Mwenye ushahidi au maelezo toshelezi jinsi Katiba ilivyomletea umasikini/utajiri

Mwenye ushahidi au maelezo toshelezi jinsi Katiba ilivyomletea umasikini/utajiri

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Nimekaa sehemu na watu makini wanabishana Katiba ilivyoathiri maisha yao na mimi nimepata cha kuuliza kwa wakuu humu.

Binafsi nikijipima sioni jinsi ilivyoathili maisha yangu. Ninawajibika kwa hivi nilivyo. Nikiwa nabidii nafanikiwa tu bila hata kujua habari za saa mbili au hotuba ya Rais imesemaje au Bunge limeamua nini.

Nikiwa mvivu, mpuuziaji, huwa nafulia tu. Huenda upeo wangu umeanza kufubaa.

Unaweza kueleza kwa lugha rahisi tu jinsi Katiba hii imekuletea umasikini au utajiri au kama haijakuathili chochote.
 
Ushahidi huo hapo

Capture-Uvuvi.PNG


Uongozi.jpg
 
Mimi Niko neutral.
Nahoji maelezo yako.
Natafuta connection na katiba naikosa. Ukiunga inakuwa vzr mkuu.
Lakini nashukuru Sana Kwa mchango
Nimekuonesha MATUNDU ya ubovu wa katiba, wewe unatetea wezi. Huko yuvisisiemu hamjawahi kufundishwa neno UADILIFU kabisa, sivyo? Endelea na uchawa wako ndugu
 
Kenya walipata katiba mpya miaka kadhaa iliyopta, je katiba hiyo imemaliza njaa na umasikini kwenye taifa lao? Je gap kati ya matajiri na masikini limeisha? Je ajira zimeongezeka?

Mimi ninachoona Taifa ili lisonge mbele pamoja na ustawi wa maisha ya watu tunahitaji viongozi bora wenye kuumizwa na shida za wananchi. Leo hii hata tukipata katiba mpya sidhani kama itabadilisha maisha ya raia kama viongozi watakuwa sio wazalendo.

Kwa sasa naona katiba inadaiwa na wanasia sana kuliko raia wa kawaida tafsiri yake ni kwamba raia wanatambua kuwa shida haipo kwenye katiba.

Ni hatari sana kuwa na katiba ambayo wanasiasa na vyama vyao wanataka kuingiza maslahi yao. Katiba tuliyonayo ni bora sana kama vyama vitatuletea wagombea bora, na katiba bora zaidi itapatikana ikiwa itaundwa na wananchi wenyewe na sio kwa msukumo wa wanasiasa na vyama vyao.
 
Kenya walipata katiba mpya miaka kadhaa iliyopta, je katiba hiyo imemaliza njaa na umasikini kwenye taifa lao? Je gap kati ya matajiri na masikini limeisha? Je ajira zimeongezeka...
Sio kazi nyepesi kuchomoa ndani ya MILKSHAKE wezi wa mali za umma, wako tayari kufia hapo... katiba mpya ni sasa

Uongozi.jpg
 
Kumbe tunabishana na mtoto mdogo hapa? Wewe ni muha wa Kigoma, sivyo? Unashindwaje kuelewa kwamba katiba imara inaleta uwajibikaji? Kiongozi akijua anaweza kuchukuliwa hatua muda wowote ule, anaweza kufanya UHALIFU wa wazi wazi?

Haya wahi kuchukue elfu saba yako sasa
Usijibu kwa mihemko hapa tunajadili so weka jazba pembeni. Katiba ya sasa haizui viongozi kuwahibishwa na ndio maana kuna sheria ambazo zimetokana na sheria mama ambayo ndio katiba ambazo ndio mahakama hutafsiri kuwahukumu hao waliokwenda kinyume kwenye utendaji wao ndio narudia kusema tunahitaji viongiozi bora.

Kupitia katiba hii hii tumeshudia mafisadi wakipelekwa mahakamani, tumeshudia wazembe wakitumuliwa kazini, tumeshuhudia mali hasili zikilindwa na kulinufaisha taifa sasa hapo tatizo ni katiba au ni wale wanaosimamia katiba.
 
Kenya walipata katiba mpya miaka kadhaa iliyopta, je katiba hiyo imemaliza njaa na umasikini kwenye taifa lao? Je gap kati ya matajiri na masikini limeisha? Je ajira zimeongezeka...
Wakenya wape muda kidogo, Kenya ule upuuzi wa Raisi kuzima internet nchi nzima kama alivyowafanyia Magu au watu kama Makonda na Sabaya kuweka watu ndani bila mashtaka wamesahau sasa and it will never come back, pesa wanakusanya inatumika ilipokusanywa kwa utaratibu mzuri sio chama cha siasa kinaamua, kuna mengi watafanikiwa kutokana na check and balance waliyoiweka kwenye katiba, na media sasa zina nguvu kuongea bila woga kitu ambacho ni muhimu sana kwa ustawi wa nchi inayofuata haki
 
Wakenya wape muda kidogo, Kenya ule upuuzi wa Raisi kuzima internet nchi nzima kama alivyowafanyia Magu au watu kama Makonda na Sabaya kuweka watu ndani bila mashtaka wamesahau sasa and it will never come back...
Swali kwenye uzi hujalijibu mkuu. Hayo uliyajibu yanamafuaa kwa wanasiasa vipi kuhusu kuodoa njaa na unasikini?
 
Katiba mpya maana yake wanasiasa wanataka kugawana vyeo, unasikia Chadema wanataka serikali za majimbo, huko wanatengeneza vyeo vipya.

Mbona watu ni matajiri na tunawaona na kwa katiba hii hii, mfano Mbowe na baba yake, tangu katiba ya mkoloni Wana pesa.
 
Swali kwenye uzi hujalijibu mkuu. Hayo uliyajibu yanamafuaa kwa wanasiasa vipi kuhusu kuodoa njaa na unasikini?
Huoni manufaa ya media zenye nguvu na zilizo huru zinazoweza kuibua ufisadi bila woga na watu wakawajibika? huoni kuna kasoro kama mtu mmoja anaweza kuzima internet nchi nzima? unaona sawa mwanasiasa kama mkuu wa wilaya kukuweka ndani bila mashtaka?
 
Back
Top Bottom