Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Mwenge haujadiliki kisayansi kwa sababu misingi na dhima yake si ya kisayansi..

NB: Kuna wakati huwa unapelekwa nyuma ya jukwaa na kutamkwa "tumaneno maneno yasiyoeleweka"..

Mkuu Paskali; mwenge ni zaidi ya moto ule.. Ni zaidi ya mwanga..!
Everything is science !
 
Aisee yanayofanyika kwenye mikesha ya mbio za mwingi ni dhambi tupu. Mikesha ya mwenge inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi, mimba zisizotarajiwa na kujifunza ulevi. Siku mwenge ukiwepo sehemu usiku ukipita asubuhi utakuta kondomu zilizotumika na pakiti na chupa za pombe kali zimetapakaa kwenye vichochoro.
 
MWENGE ni miongoni mwa mazindiko ambayo nyerere na wale wazee wa Bagamoyo waliambiwa na mfalme wa hii dunia wawe wanafanya ili kuwapumbaza raia kwa lengo la kuendelea kuwaongoza,ndiomaana siku ile tunapata uhuru waliambiwa ni lazima upelekwe mlima kilimanjaro saa 6 usiku,miongoni mwa mazindiko mengine aliyoyafanya ni kukusanya michanga/udongo kutoka mikoa yoote ya tanganyika na kwenda kufanya zindiko mahali fulani(sitapataja),haya mazindiko yamekuwa yakifanywa mara kwa mara na viongozi wa CCM kwa lengo la kuiroga nchi ndiomaana akili za watanzania ni tofauti na wakenya,waganda,wacongo na baadhi ya majirani zetu,watanzania ni wavivu na waoga sana waku-react pale maswala muhimu yanapotokea mfano,wizi wa kura,mfumuko wa bei,kodi kandamizi,miundombinu mibovu,hali duni ya maisha,uonevu wa polisi,ubadhilifu wa viongozi wetu,katiba bora,tume huru ya uchaguzi! na mengine mengi,ndiomaana Kenya Uganda Congo DRC na kwingine mambo kama hayo yakitokea huwa hapakaliki sababu akili zao sio mgando kama zetu sisi bado ule uchawi wa kupenda Amani tunao!
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda haya mazindiko yanakwisha nguvu yake sababu watanzania wengi wamekuwa aware nayo so ile nguvu inashuka kiwango chake ila kwa mikoa ambayo bado yananguvu hata uwezo wa raia wa huko wa kufikiria ni mdogo sana hiyo mikoa nikama Dodoma,Tabora,Lindi,Mtwara,Kigoma na Singida na Pwani, mikoa ambayo nguvu ya haya mazindiko ya CCM imeanza kupotea kabisa ni kama MWANZA,ARUSHA,KILIMANJARO,DSM na MBEYA akili za rai wa hii mikoa ni tofauti na mikoa mingine.
Nyerere ndio alikuwa mchawi wa CCM akishirikiana na wazee wa bagamoyo na wazee wengine 12 sitawataja hapa,baada ya nyerere kufa uchawi wa CCM akakabidhiwa Mzindakaya,stiven wassira ,Kingunge Ngombalemwilu na Andy Chande (Marehemu sasa), hao woote umri wao umekwenda na baadhi yao wapo taabani kisiasa na kiafya pia na hata wengine kuhama chama.Viongozi wengi wa kidini hapa Tanzania wanajua kuhusu haya mazindiko wapo ambao hufunga na kuomba ili kuyavunja kimesaidia sana kupunguza makali ya haya mazindiko.
Vita ya Kagera,Mafuriko ya Lindi Mtwara ,ajali ya MV Bukoba,ajali ya treni reli ya kati DODOMA,maajali ya mabasi,ajali ya watoto arusha,na mengine mengi ni miongoni mwa sadaka au mazindiko au kafara ambazo wamekuwa wakitoa,ndiomaana tunapokuwa tunakaribia uchaguzi ajali nyingi kubwa kubwa huwa zinatokea SIO BURE!
kwa makosa waliyofanya MWINYI,MKAPA NA JK walitakiwa wakamatwe na kushitakiwa lakini hapa Tanzania tunawashangilia mara tuwaonapo majukwaani akili zetu zimefungwa "TUMEROGWA" nijukumu la viongozi wetu wa dini kuweka maombi kuendelea kuvunja haya maagano ya shetani na CCM.
 

Attachments

  • wazee wa bagamoyo.JPG
    36.4 KB · Views: 117
Woote ni kasumba tu. Mbona hamjadili mwenge wa Olimpiki? Afanyacho mzungu ndio bora, cha mswazi ndio kupoteza muda, Pumbafuuuuu!!
 
Mwenye akili angekuja na Idadi na thamani ya miradi iliyofunguliwa na Mwenge toka tupate uhuru VS Gharama zilizotumiwa na Mwenge. Hii ndio njia ya kisayansi ya kuujadili mwenge !!

Na mawazo kwamba miradi haiwez kufunguliwa mpaka mbio za mwenge ni ya nan?? Na je, nchi zilizoendelea walitegemea mwenge kufungua miradi ili waendelee??
 
Sikuwahi kabla kushuhudia mwenge wa Uhuru hasa mkesha, mwaka huu nikasema nijisogeze nione kuna nini.

Tangu Siku ile najikuta nimeanza kuwa MTU wa hovyo hovyo tu.

Neno la Mungu linasema linasema, "Mkimbiani shetani naye atawakimbia"!
 
Kuna kitu siyo bure, lakini ni imani ya kipumbavu watu wenye akili zao kuendelea kuamini katika hiki kisicho wazi.
 
Mkuu pascal, uliwahi kujiuliza kwanini mwenge haupelekwaji Makanisani na Misikitini kuweka mawe ya msingi au kufungua majengo??
 
Ina maana unataka tuamini kuwa miradi hiyo iliyozinduliwa na mwenge toka uhuru ilijengwa kwa fedha zilizotokana na mapato ya michango ya mwenge ama kodi zetu!
Wakizindua miradi bila mwenge kama wanavyofanya wkt mwingine kuna nn kitapungua!
 
Mwenge ni moja ya uzuzu mkubwa ambao bado unaoendelea nchi hii huku ukigunikwa na uonevu na manyanyaso makubwa kwa wafanyakazi wa Serikali hasa Walimu.
 

Mwenge pamoja na kwamba hauna faida wala manufaa yeyote kwa TAIFA zaidi ya kulea magonjwa tu,na sitashangaa kama 90% ya wakimbiza Mwenge wameshaondoka duniani au ni waathirika wa HIV.

Ukiangalia budget ya Mwenge unaweza kujenga dispensary zenye kiwango cha kati yaani kituo kinachoweza hata kulaza idadi kidogo ya watu na kuwa na mortuary.

Na bado unawachangisha walimu na wafanyakazi wa serikali ili wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapate ulaji wao.

Inshort Mwenge ni chombo cha kupumbaza watanzania,ukitaka kuhakikisha ona UVCCM walivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…