Mwenye ushahidi au maelezo toshelezi jinsi Katiba ilivyomletea umasikini/utajiri

Katiba haiwezi kuzuia kiongozi kuwa mwizi ni malezi pekee aliyopata huyo kiongozi ndio yatamfanya awe mwizi au aeshimu mali ya uma. Mfano mzuri ni humu jukwaani ukisoma thread za watu vizuri utagundua yupi kalelewa na bibi na yupi kalelewa na wazazi wake.

Kwamba katiba itamtisha mtu aisiibe? Wala sidhani au utadai kwamba akiiba atawajibishwa? Ni wangapi wameliibia hili taifa na walipoanza kuwajibishwa na JPM mkamwita dictator? Ni wazembe wangapi walitumbuliwa mkawatetea kwa katiba hii yaani ni kama mnataka kuwaona watu wajinga.

Mimi sipingi ujio wa katiba mpya ila napingana na vijisababu mnavyovitoa wakati sababu kubwa ya wanasiasa kudai katibu mpya ni kwa ajili ya kutafuta vyeo na madaraka wala sio kwa ajili ya wananchi. Unataka kuniambia wanasisa hasa upinzani ndio wana uchungu na maisha ya mtanzania kuliko mtanzania mwenyewe.
 
Labda kupitia katika mpya tungepata viongozi competent, labda tungekuwa na dira ya taifa inayoeleweka, labda tungekuwa hakuna ukilitimba kwenye ofsi za umma, labda kungekuwa na kiwango kidogo cha rushwa, labda tungepata wataalam wanaojielewa, labda tusingekuwa na machawa, labda kila mtu angekuwa kwenye mazingira sawa ya kufanikiwa kati ya watoto wa viongozi, labda kungekuwa na uchaguzi huru, labda viongozi wangejituma ili wachaguliwe tens, watoto wa matajiri na watoto wa masikini.
Labda!!!!!
 
Hii nchi ina raia wajinga na wa hovyo sana
Kwani hii katiba iliyopo sasa ilileta chakula mezani ndio ikawekwa? Kwanini tusiondoe kabisa hata katiba hii iliyopo ili chakula kiwe kingi mezani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…