Akili huwa inafikia mwisho wakati mwingine maana ina ukomo, ni logic, ndivyo ulivyoumbwa, kwa uliyoyasema nakuelewa sana.
Ila akili zinapofikia mwisho kuna matuamini, kuna Neema, ambayo inatoka na ahadi za Mungu na hizo ndo kimbilia.
Maisha utakayoishi kutoka sasa mpaka umalize chuo yataamua uendelee na sonona au uso utakate na ufanikiwe.
Mimi kama Mkristo, nikiwa na hali kama yako, tumaini langu huwa katika ukiri wa neno la Mungu tu na hivyo huona matokeo.
Imani ni jambo la Muhimu sana kwa mwanadamu, maana uwezo wake una mwisho, ila ana roho na access ya kuunganishwa na ulimwengo usio na mipaka.