Mwenge wa uhuru wageuka baraka kwa wafanyabiashara Sumbawanga

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Hashimu Arafat Makota, kinyozi katika Manispaa ya Sumbawanga, amesema ujio wa Mwenge wa Uhuru umeongeza fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara kutokana na ongezeko la watu, wakiwemo wageni, hali iliyochochea kuongezeka kwa wateja na kipato chao.

Makota amepinga wanaobeza Mwenge wa Uhuru kwa madai ya gharama kubwa, akieleza kuwa manufaa yake yanaonekana kupitia miradi ya maendeleo inayozinduliwa katika maeneo mbalimbali ya nchi na kuchochea ustawi wa wananchi.
 
View attachment 3689711
Kicheko cha masaa
 
Yaanu msafara unaotumia mabilioni kwa siku halafu ufurahie kunufaisha kinyozi anayepata faida ya 20000?.Nchi hii inavituko sxna
 
Mbio za Mwenge wa Uhuru ni fursa ya kutambua umuhimu wa usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi.

Bi. BALBINA ANDREW mkazi wa jiji la Mwanza ameishukuru Serikali ya Tanzania kutoa fursa kwa vijana katika kushiriki mbio za mwenge. Ameeleza namna mbio za mwenge zinavyosaidia kukagua na kufungua miradi ya kimkakati katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu na miundombinu ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja.

Sambamba na hilo, Bi. BALBINA ANDREW amemshukuru Mhe. Rais DKT. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kuziishi falsafa za muasisi wa mwenge wa Uhuru Mwl. JULIUS KAMBARAGE NYERERE kwa kutoa fursa mbalimbali bila ya kujali itikadi, Dini, Kabila na Jinsia.
 
Kuna haja gani ya kua na mwenge wa uhuru kwa zama izi ilihari mgonjwa anafariki kwakukosa panadol
 
Alama ni sawa, inaweza kubaki kwenye picha tu, ila kukimbiza mwenge hiyo ni ibada ya kichawi ambayo inagharimu taifa mabilioni mengi sana ya pesa na imekuwa chanzo cha kusambaa maambukizo ya ukimwi Tanzania.
 
Bi. EVA MBIRU mkazi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ameishukuru Serikali ya Tanzania kutoa nafasi kwa wakazi wa Rukwa kuidhimisha kilele cha mwenge wa uhuru maana imewapa fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara kutokana na ujio wa wageni wanaotoka maeneo tofauti ndani ya Tanzania
 
Back
Top Bottom