Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

..... Moyo wangu una madonda mabichi sana.
Kitu cha kwanza ,punguza uzushi na kukuza mambo.Moyo wako na hayo madonda mabichi muda huu ungekua ICU.

Pili punguza woga, deal na the current issues kwanza, hayo ya baada ya kumaliza chuo una uhakika gani kama utamaliza hiko chuo ukawa mzima

Tatu, sio kwamba hao ndigu zako wanakuona kama ndio mkombozi wao .Maana kila mtu ana destiny yake.Ishi maisha yako kwanza. Msaada wa kwanza kuwapa hao ndugu zako na wazazi wako ni wewe kwanza kujiweza na kujimudu bila kuwa mzigo kwao.Huo ndio msaada wa kwanza wa msingi.Mingine inafuata.

Nimemaliza
 
Pambana mkuu mpaka tone lako la mwisho la damu.
Mungu atusimamie wapambanaji wote kutoka katika maisha duni regardless madhambi mangapi tunayomtendea.
 
Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima. Niende kwenye mada moja kwa Moja.

Mimi ni Kijana wa kitanzania na hivi sasa nipo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania jijini Dar es Salaam, nachukua shahada ya kwanza ya ualimu sayansi.

Natoka katika familia ya kawaida sana yenye jumla ya watoto tisa huku mimi ni wa kwanza yaani first born.

Hali ya uchumi ya wazazi ni duni sana hadi kufika hapa kwa Kweli ni kwa neema tu, kiufupi familia na wadogo zangu nane wananitazama mimi kama mkombozi. Hali unanifanya niishi kwa msongo mkali sana wa mawazo.

Nawaza sana mwakani nitakapomaliza chuo maisha yangu yatakuwaje? Familia na wadogo zangu tawashikaje mkono? Moyo wangu una madonda mabichi sana.

Nilibahatika kupata mkopo wa elimu ya juu lakini kwa hali ya nyumbani pesa yangu ya meals and Accomodation yaan boom huwa naikata mara mbili nusu nabaki nayo nusu natuma nyumbani.

Wanabodi nahisi maneno haya hayawezi eleza nachotaka kufikisha kwenu.

Na umri mdogo lakini sonona nahisi inanitafuna. Nataman nikimbilie South Africa kujaribu bahati yangu.

Muwe na asubuhi njema, hapa nipo njiani naelekea shule maana tupo Field lakini akili haipo Sawa.
Ukiwa na akili timamu lazima uishi na changamoto,relax.Mambo yakikuzidia unakosa majibu yake tulia yajipange menyewe Mungu atakuletea jibu. Saidiaa ndugu zako huku ukibalance msaada wako usiumize maisha Yako hususani kama wazazi wako hi na hawaumwi. Huwezi ndugu wafanya waishi maisha super ilihali hutengenezi future Yako.
 
Kwann usiitumie hio nguvu kazi ya hao ndugu zako shambani,lima mazao yenye Uhakika wa kuvuna hata kwa mvua ndogo mfano kunde, karanga,haya mazao demand yake kwa mjini ni kuwa kilo moja ya karanga lishe ufika hadi elf 4.
Kunde si chini ya elf 2 kilo.
Heka moja unavuna gunia 8-10.
Lima Heka 20.
Ukute ndugu ni wamakonde,asubuhi tu wapi migundinii hahaha wanatia hasraa Sanaa.
 
"Nilibahatika kupata mkopo wa elimu ya juu lakini kwa hali ya nyumbani pesa yangu ya meals and Accomodation yaan boom huwa naikata mara mbili nusu nabaki nayo nusu natuma nyumbani."
Hapo nilipoquote ndipo lilipo kosa lako.Ukweli ni kuwa mtaani hakueleweki na si rahisi,hizo ajira zenyewe hakuna.Ngoja nikupe mfano .Mpwa wangu alichaguliwa kujiunga UDOM kutoka mazingira magumu kama Yako.Tofauti na wewe,yeye aliamua kujiongeza baada ya kuona hatatakuwa na cha kufanya baada ya kumaliza madomo.
Alichofanya aliamua kutumia pesa ya booom kununua vifaa nya saluni,na akakamilisha.Hii ni pamoja na kununua contena na kulidizaini kama saluni.Pia aliniomba nikamsajilia line za Tigo pesa na M-PESA akaanza kutoa huduma huku anasoma.Mpaka anamaliza chuo tayari ofisi ilikuwa imekamilika.
Hukupaswa kutumia pesa ya boom kwa kuituma Nyumbani iliwe tu,bali ungeangalia mbele zaidi.Kama Bado unayo akiba angalia cha kufanya badala ya kuila.Hivi tunavyozungumza mpwa wangu alimaliza chuo na hakurudi Nyumbani ,alibaki Dodoma na anaendelea kupambania maisha yake.At least ana kitu cha kufanya badala ya kukas jobless.
 
