Mwenye Nyumba ameleta mganga wa kienyeji anatulazimisha tulambe unga anahisi kuna mchawi kwenye nyumba yake

Madhara ya kupanga uswahilini.
Alie kwambia washirikina wapo uswazi tu nani.... Kuna nyumba nilikaa uzunguni Dom... Fence tu imepakana na nyumba moja ya muhimili, upande mwingine taasisi kubwa tu na upande wa pili wa barabara hao hao watumia vingora wakienda kazini...... lakini hiyo nyumba kwa ushirikina mwenye nyumba alikuwa kinara..... Mara aoge uchi mchana,mara usiku wazunguke kumwaga dawa, mara waje kumwaga maji kwenye nyumba sijui ndo dawa!!!!!

Kikubwa usilambe...utajiingiza kwenye maagano yao... kama yeye mganga kweli aonyeshe.
 
Madam kuoga uchi, kumwaga dawa sisi haituhusu kama nyumba YAKO, tunachokataa ni KULAMBA UNGA. Chuo tulikaa na mmama huyo mwenye nyumba yule mama hata awaone mnafanya mapenzi uwani hawasemeshi ILA kodi YAKe ikifika msitafutane๐Ÿ˜‘๐Ÿ˜‘ tunakaataa KULAMBA UNGA
 
Sema nyumba zenye changamoto kama hizo huwa zinakupa presha ya kujenga mimi niliamia kwenye banda langu bila madilisha kwa hasira ya visa vya wenye nyumba zao๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Hongera sana rafiki, uzuri wewe akili unazo za kutosha.. wengine wanapitia hizo changamoto ila wanakuwa wazito kufanya maamuzi.. Bora ukae kwako hata kama hakuna mlango ila kwako.. Hapo umemaliza labda uje kuwa mnoko kwa wapangaji wako kama utapangisha ,๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Nimechukua ushauri wenu wakuu, nitaufanyia kazi na nitaleta mrejesho... asanteni ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Usilambe huo UNGA utakuwa TEJA shaulilo๐Ÿ˜‰๐Ÿ˜‰
 
Limbwata Hilo,..Shtuka usilambe,..utajikuta mshahara wako wote unaishia kwake๐Ÿ˜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