Umefanya technical mistakes chache, kwaiyo umeanza maisha na handicap ya -2. Sasa fanya machache kurekebisha ili hiyo future unayoiwazia isije kuwa ngumu zaidi!
1. Wewe ni mwanafunzi kazana sana kuboresha matokeo yako ya mwisho boresha hiyo GPA you’ll need scholarship one day it’s very competitive to get handsome scholarship.
2. Mwache Mungu afanye majukumu yake nawewe fanya majukumu yako, halafu waache wazazi wako wafanye majukumu yao. Baba yako na mama yako wanazaa watoto wote hao ilhari Hali hairuhusu lakini unajua wanamuachia nani awatunze hao watoto? Hawakuachii Wewe uwatunze Bali wanamuachia Mungu awatunze, Sasa Wewe kutoa pesa ni njia tu mojawapo Mungu aliyowapa wazazi wako ili kuendesha familia yao, ukiacha kutoa pesa sio kwamba ndugu zako watakufa na njaa, la hasha!
3. Hili la tatu ni gumu sana lakini Ndio la muhimu zaidi ni katika kusimama katika majukumu yako na kuitengeneza hiyo future yako. Ni mwendelezo wa pili, usitoe tena hizo stipends za food and accommodation kuendesha familia yako bali isave Kama unaweza, unaelekea kumaliza chuo utaitaji sana kupiga photocopy vyeti vyako kwa ajili ya kuingia kwenye cycle ya kutafuta temporary jobs, internship, volunteering posts whatever!
4. Wazo la kwenda South Africa temana nalo kwa sasa, na wazo la kujigeuza family hero achana nalo! Jitafute hapa hapa kwa mama utafanikiwa ukijipata Ndio angalia familia yako Ila kujigawa unakofanya sasa utaendelea kuwa masikini na huwenda ukimaliza chuo ukawa mzigo kwa familia yako ambao baadae wanaweza kukukataa!
All the best!