Mwenye ushahidi au maelezo toshelezi jinsi Katiba ilivyomletea umasikini/utajiri

Mwenye ushahidi au maelezo toshelezi jinsi Katiba ilivyomletea umasikini/utajiri

Nimekaa sehemu na watu makini wanabishana Katiba ilivyoathiri maisha yao na mimi nimepata cha kuuliza kwa wakuu humu...
Mimi hapa nimekuwa masikini wa kutupa kutoka katika maisha ya kawaida Kwa sababu ya katiba mbovu. Nilikua na Nyumba zangu mbili kimara zikavunjwa na sasa naishi uchochoroni Tandale uzuri, nimepanga chumba kimoja tu nalala chini sina chochote mali zangu zoote zilipotea hapa nilipo nimechoka na kupauka kama kipande cha muhogo mkavu

Nyumba zangu zilivunjwa kutokana na maamuzi ya Raisi kichaa aliyepewa madaraka makubwa na katiba iliyopo. Katiba ya sasa iliyompa nguvu ya kuamua anavyotaka yeye na hakuna wa kumfanya lolote Kwa sababu tayari anakua ana nguvu kuliko sheria au kuliko mfumo mzima uliomuwrka kwenye madaraka hayo

Nyumba zilivunjwa licha ya kesi kuwa ipo mahakamani kwenye zuio. Nilikua na biashara ya maduka katika Nyumba zote hizo iliyoniingizia kipato cha kuendesha maisha yangu na familia yangu kwa ustawi na muelekeo wa maendeleo kieleimu, kiuchumi na kijamii katika ngazi ya familia ambayo ilisimama katika misingi ya malezi bora na muelekeo chanya

Lakini bahati mbaya kutokana na katiba mbovu iliyo toa nafasi ya kuvunja haki ya utu wa mtu Kwa sababu ya ukubwa wa maamuzi ya kimadaraka aliyopewa Raisi. Baada ya kuvunjiwa nyumba Familia yangu yote ilisambaratika binti yangu kwa sasa anaishi kwa bwana na tayari ana watoto wawili akiwa na umri wa miaka 17 tu. Kijana wangu wa kiume sasahivi ni muokota chupa na siso huku akiwa nimtumiaji mzuri wa mihadarati

Watoto wangu wote walikatisha masomo wakiawa katika umri mdogo wa elimu ya msingi na kupoteza ndoto zote walizokuwa wakiziota kielimu, maisha yao yamepoteza dira wakiwa wanaishi kwa kubahatisha kama mimi baba yao huku nikiwa sina tena nguvu wala uwezo wa kuwasaidia Kwa sababu mimi mwenyewe sijielewi nimevurugwa kukucha nashinda hospitali kupambana na presha na sukari vilivyoanza baada ya kupoteza msingi wa maisha yangu

Haya yote ni matokeo ya kupoteza dira ya maisha baada ya kuvunjiwa Nyumba. Familia yangu ilisambaratika tukakosa sehemu ya kuishi mali zangu zote zilipotea ikiwemo vitu vya ndani watoto wangu walikwenda kuishi kwa rafiki wa Mama yao aliekuwa akiishi Tandale kwa mtogole huku Mama mtu akijaribu biashara ya Samaki feri iliyopelekea kupata bwana wa kumstiri na ndoa kuvunjika Kwa sababu mimi nilikua nimesha pagawa

Kwa kifupi ushahidi huo unakutosha kuanzia sasa jua kuwa KATIBA na MAISHA ni sawa na chumvi na mboga mpunbavu wewe
 
Nimekaa sehemu na watu makini wanabishana Katiba ilivyoathiri maisha yao na mimi nimepata cha kuuliza kwa wakuu humu...
Kama nimemwelewa vizuri Mr Tundu, Katiba yetu iliharibiwa na Nyerere (si Mwinyi wala Magufuli):mwaka1962 alipojipa madaraka ya Gavana na Mtemi kuteua IGP na Wakuu wa Wilaya. Hawa wanaleta umaskini kwa sababu hawakuchaguliwa na watu.

