Tetesi: Mwenyekiti Bawacha kubwaga manyanga kwa press wiki ijayo

Tetesi: Mwenyekiti Bawacha kubwaga manyanga kwa press wiki ijayo

Mbona Heche anakomba posho kila siku kupitia tone tone?😁
Akombe posho wakati pesa za tone tone zimeenda kununulia EBOLA na Mpox. ???
Kwakuwa wewe unalipwa posho chafu kwa kuandika upuuzi hapa unafikiri kila mtu analipwa posho.
Unawaza posho tu dada?
Nimekuambia mambo ya muhimbili una makia HECHE?
 
Sio bure mkaitwa nyumbu.
Umepoteza the moral high ground.
Ulianza kama voice of reason. Sasa unaita watu nyumbu!

Hahahahaaaa...

Mtetezi wa G55, waliosema wametwezwa, wamekebehiwa, unatumiaje lugha kama hizo?

"Unathibitisha kwamba unachojua ni matusi."

G55 bado wanashindwa kusema shida ni nini, haswa kwa kutumia wasemaji kama Fundi Mchundo.
 
Umepoteza the moral high ground.
Ulianza kama voice of reason. Sasa unaita watu nyumbu!

Hahahahaaaa...

Mtetezi wa G55, waliosema wametwezwa, wamekebehiwa, unatumiaje lugha kama hizo?

"Unathibitisha kwamba unachojua ni matusi."

G55 bado wanashindwa kusema shida ni nini, haswa kwa kutumia wasemaji kama Fundi Mchundo.
Sijawahi ku claim hiyo moral high ground, wala mimi kuwa ni voice of reason. Nimewaita nyumbu wale ambao wana jaribu kuwa bully wale ambao hawakubaliani nao. Wale ambao hata G-55 wawaeleze vipi wanatia pamba kwenye masikio kwa sababu tu hawataki kutofautiana na the Great Leader".

Ungekuwa umewahi kuwasema viongozi wenu waliowaita wenzao wajinga, wasaliti (na hivi karibuni punda) ninge apologise. Lakini sita apologise kwa sababu si apologise kwa hypocrites ( you are welcome kuliita hili nalo kuwa tusi). Niliwapinga kabla ya uchaguzi na nitaendelea kuwapinga kila nikiona (kwa maoni yangu) kuwa mnapotoka. Na ninafanya hivi kwa sababu nilitegemea mtakuwa better kuliko the alternative. Unfortunately, kila siku zinavyoenda naona hamna tofauti nao. Inasikitisha sana.

Mimi sijawahi kuwa msemaji wa G-55 ila kama kuwatetea dhidi ya uonevu na upotoshaji unaofanywa dhidi ndio kunanifanya niwe msemaji wao basi iwe hivyo.

Amandla...
 
Ldama salumu mwalimu kanunuliwa, sembuse huyu ambaye yupo hot kabisa?
"...yupo hot"?
Hivi anaitwa nani mkuu 'Tabutupu'!
Huyu mtu wako 'hot', hata jina lake silijui; wewe unalijuwa. U-hot wake unahusu kitu gani hasa!
 
Siasa ni imani na kila mtu ana imani yake
Samahani. Nilitaka kupita kimya kimya tu, lakini haya maneno uliyotumia hapa yakabaki yanaichoma moyoni.

Hii "imani" aliyo nayo mtu; ya kwamba ni lazima abaki madarakani kwa njia yoyote ile, hata ya wananchi wake kupoteza maisha yao, hii na yenyewe tuibariki kuwa ni "imani ya mtu" kisiasa?
 
Hutakiwi kumhukumu kwa kutaka awe unavyotaka wewe

Siasa ni imani na kila mtu ana imani yake
Iman gani inayobadilika baada miezi 3 tu toka apambane kupata hiyo nafasi. Arudi nyuma hata kutazama zile video za mkutano mkuu.

Huku ni kukosa maono kama kiongozi.
 
Bony Yai siku yake ni lini, au yeye hayumo?
Sijamsikia Sugu, kasafiri?

Wenje; ile inawezekana ilikuwa geresha tu!

Ni kama wamejipanga kwa zamu kiustadi sana.

Siku ya Mbowe itakapowadia; hapo kazi itakuwa imekwisha. Amani itatamalaki ndani ya CHADEMA, na chama kitaimarika vyema.

Huu mchezo ni kama ulipangiliwa kwa ustadi sana.
Kwanza ilipangwa kumwondoa Mwenyekiti uwanjani, ili kazi ya kuitikisa CHADEMA ianze.
Watu wa Mbowe, wakaanza mmoja baada ya mwingine, kidogo kidogo kila wiki kutangaza kuondoka ndani ya chama, sababu zikiwa ni zile zile walizofundishwa kuzisema.

Wakati huo huo, 'Mtungi' naye kaamuka na lake, kuunga mkono madai ya hao wanao ondoka CHADEMA; na kutangaza viongozi walio teuliwa na Mwenyekiti, ambaye hayupo kutetea lolote, kuwa hawatambuliwi.

Sasa kilicho baki ni kusubiriwa Mbowe, aonyeshe/azindue wanakoelekea hawa wote, sijui itakuwa CHAUMA, au vipi.

Lakini yote kwa yote, kuondoka ndani ya chama virusi hawa ni bahati kubwa sana waliyojaliwa CHADEMA. Hawa watu wangekomalia kubaki ndani ya chama wangeleta uharibifu mkubwa sana.

Huyo mama wa BAWACHA, toka mwanzo alijitangaza yeye ni mtu wa Mbowe; kwa hiyo sasa tunaelekea ukingoni, kumfikia mwamba mwenyewe afunge hii kazi.
Wahusika wa usambaratishaji walianza kutaja kabla G-55 hawajaanza kutangaza 'poor coordination'
 
Hii "imani" aliyo nayo mtu; ya kwamba ni lazima abaki madarakani kwa njia yoyote ile, hata ya wananchi wake kupoteza maisha yao, hii na yenyewe tuibariki kuwa ni "imani ya mtu" kisiasa?

Jibu lilikua kwa mujibu wa maada

Andika uzi wako tutachangia kwa hilo hapo juu
 
Iman gani inayobadilika baada miezi 3 tu toka apambane kupata hiyo nafasi. Arudi nyuma hata kutazama zile video za mkutano mkuu.

Huku ni kukosa maono kama kiongozi.

Kwani tuna limit ya muda wa kuamini?
 
Back
Top Bottom