Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa

Halafu wewe ndio unakuja kupewa uongozi au hata ukuu wa mkoa nahisi utachinja sana watu,uongozi ni hekima na busara
Hekima na busara nyingi nchini kwetu ndio zimesababisha mianya ya rushwa, wizi, uzembe, ufisadi nk.

China iliyokuwa inashindwa uchumi hata na Zimbabwe miaka ya 70, leo hii ndio nchi ya pili kwa uchumi duniani, hii yote imewezekana baada ya kuweka mambo ya busara na hekima pembeni. Sasa sisi tutakalia kuzubazwa na mambo ya hekima na busara huku hao wanaotufubaza na mambo hayo ya heshima na busara wakiendelea kutuibia na kujitajirisha wao na familia zao.
 
Acha upumbavu, Maskini mna tabu sana , kwani hilo ni jengo la kwanza kuanguka duniani hii
 
Huyo tajiri uchwara na tamaa za kijinga
Kuna vijana wangapi hawana ajira na wamesoma wangeweza hata kusimamia ila ameoana awape kibarua cha elfu 50 kina maiko
Waarabu huwa wana msemo wa kuwa Bahili huwa wanapata hasara x2
Zile NONDO ukiziangalia wewe hata km sio fundi unashtuka kidogo huyu fundi maiko aliwaza nini kupachika NONDO hizi kwenye jengo linalobeba tani kwa tani za mizigo
 
Mbona Mabasi yanaua Kila siku sijawahi sikia mwenye basi akikamatwa na Mali zake kuuzwa kugawiwa waliopata ajali?
 
Hilo linawezekana kabisa lakini sio kwa awamu hii

Kwanza huyo mmiliki hatawalipa chochote hao wahanga na badala yake yeye ndio atalipwa na kampuni ya bima na mwaka mmoja baadae anaruhusiwa kujenga upya Hilo gorofa lake na ataendelea kufanya biashara kama kawaida.

Nchi ikishakuwa corrupted kwenye Kila sekta tegemea kuona mambo mazito yakichukuliwa kwa wepesi sana.
 
Serikali yako imemkalia kimya sababu inamjua ni mtata na hayupo mwenyewe ana genge lake behind ndio maana husikii hata mmoja anaemnyooshea kidole
Sidhani kama serikali imemkalia kimya sababu ya utata. Hakuna mwenye nguvu mbele ya serikali. Ila naweza kukubaliana na wewe kama utasema kuwa jamaa ana kadi na ni mwanachana kindaki ndaki wa kijani, hapo nitakuelewa.

Ukitaka kujua kama serikali inaweza kumhenyesha jamaa, athubutu kuunga mkono au kufadhili chama cha upinzani wazi wazi ndo utapojua kwamba serikali ni dude la namna gani. Jamaa anaweza kupewa kesi ya uhujumu uchumi au ya uhaini kwamba alitaka kumuua kiongozi mkubwa wa nchi, kupindua serikali nk.
 
Mtanganyika mmoja wapo ni wewe wahi mahakamani ukamfungulie kesi mwenye Jengo uone anavyoinunua mahakama mpaka wewe mwenyewe
Ipo siku Mimi wewe na yule tutabadili fikra na kuamini tunaweza kubadili nchi yetu. Tusi wape nguvu watesi wetu waone akili zetu zimefika mwisho. Ipo siku mahakama zitatenda haki. Ya Mungu ni mengi!
 
Babu Serikali hata kumzungumzia haijathubutu ndio ujue yeye ni dude kubwa kiasi gani
 
Zile NONDO ukiziangalia wewe hata km sio fundi unashtuka kidogo huyu fundi maiko aliwaza nini kupachika NONDO hizi kwenye jengo linalobeba tani kwa tani za mizigo
Majumba mengi hayana ubora ni mda tu tutaona mengi
Hawa waliopewa kazi ya kubomoa ukuta ni wengine maana walianza majuzi tu kubomoa ukuta wa gorofa
Sasa hawa wameambiwa watoe miguu utasimama na nini?
Hao walioweka nondo ni makanjanja wengine
 
Ipo siku Mimi wewe na yule tutabadili fikra na kuamini tunaweza kubadili nchi yetu. Tusi wape nguvu watesi wetu waone akili zetu zimefika mwisho. Ipo siku mahakama zitatenda haki. Ya Mungu ni mengi!
Hio siku ni lini ambayo mahakama itatenda haki? Na hapo unataka kusemaje kwamba mahakama ikamkamate mwenye Jengo na kumfungulia kesi?
 
Majumba mengi hayana ubora ni mda tu tutaona mengi
Hawa waliopewa kazi ya kubomoa ukuta ni wengine maana walianza majuzi tu kubomoa ukuta wa gorofa
Sasa hawa wameambiwa watoe miguu utasimama na nini?
Hao walioweka nondo ni makanjanja wengine
Yaani Jengo walikwangue miguu? Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…