Update ni kwamba Stiglers Gorge inaendelea vizuri. Sema maji yamejaa yamesababisha kusimama kwa uchimbaji wa diversion tunnel, mvua ikikata maji yakaisha kazi inaendelea kama kawaida. Kwa hili serikali inapaswa kupongezwa.
SGR pia ni project nzuri, iwapo itakamilika tutaona matunda yake. Kwa sasa hii ya Morogoro Dar iko karibu 80% na natumaini kufikia December mwaka huu itakua tayari. Ile ya Moro Dom iko 30%, 2024 au kabla ya hapo itakamilika.
Katika project naunga mkono na nafuatilia ni hizi kwa sababu zina long term benefits kuliko nyingine zote.
Wangalau ww umejitahidi, sio kwamba umeongea ukweli kwa maana ya ukweli, lakini umejaribu kuja na data za hapa na pale. Hilo la SGR kwa sasa ngoja tukuache ili usitake kuandika uongo ili kuua soo. Lakini sioni bwawa hilo lilikamilika wakati Magufuli akiwa madarakani hata kama atapata miaka mitano tena.
Hiyo SGR hata mimi sikatai kuwa ni project nzuri, ila approach aliyotumia Magufuli ya kusaka kiki badala ya kuendelea na mbinu ya JK ya mkopo toka mwanzo, hapo alichemsha kitu ambacho sioni akikamilisha kabla ya kutoka madarakani. Unasema hiyo reli Dar+ Moro iko 80%, ila unasema huenda kufikia December itakuwa tayari. Hilo neno huenda lenyewe linaleta shaka kubwa. Nina shaka sana iwapo Magufuli mpaka anatoka madarakani iwapo hiyo reli itakuwa imevuka Dodoma. Sioni hilo lilitokea, kwani Magufuli ana nia ya kukamilisha hiyo reli kabla ya kutoka madarakani, lakini nia pekee haitoshi, kikubwa ni mbinu ya kufanya hivyo.
Siku za nyuma niliwahi kuandika humu wakati hiyo miradi ikipigiwa debe kubwa, na Magufuli kusifiwa kuwa ametekeleza jambo ambalo lilikuwa ni upotoshaji mkubwa, aidha wa makusudi au mihemko. Kwanza miradi hakuwa ametekeleza, bali aliouonyesha udhubutu. Ni kweli ni mtu mwenye uthubutu na mchapakazi kazi kwa asili yake, ila sio mtu mwenye mbinu za anachotamani. Nilisema Magufuli hana uwezo wa kupata 15t ndani ya miaka 5+5 ya utawala wake, huku miradi na mahitaji mengine yakiendelea. Aina ya utawala wake haimfanyi kupata hizo pesa kwa muda atakaokaa madarakani, na hata akipata mikopo kiasi fulani, basi itakuwa ni yenye riba kubwa, na masharti magumu.
Ni dhahiri kabla ya muda wake kuisha atakuwa anakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni, je atakuwa analipa madeni au kutekeleza miradi hiyo ya gharama kubwa? Sioni anatoboa vipi.