Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

Unajipa msongo wa mawazo wa nini, kama una wadogo zako wa kiume above 16 na wanafanya mchezo na shule hao wasikuumize kichwa kila mtu atabeba msalaba wake

Watoto 9, Balaa sana aisee
 
Kwa hili bandiko lako Nina uhakika hata mama manunu akikaa uchi mwenge hauwezi kumlika mafisadi😎😎😎😎jutahidi tafuta demu anaipiga vizinga utanishukuru baadae
 
Mtoto mdogo kama wewe unakataje tamaa kijana!
Simama pambana life isn't easy
Wewe ni Mwanaume
Men are fighters of their dreams .
Kaa kiume Mura.
Battles are won in the hearts of men.
Kaza Mtoto wa kiume
Acha uoga kaza na jiamini kuwa unaweza.
 
Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima. Niende kwenye mada moja kwa Moja.

Mimi ni Kijana wa kitanzania na hivi sasa nipo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania jijini Dar es Salaam, nachukua shahada ya kwanza ya ualimu sayansi.

Natoka katika familia ya kawaida sana yenye jumla ya watoto tisa huku mimi ni wa kwanza yaani first born.

Hali ya uchumi ya wazazi ni duni sana hadi kufika hapa kwa Kweli ni kwa neema tu, kiufupi familia na wadogo zangu nane wananitazama mimi kama mkombozi. Hali unanifanya niishi kwa msongo mkali sana wa mawazo.

Nawaza sana mwakani nitakapomaliza chuo maisha yangu yatakuwaje? Familia na wadogo zangu tawashikaje mkono? Moyo wangu una madonda mabichi sana.

Nilibahatika kupata mkopo wa elimu ya juu lakini kwa hali ya nyumbani pesa yangu ya meals and Accomodation yaan boom huwa naikata mara mbili nusu nabaki nayo nusu natuma nyumbani.

Wanabodi nahisi maneno haya hayawezi eleza nachotaka kufikisha kwenu.

Na umri mdogo lakini sonona nahisi inanitafuna. Nataman nikimbilie South Africa kujaribu bahati yangu.

Muwe na asubuhi njema, hapa nipo njiani naelekea shule maana tupo Field lakini akili haipo Sawa.

Kwa uzoefu wangu. Haya ndo yanakujenga..Mara nyingi mwisho huwa mzuri, mtihani ni kuvumilia tu.
 
wanafunzi wanapigwa sana mashuleni sikuizi,,, ukifatilia kiundani zaidi utaona shida ni mwalimu na stress zake anahamishia kwa watoto bila sababu..ndomana nimemtahadharisha tu hapo
Neno "kutuchapia watoto" lilitafsiriwa vibaya.
 
Yaani unajipa stress kisa watoto waliozaliwa na mtu mwingine? Come on

Ukweli ni kuwa bado wewe ni kapuku sana kuwa first born haikufanyi ubebe majukumu yasiyokuhusu jitafute wewe mwenyewe ukijipata ndiyo hangaika na hao nduguzo but mbali na hapo ipambanie future yako acha kiherehere kwenye mambo yasiyokuhusu .

Ni ushauri tu maana unajipa stress vitu vya kijingakijinga lakini kwenye orientation uliambiwa hela ya accomodation na meals ni ya kuwatumia wazazi ??

Acha ujinga stress unajitafutia ww mwenyewe kwani kabla ya kupata mkopo hao watoto na wazazi wako waliishije? Tafakari mdogo wangu .

Lakini vipi nasikia eti kipa wa Simba mbarazil haruhusiwi kucheza bongo hivi ni kweli kaka mkubwa ?

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Naona unarahisisha maisha boss,

Unafikiri ni rahisi kiasi hicho kuwatelekeza wapendwa wako wanaokuangalia?

Situation ya jamaa ni ngumu mno,kama haujawahi pitia situation ya namna hiyo hauwezi kuelewa.

Kosa nililoliona kwa mtoa mada ni moja tu 'kuwa hofu na hali hasiyo ijua'

Yeye haondoe hofu kwa sababu itafanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Mungu yupo na anaijua hali yake
 
Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima. Niende kwenye mada moja kwa Moja.

Mimi ni Kijana wa kitanzania na hivi sasa nipo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania jijini Dar es Salaam, nachukua shahada ya kwanza ya ualimu sayansi.

Natoka katika familia ya kawaida sana yenye jumla ya watoto tisa huku mimi ni wa kwanza yaani first born.

Hali ya uchumi ya wazazi ni duni sana hadi kufika hapa kwa Kweli ni kwa neema tu, kiufupi familia na wadogo zangu nane wananitazama mimi kama mkombozi. Hali unanifanya niishi kwa msongo mkali sana wa mawazo.

Nawaza sana mwakani nitakapomaliza chuo maisha yangu yatakuwaje? Familia na wadogo zangu tawashikaje mkono? Moyo wangu una madonda mabichi sana.

Nilibahatika kupata mkopo wa elimu ya juu lakini kwa hali ya nyumbani pesa yangu ya meals and Accomodation yaan boom huwa naikata mara mbili nusu nabaki nayo nusu natuma nyumbani.