Of course hasemi kuwa hata Rais huchaguliwa na watu, lakini hoja yake ni tumehuru isichaguliwe na Rais wala wateule wa Rais wala Bunge la CCM. Kwa kifupi, mtu pekee anayeona anafaa ni Ndug Fatuma Karume awe Mwenyekiti na Askofu Dr Pius Bagonza kama Makamo wake kuzingatia gender na pande 2 za Muungano.

Tukiweza iwe hivyo basi CHADEMA 2025 watashiriki kura, la sivyo hawatoshiriki na watafanya fujo kuhakikisha uchaguzi mzima usiwepo hata kwa wanaokubali kushiriki. Hiyo ni njia pekee itakayotupaisha maendeleo kuzidi Singapore ya Mhe. Heche.
 
Ngoja kidogo nijaribu kufafanua kwa kadri ya mtazamo wangu.....

Katiba ni sheria mama katika kuongoza na kuendesha nchi...
Excellent.

Nimependa ulivyoelezea hasa hapo kwenye uwajibikaji, kutowajibika lwa kulea uzembe unaoleta maumivu kwa wale anaowaongoza, hata kama ni kwa Katiba mbovu tuliyonayo, lazjma awe tayari kulaumiwa..
 
Nimekaa sehemu na watu makini wanabishana Katiba ilivyoathiri maisha yao na mimi nimepata cha kuuliza kwa wakuu humu.

Binafsi nikijipima sioni jinsi ilivyoathili maisha yangu. Ninawajibika kwa hivi nilivyo. Nikiwa nabidii nafanikiwa tu bila hata kujua habari za saa mbili au hotuba ya Rais imesemaje au Bunge limeamua nini.

Nikiwa mvivu, mpuuziaji, huwa nafulia tu. Huenda upeo wangu umeanza kufubaa.

Unaweza kueleza kwa lugha rahisi tu jinsi Katiba hii imekuletea umasikini au utajiri au kama haijakuathili chochote.
Hii katiba iliyopo ilitengenezwa kwa ajili ya chama kimoja kilichokuwepo wakati huo na pia kwa ajili ya watu milioni tisa waliokuwepo Nchi nzima mwaka 1962 ! Leo Nchi ina vyama vingi vya siasa na Nchi ina watu zaidi ya milioni 61 ! Mapungufu ni mengi sana na imeshapitwa na wakati !! Chombo kilichotengenezwa kwa ajili ya kubeba abiria 9 hakiwezi kikabeba abiria 61 !
 
Mayo tena wajina wa babu yangu unaniangusha sana kusema JPM hakufanikiwa kwenye madini. Hivi kodi alikuwa anakusanya kwenye madini ambazo ndizo zilizofanya maendeleo mbalimbali huku akiacha kuwasumbua wananchi na vikodi vidogo vidogo leo hii umesahau?
Una uhakika ,vipi alikula uoe mfupa wa mikataba au ilkuwa propaganda tu..Unajua mziki wa Accasia na Makinikia😁😁 tatizo ..Le jamaa alelyongo sana!?
 
Katiba mpya ikileta tume huru ya uchaguzi tutapata viongozi Bora na tutaweza kuwaondoa madarakani wakipotoka.

Katiba mpya itaondoa viongozi wa kuteuliwa Bali watu washindane kwa vyeti.

Katiba mpya itaondoa mtu mmoja kuwa na kazi mbili na kuleta unemployment mfano mbunge asiwe waziri maana hapo kachukua ajira ya mtu mwingine.

Katiba mpya itaondoa wabunge vilaza bungeni maana tutasema mbunge lazima awe graduate Ili awe na uelewa wa mambo na kutoruhusu sheria mbovu na kandamizi kupita na pia mbunge aweze kusimamia matumizi ya rasilimali zetu na kupinga bajeti mbovu.

