Mwenye Kumbukumbu ya miaka 1974 ya ukame na uhaba wa mazao

Punguza ubishi na mahaba yako alichosema ndiyo ukweli, watu walihamishwa kwenye mashamba yao ya muda mrefu na kupelekwa kuanza upya...
 
Taarifa yako siyo kweli kabisa. Operation vijiji ilikuwa mwaka 1973 na wala haikuwa sababu kubwa ya njaa ya mwaka 1974 kwani watanzania wakati huo tulikuwa tunalima, kuvuna na kula mwaka huo huo, yaani hatukuwa na utamaduni wa kutunza chakula. Wakati wa operation vijiji, bado watu walilima na hawakuwa na njaa. Mwaka 1974 kulikuwa na ukame wa kutisha sana, mpaka hata mifugo ilikuwa inakufa kwa njaa. Njaa hiyo haikuikumba Tanzania tu, bali karibu Afrika yote ikiwemo Kenya na ethiopia ambao hawakua na Operation vijiji. Ni wakati huo ndipo Tanzania ikaanzisha National Milling ilin wawe wanatunza mazao kwa ajili ya matumizi ya baadaye, na vile vile ndipo ikaja Siasa ni Kilimo kuhimiza matumizi mazuri ya ardhi kwa kilimo.



Hii ni Article ya April 1974 ikionyesha kuwa Kenya, Ethiopia na Sudan njaa ilikuwa kali.
 
Hapana na mzee ambae ayuko katika siasa za chama chochote tanzania
 
Mzee Said tafadhali kwa hishma na taadhima kama una lolote la kutwambia kama mwanahistoria Nguli namaanisha Mzee Mohamed Said mwandishi popote ulipo tafadhali[emoji122]
Ni furaha sana mzee wetu akijitokeza na kufafanua jambo hili naamini yeye ndo mkongwe wa historia karibu mzee wangu Mohamed said
 
Asante kwa hii mkuu
 

Siku zote imani huja kwa kusikia. Na maisha ya mwanadamu hutawaliwa zaidi na hisia ambazo huweza kuwa kweli au si kweli.
Binafsi sijawahi kushuhudia hizo tofauti hata kwa miaka ya hivi karibuni. Kwahiyo naona kama imekaa kiimani zaidi kuliko kitaalamu.

Hata hivyo, nadhani umefika wakati sasa tuache kutegemea mvua, badala yake zifanyike jitihada za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji. Tz imebarikiwa mito, maziwa na vyanzo vingine vya maji. Ni kuamua tu kuwekeza.
 
Tanzania haijatajwa hapo. Na hizo nchi huathirika sana na ukame.
 
Tutabishana hapa mpaka kuche. Since wewe ni mtu mzima mwenzangu.
Let us agree to disagree.
 
Mkuu mpaka sasa umeshawekeza ekari ngapi za kilimo cha umwagiliaji kwenye hio mito?
 
Nakumbuka wakati huo niko chuo kikuu, mambo yalikua magumu sana
 
Tanzania haijatajwa hapo. Na hizo nchi huathirika sana na ukame.
Tanzania haijatajwa kwa sababu njaa yetu haikuwa kali kama yao, ndiyo maana namshangaa aliyesema tanzania ilikuwa na njaa sana kwa sababu ya operesheni vijiji. Ingawa kuna baadhi ya mikoa Tanzania ilikuwa na njaa sana hasa mikoa ya kati na mikoa ya kaskazini, lakini kulikuwa na mikoa ambayo haikuwa na njaa kabisa. Tulikuza tatizo la njaa kwa vile wengi hawakutambua vitu kama viazi na mihopo kuwa chakula. Kwa hiyo njaa ilitangazwa kwa kukosekana kwa Mahindi, Mchele na Ngano. Lakini bado sehemu kubwa ya nchi ilikuwa na vyakula kama mihogo na viazi.
 
Ukame ulikuwepo sana tu 1973/74. Haukuwa Tanzania peke yake. Njaa ilipiga mpaka nchi jirani. Zoezi la ujamaa villagisation lilianza kipindi hicho cha 1973. Zoezi hili halikuwafurahisha mabeberu ambao hawakutaka Tanzania iwe kitovu cha ujamaa. Wakatumia njaa iliyotokana na ukame kama fursa ya kuonesha kuwa ujamaa haufai. Kwenye media zao na maandiko yao wakasema Njaa hiyo ilitokana na sera za ujamaa hususan, zoezi la villagisation. Bahati mbaya walioamini stori za mabeberu ni wengi sana.

Kipindupindu kimeanza kusumbua Tanzania mwaka 1978. Hakuna uhusiano wa cholera na zoezi la ujamaa villagisation la 1973.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…