Mwenye ushahidi Mbowe kula ruzuku ama kupewa rushwa auweke hapa!

Mwenye ushahidi Mbowe kula ruzuku ama kupewa rushwa auweke hapa!

Chama kikuu cha upinzani kimeazishwa mwaka 1992 kweli tuna ofisi ya kupanga ya room 3.

Ruzuku ya chama inafanya kazi gani?
 
Attachments

  • IMG_8767.jpeg
    IMG_8767.jpeg
    47.3 KB · Views: 2
Hela walipwe CHADEMA mchanganuo atoe Mbowe... unawaza sawasawa wewe!!

Yaani unataka kusema Serikali inayoongozwa na CCM badala ya kuweka hela kwenye Akaunti ya CHADEMA yenyewe inaweka hela kwenye Akaunti ya Mbowe?? Si Ujuha huo!!??
Unaona sasa akili yako ruzuku ni kodi zetu tuna haki ya kuhoji.
 
Nadhani ukitaka kumpima Mbowe tumia vigezo vyote vinavyohitajika na vinavyopaswa kulinganishwa na wengine. Idadi na ubora wa wabunge,majimbo waliyoweza kushika na changamoto zake,maana majimbo ya mjini si mchezo,uwezo wake wa ku-train viongozi mpaka ngazi za chini,ushawishi wa chama chake na kufahamika mpaka ngazi za chini na mengine. Hakuna binadamu asiyeweza kuhongwa ila matokeo ya kuhongwa huwa hayajifichi. Kwa mazingira ya katiba na kanuni na tabia zetu watanzania wenyewe kutegemea angeweza kufanya miujiza zaidi ni kumuonea. Shida ya Mbowe na pengine ndio uzuri wake ni kwamba kwa kiasi fulani amestaarabika na haamini sanaa kwenye violence na kelele. Anajua ana nguvu ila anajua pia kuwa na kiasi cha namna anavyotumia sauti yake na ndio maana ni rahisi kuona amehongeka. Emotional intelligence ya Mbowe ni kubwa sana nikitakaga kumhukumu narudigi kwenye hotuba yake baada ya Mzee Magufuli kupumzika. Pamoja na yote aliyopitia,that speech was balanced. Kwenye ishu ya Kanisa na fedha,mimi nitamtetea Mbowe...ukiacha kuwa Mbowe ni Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani,Mbowe huko kwao ni Mzee wa heshima,ni kiongozi asiye na title kwa sasa kwenye jamii,alikuwa Mbunge zaidi ya miaka 15. Ukitegemea atategemewa kusaidia kanisa analosali na pengine atakaloagwa akimaliza mwendo na asifanye hivyo ni sawa na kutegemea asijenge kwake. He had to,whatever it takes.Aliweka mbele mategemeo ya wanaomtegemea na sio hisia zake kuhusu mtu fulani au huyo fulani ni nani. Ibada zitafanyika pale kwa wenye vyama,wasio navyo na hata wasioelewa bado vyama ni nini (watoto). Mwisho wa siku he is human,ana mapungufu na ukamilifu hautawahi kuwa wake.
 
Hili swali ni lile lile swali ambalo watetezi wa mafisadi ya ccm huwa wanauliza kuwa mwenye ushahidi auweke wazi. Ni swali lile lile ambalo CHADEMA waliuliza kuwa mwenye ushahidi wa ufisadi wa lowasa aupeleke mahakamani wakati ni wao wenyewe waliozunguka Tanzania kwa miaka 8 mfululizo waksiema ni fisadi, anafaa kupigwa mawe.
Kwa nchi hii ilivyo, ukitaka ushahidi, kila kigogo ni msafi maana hutoupata.
Mind you, mimi si kati ya wanaosema Mbowe anakula ruzuku ila tu ninalinganisha swali lako na swali lililozoeleka
Kwenye siasa za kugombea madaraka huwa kunakuwa na fitina, uongo, sarakasi na propoganda nyingi sana ndani ya vyama na kati ya vyama, mfano ni huu ambao Kinana alienda mbali zaidi hadi akamuhusisha Lowassa na magaidi au watu wenye misimamo mikali!
 
Chama kikuu cha upinzani kimeazishwa mwaka 1992 kweli tuna ofisi ya kupanga ya room 3.

Ruzuku ya chama inafanya kazi gani?
Na ile ya Mikocheni??

Bado nasubiri jibu kujua kama Rais ndiye anayemhonga Mbowe!!
 
Kama wewe una ushahidi kwamba Freeman Mbowe anakula Ruzuku za CHADEMA ama yeye binafsi au uongozi mzima wa CHADEMA yeye akiwa mwenyekiti wake, walipewa rushwa na CCM ili waache harakati za kuipigania Tanganyika na Zanzibar, uuweke hapa ili watanzania wote wauone.

