Mwenye Kumbukumbu ya miaka 1974 ya ukame na uhaba wa mazao

Mwenye Kumbukumbu ya miaka 1974 ya ukame na uhaba wa mazao

Alex korosso

Senior Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
126
Reaction score
217
Leo katika pita pita zangu nimekutana na mzee wa makamo nikajaribu kumshilikisha mipago yangu ya kilimo pamoja na utunzaji wa mazao pindi yatakapo panda bei niweze kupata faida.

Mzee ameanza kunipa historia ya kuanzia miaka ya 1974 na kunieleza ya kuwa na uzoefu wa hio biashara kwa mda mrefu.

Amenieleza kuwa miaka inayoishia na nne yani 1974,1984,1994, 2004, 2014 hua aina mvua kabisa ndo maana mazao ya chakula mfano mahindi huwa yanapanda sana bei kutokana na ukame.

Amenishauri kama nataka kuingia kwenye mfumo wa hiyo biashara nisubiri mpaka mwakani yani 2023 ndo ninunue mazao ya kutosha ili mwaka 2024 niweze kupata faida.

Je, niliyoelezwa ni ya kweli au mzee anataka kunichomesha kwa yeyote mwenye uzoefu wa haya mambo anaweza kunisaidia 🙏
 
Huyo mzee atakua mfuasi wa CCM , anaongea bila data.
1974 kulikua na njaa, njaa ile haikusababishwa na ukosefu wa mvua Kama watu wa TANU walivyo waaminisha wananchi kipindi kile.
1973 kulikua na zoezi liitwalo operation vijiji. Watu walilazimishwa na serikali ya TANU kuhama makazi Yao ya asili na kwenda kurundikana kwenye vijiji vya ujamaa.
Mwaka ule watu wengi hawakujihusisha na kilimo kwasababu walikua wanajenga nyumba kwenye makazi mapya (vijiiji vya ujamaa)
Mtakumbuka 1974 kulikua na kipindupindu kikali mmno kilichosababishwa na mrundikano wa watu na ku share maji, ambayo yalikua adimu.
 
Nilikuwa Dodoma mwaka huo ukweli ni kwamba ukame ulikuwa mkubwa mno, zaidi ya kawaida. Usifikiri hatukuwepo. Chuki zako za TANU na sera zake za vijiji vya ujamaa zisikufanye utake kupindisha ukweli.
 
Mzee Said tafadhali kwa hishma na taadhima kama una lolote la kutwambia kama mwanahistoria Nguli namaanisha Mzee Mohamed Said mwandishi popote ulipo tafadhali[emoji122]
 
Back
Top Bottom