Wanabodi nahisi maneno haya hayawezi eleza nachotaka kufikisha kwenu.

Na umri mdogo lakini sonona nahisi inanitafuna. Nataman nikimbilie South Africa kujaribu bahati yangu.

Muwe na asubuhi njema, hapa nipo njiani naelekea shule maana tupo Field lakini akili haipo Sawa.
Una mwandiko mzuri
 
Wew unamiaka mingap
Wadogo zako wanamiaka mingapi ki umri
Hasa watatu wamwisho
 
pole sana ndugu chakukushauri jikomboe kwanza wewe ukishajikomboa ndipo ukumbuke kuokoa wengine,we mwenyewe una hitaji ukomboz af tena dah...saidia pale unapoweza kila jicho litajililia ,tuliza akili,soma na elewa baada ya kumaliza na kufanikiwa ndo uje uwainue ndugu zako,umekosea sana kwa kuiaminisha familia yako uko vizuri.....jitahidi kuwa unalialia ili waamini bado unasota hujatoka kimaisha,wanalia shida kidogo tayali ushatuma pesa unawazoesha vibaya sikufundishi roho mbaya, ila inawezekanaje mateka kumkomboa mateka mwenzake ili hali nayeye ametekwa naye yupochini ya ulinzi kama walivyo mateka wenziye?...usilaumu waambie hali halisi kwamba nawewe hali ngumu safari bado...au we ni wale akifika hom misifa kibao suti kubwa mixa travota,malaptop ohh sisi bwana tunasoma huku tunalipwa sifa za kipuuzi matokeo yake unawajengea picha ushafanikiwa,hatimaye unakuwa kimbilio kwa shida zao....waaminishe kwamba bado nawewe unasota...kipindi kabla hujapata boom au univasity walikuwa wanaishi vipi? wewe ndo ulikosea
 
Ushauri mzuri,lakini mkuu kuwaaacha sio rahisi..naongea kitu ambacho nakijua.

Na mtoa mada anapoongelea kutegemeka nafikiri anaongelea kutegemeka katika basic needs ie foods,clothes and may be shelters.

Ni vitu vidogo lakini kwa familia kubwa kama hiyo,ni jambo kubwa kuwahakikisha hayo mahitaji ambayo ni ya lazima.

Mtoa mada hazungumziii fate ya kila mwanafamilia,anazungumzia kutegemeka katika basic needs..je hawaache?

Alafu suala la kugemeka sio suala la hiari,yaani ni mazingira yanakualazimu
 
Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima. Niende kwenye mada moja kwa Moja.

Mimi ni Kijana wa kitanzania na hivi sasa nipo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania jijini Dar es Salaam, nachukua shahada ya kwanza ya ualimu sayansi.

Natoka katika familia ya kawaida sana yenye jumla ya watoto tisa huku mimi ni wa kwanza yaani first born.

Hali ya uchumi ya wazazi ni duni sana hadi kufika hapa kwa Kweli ni kwa neema tu, kiufupi familia na wadogo zangu nane wananitazama mimi kama mkombozi. Hali unanifanya niishi kwa msongo mkali sana wa mawazo.

Nawaza sana mwakani nitakapomaliza chuo maisha yangu yatakuwaje? Familia na wadogo zangu tawashikaje mkono? Moyo wangu una madonda mabichi sana.

Nilibahatika kupata mkopo wa elimu ya juu lakini kwa hali ya nyumbani pesa yangu ya meals and Accomodation yaan boom huwa naikata mara mbili nusu nabaki nayo nusu natuma nyumbani.

Wanabodi nahisi maneno haya hayawezi eleza nachotaka kufikisha kwenu.

Na umri mdogo lakini sonona nahisi inanitafuna. Nataman nikimbilie South Africa kujaribu bahati yangu.

Muwe na asubuhi njema, hapa nipo njiani naelekea shule maana tupo Field lakini akili haipo Sawa.
Maisha yako anayajua mungu sisi hatujui
 
Aliye wazaa alikuwa anawazaa wote 9 bila hofu na bado hana hofu,wewe unapata hofu
🤣🤣🤣....halafu huyu mzazi inaonekana bado anazaa....manake kama first born ndo yupo chuo inamaanisha yupo kwenye 20's..Wala hajali..
 
Ukipiga hesabu ya kuangalia walimu wanavyo sota kitaa hapo ndo nguvu inakata kabisa.

Kwanini unaiwazia kesho ajuaye MUNGU Mkuu usuruhusu Mawazo kaama hayo yachukue nafasi kichwani mwako, kigumu Focus na ulicho nacho tena Bora yako wewe hata upo chuoni unachukua shahada, wengine ni ma First Born hatuna hata Elimu ya Secondary lakin tunakomaa maisha yanasonga,so why wewe ujipe stress kwa kitu ambacho Bado hujakifikia.

Kingine usijidanganye ukaenda South Africa, aisee utarudi maiti wale jamaa wanauna kama mtu anachinja kuku, na utambue SA ni Nchi ya kwanza ambayo inaongoza kwa Mauji Africa na pia hata Duniani kwenye zile nchi Top SA ipo so Kuwa makin wale jamaa ni makatiri sana.

Kila la kheri
 
Back
Top Bottom