Sema kweli ama kaa Kimya!!
"MTI WENYE MATUNDA NDIO HUPIGWA MAWE" NI WAJINGA NA WAPUMBAVU WALIOKOSA HOJA WANAMZULIA JABALI LA SIASA ZA UPINZANI Kamanda MBOWE

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Unaona sasa akili yako ruzuku ni kodi zetu tuna haki ya kuhoji.
Kuna mahali nimesema isihojiwe... ila hujui jinsi ya kuhoji.

Bado nataka useme Rais ndiye anayemhonga Mbowe!!??
 
Kwenye siasa za kugombea madaraka huwa kunakuwa na fitina, uongo, sarakasi na propoganda nyingi sana ndani ya vyama na kati ya vyama, mfano ni huu ambao Kinana alienda mbali zaidi hadi akamuhusisha Lowassa na magaidi au watu wenye misimamo mikali!
CHADEMA tulitegemea iwe tofauti. Sasa kama ilizunguka miaka 8 ikisema lowassa ni fisadi halafu baadaye ikasema si fisadi sasa ni vigumu kuamini kingine watakachosema maana ni vigumu kutofautisha ni wapi wanasema ukweli na wapi wanasema uongo.
 
Haya mambo kwa watu walio ndani wanajua. Ni kama kujiuliza kilianza nini kati ya Yai na kuku.

Nani huwa anachangia operesheni mbali mbali za CHADEMA na gharama zake huwa ni kiasi gani. Operesheni nyingi zinaendeshwa kwa mtindo wa kujenga chama hivyo kunakuwa na kundi kubwa sana la watu toka Makao Makuu.

Jee kwa siku moja zinatumika shilingi ngapi. Mtazamo wa chama ilikuwa kujenga watu ambao mwisho wa siku waje wajenge ofisi za chama nchi nzima. Kuna baadhi ya maeneo hili limefanikiwa sana.
Ahaaa ahaa, imebidi nicheke sana, kwamba uwe na wanafunzi wengi, kisha hao wanafunzi ndio waje wajenge madarasa! Haya tuseme hao watu wameshakuwa wengi, je ofisi ziko wapi?
 
ficha wewe.
Hoja hiyo imepitwa na wakati...

Mbona CCM ina ofisi kila kona na bado umaskini wa watanzania unazidi kutamalaki.

Hivi watanzania wakawaida wasio wanachama wa chama cha siasa ofisi za chama hicho zinawahusu nini??
 
Na ile ya Mikocheni??

Bado nasubiri jibu kujua kama Rais ndiye anayemhonga Mbowe!!
Chadema wana ofisi Mikocheni? Kwa faida ya JF naomba tuwekee japo picha.

Hamna sehemu nimekuambia Rais anamuonga Mbowe nimeuliza kwa nimi IIkulu uwa anaenda peke yake? Ni jibu tu
 
Ahaaa ahaa, imebidi nicheke sana, kwamba uwe na wanafunzi wengi, kisha hao wanafunzi ndio waje wajenge madarasa! Haya tuseme hao watu wameshakuwa wengi, je ofisi ziko wapi?
Tindo Ofisi za CHADEMA zilizojengwa kwa nguvu za wanachama ziko nyingi za kutosha tu. fanya utafiti.

Lakini kimantiki Ofisi za CHADEMA zimepunguza kiasi gani ufanisi wa CHADEMA kujipambanua kwa wananchi??
 
Kama wewe una ushahidi kwamba Freeman Mbowe anakula Ruzuku za CHADEMA ama yeye binafsi au uongozi mzima wa CHADEMA yeye akiwa mwenyekiti wake, walipewa rushwa na CCM ili waache harakati za kuipigania Tanganyika na Zanzibar, uuweke hapa ili watanzania wote wauone.

Sema kweli ama kaa Kimya!!

Ushahidi ni ofisi ya chadema kuwa chafu kwa miaka 30
 
Hamna sehemu nimekuambia Rais anamuonga Mbowe nimeuliza kwa nimi IIkulu uwa anaenda peke yake? Ni jibu tu
Hoja ya Mbowe kwenda Ikulu peke yake uliileta kuashiria kwamba huko ndiko inawezekana anakohongwa. Sasa nakuuliza jee Rais ndiye huwa anamhonga Mbowe??
 
Chama kikuu cha upinzani kimeazishwa mwaka 1992 kweli tuna ofisi ya kupanga ya room 3.

Ruzuku ya chama inafanya kazi gani?
Vyama karibia vyote vya siasa Kenya vimekuwa havimiliki ofisi zao kwa miaka mingi sana. Kwa sasa chama kikubwa chenye kumiliki ofisi ni ODM. UDA ya Ruto na Jubilee ya Uhuru Kenyatta wanakodi ofisi zao.
 
KANU ofisi yao ilikuwa kwenye Jengo la Kenyatta International Conference Center na walipoingia NARC wakawafurusha KANU kwenye Jengo lile.
 
Back
Top Bottom