Katiba mpya itaondoa wabunge wa kuteuliwa ambao hawawakilishi Mwananchi yoyote Bali ni upigaji tu na matumizi mabaya ya Tozo!

Katiba mpya itawapa wananchi nguvu ya kuhoji matumizi mabaya ya tozo mfano ununuzi wa mashangingi ndege nk versus BarAbara mpya, zahanati na mashule.

Katiba mpya itawapa wananchi haki ya kuandamana Barabarani bila woga wa kumwagiwa maji ya tindikali ya washawasha wanapokuwa hawaelewi mambo ya kibabe Kama umeme kukatwa ovyo na maji kukosekana au kusua sua kwa miradi ya kimkakati kama SGR na Nyerere Dam.

Katiba mpya itaondoa kifungu Cha makamu wa Rais kuwa Rais directly pale Rais aliechaguliwa kwa sanduku la kura akifa akiwa madarakani. Uchaguzi ufanyike haraka.

Katiba mpya itaondoa vyeo ambavyo havieleweki kama Mkuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya vyeo ambavyo watu hupewa kwa sifa kama jinsia yake , uchawa wake, ukada wake, dini yake nk.

Pia wananchi tutakuwa na nafasi ya kuamua mambo mengi kwa kupiga kura ya maoni kukataa maamuzi yanayotudidimiza Katika Umaskini kama vile elimu ya Sasa haifai inatumia sera ujamaa ambao umefeli maana nchi haizalishi wawekezaji wengi. Nchi hii inapaswa kuanza kutumia sera za kibepari Ili watu wawe industrious wazalishe na kuilipa kodi serikali.

ila pia kwa nguvu ya katiba mpya wananchi tutasema hatutaki kiswahili kitumike Kufundisha mashuleni tunataka English tu Ili tuweze kuondoka kwenda nje kusaka ajira na tupate wawekezaji Toka nje waje.

Katiba mpya itaondoa ukiritimba wa watu flani kujimilikisha nchi na kufuja Mali za umma maana kwasasa hawagusiki mfano mifugo ya wakubwa ilioko hifadhini!

Katiba mpya itarekebisha sheria za kumiliki ardhi na wale wenye ardhi kubwa wasizoziendeleza wanyang'anywe!

Katiba mpya haitaleta chakula Mezani ila itafumua mifumo mibovu inayokuza ufisadi na majizi yote kuwajibishwa na hapo pesa ya Tozo itatumika vizuri na nchi kuendelea!

Mimi ni kijani ila Tunda Liso ni muhimu sana kusaidia kupaza sauti ya ukombozi wa hii nchi maana kelele zake zinakera sana watu!
 
Kenya walipata katiba mpya miaka kadhaa iliyopta, je katiba hiyo imemaliza njaa na umasikini kwenye taifa lao? Je gap kati ya matajiri na masikini limeisha? Je ajira zimeongezeka?

Mimi ninachoona Taifa ili lisonge mbele pamoja na ustawi wa maisha ya watu tunahitaji viongozi bora wenye kuumizwa na shida za wananchi. Leo hii hata tukipata katiba mpya sidhani kama itabadilisha maisha ya raia kama viongozi watakuwa sio wazalendo.

Kwa sasa naona katiba inadaiwa na wanasia sana kuliko raia wa kawaida tafsiri yake ni kwamba raia wanatambua kuwa shida haipo kwenye katiba.

Ni hatari sana kuwa na katiba ambayo wanasiasa na vyama vyao wanataka kuingiza maslahi yao. Katiba tuliyonayo ni bora sana kama vyama vitatuletea wagombea bora, na katiba bora zaidi itapatikana ikiwa itaundwa na wananchi wenyewe na sio kwa msukumo wa wanasiasa na vyama vyao.
Kama kitu hufahamu Bora ukae kimya, gap la tajiri na maskini Kenya limepungua sana sababu County government zinasimamia miradi ya ndani na rasilimali za pale zinanufaisha county Ile. Mfano kabla ya county Ina maana Odinga alifeli uchaguzi basi western yote haipati miradi ila Kwa kuwa Kodi inayokusanywa Western na Nyanza kiasi kikubwa kinabakia huko basi obvious gap la umaskini kati ya kaunti umepungua.

