Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Sidhani kama vichwapanzi wanaweza kukuelewa
Mimi hapa nimekuwa masikini wa kutupa kutoka katika maisha ya kawaida Kwa sababu ya katiba mbovu. Nilikua na Nyumba zangu mbili kimara zikavunjwa na sasa naishi uchochoroni Tandale uzuri, nimepanga chumba kimoja tu nalala chini sina chochote mali zangu zoote zilipotea hapa nilipo nimechoka na kupauka kama kipande cha muhogo mkavu
Nyumba zangu zilivunjwa kutokana na maamuzi ya Raisi kichaa aliyepewa madaraka makubwa na katiba iliyopo. Katiba ya sasa iliyompa nguvu ya kuamua anavyotaka yeye na hakuna wa kumfanya lolote Kwa sababu tayari anakua ana nguvu kuliko sheria au kuliko mfumo mzima uliomuwrka kwenye madaraka hayo
Nyumba zilivunjwa licha ya kesi kuwa ipo mahakamani kwenye zuio. Nilikua na biashara ya maduka katika Nyumba zote hizo iliyoniingizia kipato cha kuendesha maisha yangu na familia yangu kwa ustawi na muelekeo wa maendeleo kieleimu, kiuchumi na kijamii katika ngazi ya familia ambayo ilisimama katika misingi ya malezi bora na muelekeo chanya
Lakini bahati mbaya kutokana na katiba mbovu iliyo toa nafasi ya kuvunja haki ya utu wa mtu Kwa sababu ya ukubwa wa maamuzi ya kimadaraka aliyopewa Raisi. Baada ya kuvunjiwa nyumba Familia yangu yote ilisambaratika binti yangu kwa sasa anaishi kwa bwana na tayari ana watoto wawili akiwa na umri wa miaka 17 tu. Kijana wangu wa kiume sasahivi ni muokota chupa na siso huku akiwa nimtumiaji mzuri wa mihadarati
Watoto wangu wote walikatisha masomo wakiawa katika umri mdogo wa elimu ya msingi na kupoteza ndoto zote walizokuwa wakiziota kielimu, maisha yao yamepoteza dira wakiwa wanaishi kwa kubahatisha kama mimi baba yao huku nikiwa sina tena nguvu wala uwezo wa kuwasaidia Kwa sababu mimi mwenyewe sijielewi nimevurugwa kukucha nashinda hospitali kupambana na presha na sukari vilivyoanza baada ya kupoteza msingi wa maisha yangu
Haya yote ni matokeo ya kupoteza dira ya maisha baada ya kuvunjiwa Nyumba. Familia yangu ilisambaratika tukakosa sehemu ya kuishi mali zangu zote zilipotea ikiwemo vitu vya ndani watoto wangu walikwenda kuishi kwa rafiki wa Mama yao aliekuwa akiishi Tandale kwa mtogole huku Mama mtu akijaribu biashara ya Samaki feri iliyopelekea kupata bwana wa kumstiri na ndoa kuvunjika Kwa sababu mimi nilikua nimesha pagawa
Kwa kifupi ushahidi huo unakutosha kuanzia sasa jua kuwa KATIBA na MAISHA ni sawa na chumvi na mboga mpunbavu wewe