Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
CCM kauli za kijinga kama hizi kwao ndio sifa , yaani ujinga ni kigezo kikuu cha uongozi huko ccm
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ameshaonesha upande wa CCM inaouficha usionekane.Sijafurahishwa na kauli hiyo na hasa Kwa kuwa inatoa hukumu ya jumla badala ya hukumu Kwa mtu mmoja mmoja.
Falsafa za viongozi kuanzia wa alamu ya kwanza mpaka sasa ni kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana bila kujalisha din zao, kabila zao au vyama vyama ila Leo umetumika ubaguzi wa uchama ambao ni hatari Kwa afya ya demokrasia na siasa safi.
Maamuzi ya wazazi yasiwe sababu ya watoto kuumia au kuumizwa. Kwa sababu Kwa Sheria za nchi yetu mtu aliye chini ya miaka 18 anatambuliwa kama mtoto hivyo Sheria ya uchaguzi pia imemkataza mtoto kutopiga kura.
Kwa mantiki hiyo, kauli ya Mwenyekiti sabaya inaweza kuwa ni chanzo Cha watoto kutopewa haki zao za msingi kama elimu Kwa sababu ya maamuzi ya upigaji kura ya wazazi wao. Tumeanza kuwabagua watu Kwa vyama vyao, tutakuja kuwabagua Kwa kabila zao na mwishowe Kwa dini zao. Hilo likemewe Kwa nguvu zote, Rais ameonesha dhamira ya dhati kabisa kuunganisha watu wote
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.
Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.
View attachment 2922327
Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.
Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.
Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.
Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo.
Hakika, Lazima uteseke sanaWazee kama hawa omba MUNGU asiwe jirani yako ambaye mmepaka mipaka
Hajakosea hawa wenye akili kubwa wahame nchi wakatawale wenzao wenye akili kubwa.In fact hawa akili kubwa tutawatawal hadi kiama .KUDADADEKISasa kama tumewaruhusu watu wenye akili ndogo kututawala, unategemea nini?
HAMIENI MACHAME KWA MZEE MBOWE MUANZISHE HIMAYA YENU MAZIMA
CHACHA WANGWE ANAKUHUSU HAPAHuu unaonekana ni Ukoo wa Wauaji.
Aibu hii kwa kiongozi wa karne ya 21 Tanzania hiiLike father like son, yes ndiyo unaweza kuwaita hawa watu.
Msikilizeni Baba yake sabaya aliyekuwa DC jinsi anavyo mwaga ugoro bila aibu.
Eti ukiwachagua wapinzani serikali haitakuketea maji kijijini kwenu,huu ni wendawazimu wa kiwango cha SGR View attachment 2922294
Chacha wangwe ameingiaje hapa?CHACHA WANGWE ANAKUHUSU HAPA