2. Unasema tupate viongozi Bora utawapataje kama hakuna tume huru?? Mbunge wa CCM mfano wa Tabora mjini hakuna alichofanya miaka yote ila Kila uchaguzi anajua atashinda hata wakimkataa. Kwa Kenya 80%ya wabunge wa 2017 hawakushinda 2022!! Je Tanzania unadhani Kuna siku litatokea Hilo?

3. Haya mfano wabunge hawataki tozo kwenye bajeti, katiba inasema ukipinga bajeti Rais ana mamlaka kuvunja bunge!! Sasa Kuna faida Gani ya kuwa na wabunge wazalendo kama katiba haiwaruhusu kupinga bajeti.

Let's be serious
 
IMG_0215.jpg
 
Kenya walipata katiba mpya miaka kadhaa iliyopta, je katiba hiyo imemaliza njaa na umasikini kwenye taifa lao? Je gap kati ya matajiri na masikini limeisha? Je ajira zimeongezeka?

Mimi ninachoona Taifa ili lisonge mbele pamoja na ustawi wa maisha ya watu tunahitaji viongozi bora wenye kuumizwa na shida za wananchi. Leo hii hata tukipata katiba mpya sidhani kama itabadilisha maisha ya raia kama viongozi watakuwa sio wazalendo.

Kwa sasa naona katiba inadaiwa na wanasia sana kuliko raia wa kawaida tafsiri yake ni kwamba raia wanatambua kuwa shida haipo kwenye katiba.

Ni hatari sana kuwa na katiba ambayo wanasiasa na vyama vyao wanataka kuingiza maslahi yao. Katiba tuliyonayo ni bora sana kama vyama vitatuletea wagombea bora, na katiba bora zaidi itapatikana ikiwa itaundwa na wananchi wenyewe na sio kwa msukumo wa wanasiasa na vyama vyao.
Ficha ujinga wako,hao wananchi ndo wanaopewa kanga na pombe kipindi Cha uchafuzi.ndo waijue katiba???
 
Mim ninaiman kuwa tuliomo humu ni wasomi kumbe kunawengine hata shule hawana , unasema kuwa katiba haileti ugali mawazo mfu kabisa
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Sasa watu wachache kupiga pesa ndio Katiba.

Mbona Yuda alipiga pesa na hawakuwa hata na katiba. Upigaji ni Moja ya dhambi kongwe.

Sijaona katiba inapoingia hapo. Dadavua Kwa kina kidogo Bro
Sasa hapa naona unajaribu kuchangaya au kukimbia ulichouliza, umezungumzia katika na umetoa mfano wa yuda, sasa kwanin usingetoa mfano uhusuyo katiba bila kuchangani mambo ya imani za watu n katiba
 
Katiba ni utajiri katiba ni umaskini kwa taifa... Chukulia mfano mgao wa umeme na maji bila ya kuwa na sababu zinazoeleweka zihusuyo mgao huo, huku ukijua wazi wahusika wanaliona na hawafanyi lolote, na hapo hapo wewe ni mzalishaji wa kuku wakisasa au ni mmiliki wa kampuni yakutotolesha vifaranga...

Je kupitia mfano huu wa kuku unadhani wewe kwa kila sekunde unapoteza sh ngapi, na hapo hapo kunawafanyakazi waotegemea umeme huo kulisha familia zao kupitia ajira yako ya kuku
 
Mim ninaiman kuwa tuliomo humu ni wasomi kumbe kunawengine hata shule hawana , unasema kuwa katiba haileti ugali mawazo mfu kabisa

..wengine wametumwa kupotosha na kuharibu mjadala wa katiba.
 
