Mwenezi CCM kupatikana 03/04/2024; Nani anafaa kurithi mikoba ya Makonda?
Chama cha mapinduzi CCM ndani ya miaka minne ya Samia wamebadili makatibu wenezi karibu watatu.

Imefika hatua leo waanza kutafuta makatibu wenezi kwa tochi tena mchana, chama ambacho kinajinasibu kina viongozi makini, vijana makini leo wakumuwaza Mwijaku kweli?Wakumuwaza Dotto magari kweli?

Vijana wa Lumumba mjitafakari ambao mnajiita CCM kindakindaki leo hamna sifa ya kupewa uenezi jambo la aibu sana mkiambiwa CCM imefilisika kimawazo mnapinga.

Hiyo haitoshi mpaka mnawaza tena kupangua wakuu wa mikoa waje kushika hiyo nafasi wakati mnavijana wengi.

SIna mengi ila HONGERA SALIM KIKEKE KWA KWENDA KUTEULIWA KUWA KATIBU MUENEZI CCM
 
Kama Makonda aliyekuwa na mvuto hajakubalika, unadhani nani atakubalika wakati unajua "Bosi wa sasa hataki kuzidiwa umaarufu"!
Wateule wake wote wamepooza kama maandazi ya mhogo yaliyolala (namaanisha kiporo cha maandazi ya mhogo).
Zero brain, academic failure, murder suspect... ana mvuto gani?

Au unamaanisha kwa lile genge yatima?
 
Kama kichwa kinavyojieleza na pia makada ambao wanajisifu watoto wa mama ambao wapo Lumumba leo wanaenda mpigia magoti bosi mpya SALIM KIKEKE ambaye ndiye anaenda kuwa muenezi wa CCM.
Mnaobaki endeleeni kusema mama anaupiga mwingi kongole sana KIKEKE
Nyie ndo mnamchulia Kila mwaka, Mkiona Uchaguzi unataka Kufanyika wa mwenezi bhasi mnaanza kumletea Uchawi..
Hata kama mteuaji anataka kumchagua anaacha..
Kwanini
 
Tetesi sio uhalisia
FB_IMG_16854885764003555.jpg
 
Ili kukivuta Kizazi kipya Chamani ni lazima Katibu wetu wa Itikadi na Uenezi awe na Mvuto wa Asili siyo wa Mchongo

Mlale Unono 😀😀
Unasema?
Yaani sisiem iombewe mema?
Kuna shida uko nayo kichwani mwako.

Binafisi nikisikia kuwa sisiemu na waliowahi kupita sisiem wote wakiwemo na ndugu zangu ambao pia ni sisiem wamepatwa na tetemeko la ardhi na kutojulikana waliko nitaendelea na shughuri zangu tu wala sitoshituka hata kidogo.

Ukiachilia mbali mimi kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa ila ninatambua kuwa matatizo mengi yanayo sababishwa na binadamu hapa Tanganyika yanasababishwa na hao niliowataja.
 
Makada ambao wanajisifu watoto wa mama ambao wapo Lumumba leo wanaenda mpigia magoti bosi mpya SALIM KIKEKE ambaye ndiye anaenda kuwa Mwenezi wa CCM.

Mnaobaki endeleeni kusema mama anaupiga mwingi kongole sana KIKEKE
kwani kuna ubaya gani akiteuliwa huyo muungwana, na halafu hao wengine wakaendelea kua wanachama watiifu na wafuasi kindakinaki wa Chama Cha Mapinduzi 🐒
 
Back
Top Bottom