KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Ngoja kidogo nijaribu kufafanua kwa kadri ya mtazamo wangu.....
Katiba ni sheria mama katika kuongoza na kuendesha nchi.
Katiba nzuri huzalisha utawala bora unaozingatia haki na usawa kwa wananchi wake pasi na kuangalia hadhi na nafasi ya mtu.
Katiba bora inayozingatia haki na usawa huleta uwajibikaji na uwajibishwaji kwa wote na wale wanaokiuka.........
Katiba bora ambayo huzaa utawala bora na uwajibikaji huzalisha sera nzuri na mipango ya kimaendeleo kwenye jamii husika....sera hizo na mipango mizuri ikiingia katika uwajibikaji humgusa mwananchi moja kwa moja.
Kwa mfano katiba inasema kila mtu ana haki ya kuishi kwa amani na usalama.....jeshi la polisi kupitia wizara ya mambo ya ndani au jeshi la ulinzi kupitia wizara ya ulinzi vitalazimika kutunga sera na mipango ya kumhakikishia huyu mtu usalama na amani itakayomfanya kuweza kufanya shughuli zake za kujiletea maendeleo pasi na hofu yoyote.
Mfano katiba inasema kuwa kila mtu ana haki ya kuishi....serikali kupitia wizara ya afya watatunga sera na mipango ya kuboresha huduma za afya ili watu waishi maisha mazuri yenye siha njema......na sheria kali na adhabu vitatungwa kwa yoyote atakayejaribu kudhurumu haki hiyo.
Hiyo ni mifano ya mambo machache yanayoonyesha namna ambavyo katiba inakugusa moja kwa moja au sio moja kwa moja kupitia sera na mipango katika utekelezaji wa matakwa ya kikatiba.
NB;
Huo ni mtazamo wangu tu kwa jinsi nilivyoona.....