Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

Usijiangaishe Kwa masuala ambayo yapo nje ya uwezo wako,hebu jiulize pamoja na kuwaza sanaaa kuhusu Hali ya uchumi wa familia Yako,Je Kuna mabadiliko yoyote? Jibu ni hamna. Muhimu ishi Leo maisha ni mafupi sana unapoishi Kwa stress muhimu zaidi hautaweza kumsaidia yoyote kuinuka kiuchumi kama wewe hujasimama sawa sawa,yaani inakuhitaji wewe kwanza ukae sawa kiuchumi ndipo unanze kumsaidia ndugu,jamaa. Umaskini upo na hautaweza kuumaliza kamwe pambania ndoto zako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sema huu ushauri anahitaji kuufanyia lamination kabisa sema sijui Kama anakuelewa.
 
Umefanya technical mistakes chache, kwaiyo umeanza maisha na handicap ya -2. Sasa fanya machache kurekebisha ili hiyo future unayoiwazia isije kuwa ngumu zaidi!

1. Wewe ni mwanafunzi kazana sana kuboresha matokeo yako ya mwisho boresha hiyo GPA you’ll need scholarship one day it’s very competitive to get handsome scholarship.

2. Mwache Mungu afanye majukumu yake nawewe fanya majukumu yako, halafu waache wazazi wako wafanye majukumu yao. Baba yako na mama yako wanazaa watoto wote hao ilhari Hali hairuhusu lakini unajua wanamuachia nani awatunze hao watoto? Hawakuachii Wewe uwatunze Bali wanamuachia Mungu awatunze, Sasa Wewe kutoa pesa ni njia tu mojawapo Mungu aliyowapa wazazi wako ili kuendesha familia yao, ukiacha kutoa pesa sio kwamba ndugu zako watakufa na njaa, la hasha!

3. Hili la tatu ni gumu sana lakini Ndio la muhimu zaidi ni katika kusimama katika majukumu yako na kuitengeneza hiyo future yako. Ni mwendelezo wa pili, usitoe tena hizo stipends za food and accommodation kuendesha familia yako bali isave Kama unaweza, unaelekea kumaliza chuo utaitaji sana kupiga photocopy vyeti vyako kwa ajili ya kuingia kwenye cycle ya kutafuta temporary jobs, internship, volunteering posts whatever!

4. Wazo la kwenda South Africa temana nalo kwa sasa, na wazo la kujigeuza family hero achana nalo! Jitafute hapa hapa kwa mama utafanikiwa ukijipata Ndio angalia familia yako Ila kujigawa unakofanya sasa utaendelea kuwa masikini na huwenda ukimaliza chuo ukawa mzigo kwa familia yako ambao baadae wanaweza kukukataa!

All the best!
 
Watoto wa Babaako sio wako, wasikuue maana hata ukifa mara 10 hawatapata unachotamani wakipate, soma na maliza then jipange na uwe na subra, ukiwa na haraka utaingia matatani. Babaako pengine hata hawazi wala hana shida ila shida ya watoto wa mtu unajibebesha wewe. Ukitoka kimaisha unaweza kuwasaidia kwa uwezo wako ila kama huna usitake kujibebesha mashida yasiokuhusu. Zingatia ushaur au laah utaiba uchomwe moto au ufe kwa sonona.
 
Pole. Hakikisha unapotoka chuo umeshajua mtaani unaingiaje namaanisha shughuli gani utaifanya. Suala la Ajira ni kizungumkuti kwahiyo wewe weka degree yako mfukoni piga kazi yoyote mpaka upate panapoeleweka.
 
Back
Top Bottom