Kwanza nikupe hongera kwa kutambua changamoto zako maana hapo umesolve nusu ya hizo changamoto
Ila approach uliyotumia ndio umekosea, huwezi kutuma nusu ya boom lako nyumbani ukahisi unaweza kutatua hizo changamoto hapo ni kuendelea kujiingiza zaidi kwenye lindi la umasikini
Kama umeweza kama nusu ya bumu lako
1 save hiyo hela na tafuta kitu cha kufanya iwe mpesa, au kuwa mobile Stationary wasaidie kuprint unaosoma nao hata kwa faida kidogo
2. Tafiti na tafuta mashirika ujiunge na program zao hasa zile exchange, volunteering programs na uone unaweza navigate vipi kupata fursa huko
3 tafuta mashule ya binafsi uombe hata kufundisha hasa weekend days kujijengea nafasi
Nina mengi Sema muda wa kutype ndio changamoto
Inshort jiongeze, kujifungia chuo na kupiga msuli sana bila kubuild connection kwenye real world itakuwa changamoto kubwa kuliko hata hao ndugu zako
 
South hakuna mishe saizi mdogo wangu, Zamia Namibia, kama uko determined unatoboa. Kule at least kazi zipo. Hopefully mambo yatakaa sawa tu kwako with time. We all have been through that at one point, heads up.
 
Aliye wazaa alikuwa anawazaa wote 9 bila hofu na bado hana hofu,wewe unapata hofu
Nilitaka kusema hili nikaona nitamuongezea uchungu mtoa mada. Yeye apambane tu atatoboa...
Ila huwa inashangaza sana mtu hana uwezo anazaa watoto wengi namna hiyo.

Yaani jamaa anatunza wadogo zake 8 pamoja na wazazi , hapo bado yeye hajaanzisha familia yake.
 
Niombee Mungu nipate fedha za kufungua ka shule ka English Medium nikupe ajira mwaka 2025

Wanasema "Undugu kufaana na sio Kufanana"
 
Ukishamaliza chuo, usije mtaani ukajiona wewe ni msomi na ukadharau vijana ambao hawajaenda shule. Hapo utalaaniwa na ulimwengu utakufundisha adabu.

Na kuhakikishi hao vijana ambao hawajaenda shule au kufika level uliyopo wewe ndiyo watakua walimu wako bora sana wa kukufundisha maisha ya kujitegemea na wakati mwingine kukupadili za hela ya kununua hata mswaki, na hao ndiyo watakua ndugu zako na marafiki zako wa kweli.

kama unaweza chukua masomo ya jioni anza kujichanganya na vijana wanaopambana mtaani piga nao hata vibarua, ingia kwenye makampuni ya ulinzi linda day ukutane na watu wengi jioni nenda kapige kitabu, piga vikazi vya hapa na pale unajenga kufahamika sana na usiangalie wezako chuoni watakuonaje.

Ili siku ukihitimu chuo unakua na elimu mbili ya darasani na elimu ya maisha halisi ya duniani na wakati mwingine unakua na connection ya vihela hela hata vya kununulia vocha, Kuliko utoke chuo uje uanze upya kitaa.

Waheshimu sana uliowaacha mtaani na pia usikate tamaa kivyovyote vile. Ukiona maisha hayaendi jua wazi kabisa ndiyo utu uzima huo na usikate tamaa kamwe.

Amini katika kufanya kazi na usiamini miujiza, maisha tunaanzia chini hauwi navyo tuu gafla unatafuta kidogo kidogo,

Ukiwa na deni usiamini katika kuombewa kufuta deni kimuujiza amini kufanya kazi na kulipa deni la watu

Pia kumbuka sana Mwamini Mungu hatakama hatokujibu kile unacho muomba , kumbuka Mungu atabaki kua Mungu tuu haijalishi utapitia magumu kiasi gani. Mungu yupo anakuona siku zote
 
Back
Top Bottom