Katiba mpya maana yake wanasiasa wanataka kugawana vyeo, unasikia Chadema wanataka serikali za majimbo, huko wanatengeneza vyeo vipya.

Mbona watu ni matajiri na tunawaona na kwa katiba hii hii, mfano Mbowe na baba yake, tangu katiba ya mkoloni Wana pesa.
SPOT ON
 
Mimi hapa nimekuwa masikini wa kutupa kutoka katika maisha ya kawaida Kwa sababu ya katiba mbovu. Nilikua na Nyumba zangu mbili kimara zikavunjwa na sasa naishi uchochoroni Tandale uzuri, nimepanga chumba kimoja tu nalala chini sina chochote mali zangu zoote zilipotea hapa nilipo nimechoka na kupauka kama kipande cha muhogo mkavu

Nyumba zangu zilivunjwa kutokana na maamuzi ya Raisi kichaa aliyepewa madaraka makubwa na katiba iliyopo. Katiba ya sasa iliyompa nguvu ya kuamua anavyotaka yeye na hakuna wa kumfanya lolote Kwa sababu tayari anakua ana nguvu kuliko sheria au kuliko mfumo mzima uliomuwrka kwenye madaraka hayo

Nyumba zilivunjwa licha ya kesi kuwa ipo mahakamani kwenye zuio. Nilikua na biashara ya maduka katika Nyumba zote hizo iliyoniingizia kipato cha kuendesha maisha yangu na familia yangu kwa ustawi na muelekeo wa maendeleo kieleimu, kiuchumi na kijamii katika ngazi ya familia ambayo ilisimama katika misingi ya malezi bora na muelekeo chanya

Lakini bahati mbaya kutokana na katiba mbovu iliyo toa nafasi ya kuvunja haki ya utu wa mtu Kwa sababu ya ukubwa wa maamuzi ya kimadaraka aliyopewa Raisi. Baada ya kuvunjiwa nyumba Familia yangu yote ilisambaratika binti yangu kwa sasa anaishi kwa bwana na tayari ana watoto wawili akiwa na umri wa miaka 17 tu. Kijana wangu wa kiume sasahivi ni muokota chupa na siso huku akiwa nimtumiaji mzuri wa mihadarati

Watoto wangu wote walikatisha masomo wakiawa katika umri mdogo wa elimu ya msingi na kupoteza ndoto zote walizokuwa wakiziota kielimu, maisha yao yamepoteza dira wakiwa wanaishi kwa kubahatisha kama mimi baba yao huku nikiwa sina tena nguvu wala uwezo wa kuwasaidia Kwa sababu mimi mwenyewe sijielewi nimevurugwa kukucha nashinda hospitali kupambana na presha na sukari vilivyoanza baada ya kupoteza msingi wa maisha yangu

Haya yote ni matokeo ya kupoteza dira ya maisha baada ya kuvunjiwa Nyumba. Familia yangu ilisambaratika tukakosa sehemu ya kuishi mali zangu zote zilipotea ikiwemo vitu vya ndani watoto wangu walikwenda kuishi kwa rafiki wa Mama yao aliekuwa akiishi Tandale kwa mtogole huku Mama mtu akijaribu biashara ya Samaki feri iliyopelekea kupata bwana wa kumstiri na ndoa kuvunjika Kwa sababu mimi nilikua nimesha pagawa

Kwa kifupi ushahidi huo unakutosha kuanzia sasa jua kuwa KATIBA na MAISHA ni sawa na chumvi na mboga mpunbavu wewe
Unaweza kutusaidia uliacha lini kuwa kichaa? kwani ni ukichaa tu utakuwa ulikupeleka kujenga sehemu ambako kichaa anaweza kukutoa
 
Back
Top Bottom