Mwenye ushahidi au maelezo toshelezi jinsi Katiba ilivyomletea umasikini/utajiri

Sidhani kama vichwapanzi wanaweza kukuelewa
 
Mikopo tunayokopa Tanzania bara kwa maendeleo na wa zanzibar walikua wana 3% yao inapelekwa huko, na mlipaji wa mkopo ni Tanzania bara hiyo ni shida inayoletwa na katiba tena nasikia sahivi wanachukua 7% sio 3% tena
 
Sasa watu wachache kupiga pesa ndio Katiba.

Mbona Yuda alipiga pesa na hawakuwa hata na katiba. Upigaji ni Moja ya dhambi kongwe.


Sijaona katiba inapoingia hapo. Dadavua Kwa kina kidogo Bro
Ondoa upofu wa fikra
 
Mikopo tunayokopa Tanzania bara kwa maendeleo na wa zanzibar walikua wana 3% yao inapelekwa huko, na mlipaji wa mkopo ni Tanzania bara hiyo ni shida inayoletwa na katiba tena nasikia sahivi wanachukua 7% sio 3% tena
 
Wakati wa uanaharakati mazingira wa Pro. Wangari Maathai Kenya, kuna kiongozi mkubwa wa nchi alikuwa anshangaa mwanamama anayesema mvua inatokana na miti wakati inatoka mawinguni😂😂😂😂😂
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wakati wa uanaharakati mazingira wa Pro. Wangari Maathai Kenya, kuna kiongozi mkubwa wa nchi alikuwa anshangaa mwanamama anayesema mvua inatokana na miti wakati inatoka mawinguni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
 
Braza taratibu basi tukuelewe wote kwa faida ya wengi. Kama unapanic sana!!
 
Mtoa mada ni mtoto. Maendeleo ya nchi 80% huletwa na serikali ambao ni wanasiasa. Na nchi ili iendelee Inahitaji uongozi Bora ambao hutokana na katiba Bora. Huwezi kua na viongozi Bora wanaotokana na katiba mbovu never ever.

Leo hii Kodi zetu ziko juu sana kutokana na maamuzi ya viongozi wanaotokana na katiba. Mbovu tuliyonayo. Viongozi hawawajibiki. Nape anakujubu anavyotaka. Makamba anhujumu tanesco kutokana na katiba mbovu.

Mwigulu anaweka na kuongeza Kodi kila sehemu bila kuulizwa. Hii inapelekea Biashara kufa na kuongeza umaskn.

Bashe naye Hana msaada kwa wakulima. Wakulima wamebaki huko wanatapatapa kama watoto yatima. Serikali hii inayotokana na katiba mbovu ndo inaongeza umaskn kila siku kwa watu
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba ili nchi ipate maendeleo inahitaji Mambo manne.
Nayo ni (1) Watu (1) Ardhi (3) Uongozi (4) Siasa safi ambayo itatokana na katiba bora.
 
Hao viongozi waziri unaowasema watapatikanaje Sasa bila katiba Bora yenye kuweka Msingi wa kwenda mahakamani kura zikiibiwa. Katiba ikiwa mbovu kama hii tuliyonayo rais akiamka anaweza kusema chochote na kikawa Sheria na wewe kikakuathiri moja kwa moja na huna pa kwenda mana mahakama zote zinapewa marlekezo kwamba funga nani acha nani. Mfano mzuri ni dictator jpm
 
Mm nilivyoanza kuskia mambo ya katiba mpya nikajua italeta chakula mezani, kumbe bado unatakiwa kupambana vile vile ili upate chakula hata kama katiba imechakaa

Kwani hii katiba iliyopo sasa ilileta chakula mezani ndio ikawekwa? Kwanini tusiondoe kabisa hata katiba hii iliyopo ili chakula kiwe kingi mezani?
 
Kama katiba mpya ndiyo muarobaini wa umasikini wa mtu mmoja mmoja,

Je matajiri wa sasa wao wanatumia katiba ipi?

NB:Kuna watu wamefanikiwa kimaisha bila hata kufungamana na CCM.
Hata gerezani kuna wenye afya njema lkn wote wanakula chakula cha aina moja na huu ni mwaka 10 wako wote, ila una mawazo ya kitoto sana.
 
Bila Katiba mpya, hatutaweza kutoboa kamwe. Yaani zaidi ya asilimia 90 MATUMIZI BINASI, zinazobaki ndio zitaleta maendeleo kweli? MAISHA MAGUMU = KATIBA MBOVU

 
Kwani hii katiba iliyopo sasa ilileta chakula mezani ndio ikawekwa? Kwanini tusiondoe kabisa hata katiba hii iliyopo ili chakula kiwe kingi mezani?
Wap nimeandika katiba inaleta chakula.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…