Tetesi: Mwenyekiti Bawacha kubwaga manyanga kwa press wiki ijayo

Huyo mama ni dhahiri alikuwa upande wa mbowe ataondoka kufuata genge lao huko linakoelekea
 
Mbona unafuatilia na kushadadia mambo ya chadema ambayo hayakuhusu.Ungeshughulika na mambo ya kujenga na kuimarisha chama chako cha ccm kuelekea uchaguzi.
 
Ndugu yangu Zanzibar-ASP, hata santuri ikiwa nzuri kiasi gani, mbuzi watasimama pale pale na usimtegemee kumuona akitikisa hata hako kamkia kake. Waliopanga upuuzi huu tunaoushuhudia, kwa akili zao waliamini kabisa Chadema lazima isambaratike!

Kumbe! Chadema walijua kila kilichokuwa kikipangwa na walijua ni lini misafara ya wasaliti itaanza. Kwamba leo waondoke watano, kesho saba, keshokutwa kumi, mtondo kumi na wawili, mtondogoo kumi na watano...walivyo wapuuzi wakaipa jina gharika.

Eti gharika kuikumba Chadema, upuuzi mtupu. Kiongozi mkuu, Mh. Tundu Lissu, kabambikiwa kesi na kuswekwa ndani, Chadema haikutetereka. Wanachama kutekwa, kuteswa na kupotezwa, Chadema haikutetereka sasa itakuwa hawa wanaojiita G-55, thubutu!
 
Narudia Tena , aondoke haraka tumchague Rose Mayemba kama Mwenyekiti wa BAWACHA.
 
Wewe ni miongoni mwa g55 akili yako inajionesha hivi unaweza hama chama kisa aliyeshinda humpendi
Chadema siyo viongozi chadema ni wananchi ndiyo maana watahama viroboto wote lakini chadema itaendelea kudumu.
Tatizo la watu kama wewe ni kuwa mnameza kila mnachoambiwa bila kulitafakari. Sio bure mkaitwa nyumbu. Hakuna mahali G-55 wamesema kuwa wanaondoka kwa sababu Lissu kashinda. Wamesema wanaondoka kwa sababu ya vitendo vya viongozi wa sasa wa Chadema. Hawa unaowaita viroboto ndio walioofikisha CDM hapa ilipo. Wewe umechangia nini kwa Chadema?

Amandla...
 
Pole mkuu, unachokidhani sicho hicho...
 
Waliamini wao watashinda 100%, tatizo lilianzia hapo.Unahamaje kwenye chama kwa sababu ya kizembe hivi?
 
Pole mkuu, unachokidhani sicho hicho...
Huyo labda ndiye wasaliti, G-55, wamemchagua kuwa msemaji wao kwenye social media, ha ha haa. Anavyohaha humu JF unaweza hata kumhurumia.
 
Sawa. Mmeacha kwenda kuvua kwa sababu Mamlaka ya Uvuvi imewakataza? Nyinyi ndio mnasema mtapambana na CCM kuliko walivyofanya wakina Ruge, Aisha na wengine? Nyinyi ambao mlimkimbia kiongozi wenu alipobebwa mbele yenu! Nyinyi ambao mmeogopa kwenda Mahakamani kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wenu mpaka mpate kibali cha serikali!

Hamjawahi na hamtawahi kukipigania chama chenu. Na CCM wanajua hilo ndio maana wanawachezea wanavyopenda.

Amandla...
 
Ni bora kuelewa kinachovutia wengi Chadema ni Hoja ya Katiba na uchaguzi huru!

Sio Uongozi, mathalani wa Mbowe na team yake waliokaa zaidi ya 20 yrs with no substantial call for such changes!

So,kutoka kwao..ni
"KUVUJA KWA PAKACHA...
Mabadiliko haya yameanza kuzungumzwa kwanguvu na ari zaidi 2015..from there akaja JPM...akaua siasa za nchi kwa maslahi yake na chama chake,bila kujua madhara kwa chama kwa muda wa kati na mrefu..


Naona by 2030...yanaenda kutimia, its fate,lazima iwe hivyo!
 
Mbona unafuatilia na kushadadia mambo ya chadema ambayo hayakuhusu.Ungeshughulika na mambo ya kujenga na kuimarisha chama chako cha ccm kuelekea uchaguzi.
Si kila siku mnatuambia Chadema ni ya taifa zima na mnatupigania wananchi wote? Kumbe mnachotaka ni kusifiwa tu? Mnatofauti gani na CCM katika kuendekeza uchawa?

Amandla...
 
Pole mkuu, unachokidhani sicho hicho...
Hamna taabu. Mradi ni mawazo yangu na sio ya mtu mwingine. Ukweli utajulikana tu hivi karibuni. Kama nimekosea nitaomba radhi. Sidhani kama wewe unaweza kufanya hivyo.

Amandla...
 
Huyu aondoke mara Moja , kwanza hajulikan, Hana msaada wowote na Chama .

Pili hawez kufanya kazi na Uongozi mpya.

Aondoke, tuiingize MTU mpya.
uchungu na hasira za kuachwa hazijifichi kwa sura, maneno wala matendo gentleman,

na bado πŸ’
 
Habari za kuaminika ni kwamba Ma dam amesha wekwa kwenye ratiba ya kutangaza kuachana na CHADEMA wiki ijayo.

Sababu ni zilezile na atatangaza ameondoka na bawacha 500.

Kazi ipo
Safi sana, achukue hela hizo, sijui wanampa milioni ngapi!
 
Habari za kuaminika ni kwamba Ma dam amesha wekwa kwenye ratiba ya kutangaza kuachana na CHADEMA wiki ijayo.

Sababu ni zilezile na atatangaza ameondoka na bawacha 500.

Kazi ipo
ni vizur sana wananchi kutumia uhuru na haki zao za kikatiba bila wengine kuwakasirikia πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…