mwanzo mapato mengi yaliishia kwa hao matapeli. Tatizo kubwa la udart kwa sasa ni uchache wa mabasi na pengine upotevu wa mapato mkubwa. Wale matapeli wa simon group badala ya kuleta mabasi 400 marefu 'articulate buses' yaliyokua ndio mahitaji wakaweza kuingiza mabasi kiasi cha zaidi mia mengi yakiwa yale ya kawaida 'standard buses' na hata hivyo walishindwa kulipia ushuru mengi yakabakia yamezuiliwa bandarini.Aisee, Naomba nitoe pole kwa watumiaji wa huu usafiri.
Binafsi nilikuwa najua ni changamoto kidogo tu na kuona kama vile wabongo tunapenda kulalamika, Nimenyoosha mikono leo.
Kwenye kituo kuna watu wengi sana, magari hakuna! yanayokuja yamejaa kupita kiasi.
Nimeingia kituo cha City Council (Jiji) saa 11 kasoro 15 jioni sasa ni karibia saa 12 jioni bado sijafanikiwa kupanda.
Nchi yetu inashida sana wadau.
Kuna watu wanatakiwa kuchapwa viboko hadharani, kwa hujuma ya huu mradi hii idadi kubwa hivi ya watu ni pesa yakutosha.
Huu mradi ulipaswa kuwa mfano wakuigwa as hakuna nchi iliyouweza East Africa zaidi yetu.
Ni balaa na nusu.
Poleni sana watumia Mwendokasi kwa mateso makali.