Mwenye ushahidi Mbowe kula ruzuku ama kupewa rushwa auweke hapa!

Unaona wanaCHADEMA wananung'unika jinsi Uongozi wa CDM ulivyokosa prorities.



wakipewa Nchi itakuwaje?

Mwishowe hata gari la Raisi liishiwe mafuta baraharani kama Helikopta.
 
Umelisoma bandiko langu wa muimo tofauti sana.

CCM wanaposema mwenye ushahidi aje hujua watu wataogopa dola na hawatajitokeza, lakini kwa Mbowe kama ushahidi upo CCM au wabaya wake wangeshautumia kwa kuwa yeye hana dola.

suala la Lowassa linaeleweke wengine wasioelewa ni wale walioshibishwa Propaganda za CCM. Mpaka leo CHADEMA wanataka Lowassa afikishwe mahakamani na wao walisema ni kwa nini afikishwi mahakamani kama anatuhumiwa kwa ufisadi,

Hivi ufisadi wa Lowassa unahusiana na nini hasa!!??
 
Umeishajiuliza kwa nini uwa anaenda Ikulu peke yake hataki kuongozana nq mtu?
 
Angejenga jengo moja kubwa tu kuliko kununua magari mengi ya M4C au kukodi chopa.

Uko sahihi sana, kulikuwa na uwezo mkubwa ww kujenga ofisi ya 500m-1b, lakini wakaingia kwenye mambo mengine kabisa. Na uwezakano wa Kila wilaya na Mkoa kuwa na ofisi ya 30-50m ulikuwa mkubwa mno.
 
Mpaka leo wanataka afikishwe mahakamani wakati walimpa nafasi ya kugombea uraisi kupitia chama chao? Yani mtu unayetaka afikishwe mahakamani kwa ufisadi unampa nafasi ya kugombea urais. Hakuna propaganda, bali ni CHADEMA waliozunguka nchi nzima waksiema ni fisadi.
Sasa kwanini wahangaike naye kama wanaona hana meno ya kuwasumbua sasa katulia tuli. Sijasema kuwa ni kweli ila kama ni kweli hawana muda naye. CCM wakishakuweka chobingo wakajua huna hatari basi hata hawasumbuki na wewe. Si unaona COVID-19, siku hizi hata hawawasumbui kama zamani enzi zile mara Halima awekwe ndani, mara sijui aitwe polisi.
 
Usinisemee jibu swali kwa nini safari za Ikulu anaenda peke yake hataki kuongozana na mtu?
Mjadala ni Mbowe kuhongwa... Wewe unaleta mambo ya yeye kwenda Ikulu peke yake. Ni kama unaashiria kwamba huwa akienda Ikulu ndiyo anakwenda kuhongwa.

Sasa nakuuliza kuwa unataka kusema Rais ndiye huwa anamhonga Mbowe!!??
 
Kwa hali yoyote CHADEMA hawakushindwa kujenga ofisi kubwa za chama chao za ghorofa hata 3 kama wangetaka, ila itakuwa tu hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo jambo ambalo likikuwa kosa kubwa la kisiasa.

Ni kweli hakuna umuhimu kabisa wa vyama kumiliki majengo au kufanya biashara, kwa sababu havina tija yoyote katika kuongeza demokrasia ya nchi, utawala bora au maendeleo, zaidi sana vinaharibu demokrasia ndani ya vyama kwa kuzigeuza siasa kuwa ujasiriamili na kuzalisha career politicians wasioweza kufanya jambo lolote nje ya siasa.
Ila raia wengi hawana ufahamu huu, ilibidi tu CHADEMA wamiliki majengo mawili matatu kufuta hizi kelele za kijuha.
 
Mpaka leo wanataka afikishwe mahakamani wakati walimpa nafasi ya kugombea uraisi kupitia chama chao?
Kumpa nafasi ya kugombea ilikuwa ni kosa la kiufundi lakini siyo jinai. Lakini kama mpaka leo kama inaaminika kwamba ni fisadi si wamfikishe mahakamani??

Kuna bandiko humu nikishadadia Lowassa afikishwe mahakamani.
Yani mtu unayetaka afikishwe mahakamani kwa ufisadi unampa nafasi ya kugombea urais. Hakuna propaganda, bali ni CHADEMA waliozunguka nchi nzima waksiema ni fisadi.
kwani ufisadi wa Lowassa uliokuwa unasemwa na CHADEMA ulihusu nini hasa!!??
 
Nakuja baadaye ngoja nitoke shambani.lakini nikakutage mmeniandalia majibu ya fedha za join the chain zilipatikani shilling ngapi na zipo wapi? Nikute pia majibu ya zilipo pelekwa million mia moja alizotoa mzee sabodo. Nikute pia majibu ya wapi michango ya wabunge kwa miaka yote waliyokuwa wanakatwa kila mwezi pamoja na mamilioni ya Ruzuku zilikwenda wapi ikiwa chama kilikuwa kinakaa kwenye pagala la kupanga ambalo lilikuwa halipakwi hata rangi? Nikute pia majibu kuwa katika ile michango ya Hanang ambayo mbowe aliweka picha yake na namba ya simu ili achangiwe alipata shilingi ngapi na pesa zimekwenda wapi wakati chama hakijapeleka cha kueleweka kwa waathirika wa Hanang?

Hayo ni maswali baadhi tu kati ya mengi nitakayokuja nayo nikipumzika mwili baada ya kutoka shambani
 
Hapa umesalimia tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Unataka ushahidi upi? Anatakiwa atoe matumizi ya ruzuku aweke mchanganua wa hesabu tuone kutuambia tulete ushahidi wakati akaunti ya ruzuku yeye ndiyo anatoa pesa unataka twenda benki kuomba statement ?
Hela walipwe CHADEMA mchanganuo atoe Mbowe... unawaza sawasawa wewe!!

Yaani unataka kusema Serikali inayoongozwa na CCM badala ya kuweka hela kwenye Akaunti ya CHADEMA yenyewe inaweka hela kwenye Akaunti ya Mbowe?? Si Ujuha huo!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…