Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Arusha (Baba yake Sabaya): Ukichagua upinzani serikali haitakuletea maji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akizungumza na Wanachama wa chama chake amenukuliwa akidai kuwa Katiba Mpya haiwezi kuwa na faida ya kuwaletea huduma ya maji.

Kupitia video iliyotolewa na Mtandao wa Siasa za Bongo, amenukuliwa amesema “Katiba Mpya italeta maji hapa? Mnakuja kuleta uchafu tu, na sisi tutakaa hivihivi, tutaendana na wale wa chama chetu, wale mtakaoenda pembeni tuone Mkuu wa Mkoa aje akulete maji, (anageuka kumtazama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella) unajipenda Mkuu? Rais Samia atakukubali tena?”

Chanzo: Siasa za Bongo
Wabunge karibia wote ni ccm wanashindwa nini kupeleka maendeleo
 
View attachment 2922329

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.

Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.

Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.

View attachment 2922330

Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.

Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.

Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo

MY TAKE
Angeongezea tu kwamba, Serikali haitokusanya kodi toka kwa wananchi wanaoishi maeneo yanayoongozwa na wapinzani. Hapo tutaelewana.
Kwani Serikali ni Nani??
 
Piga chini ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine wa aina hiyo.
Inaonesha hauna uvumilivu na kukosekana uvumilivu ni hatari sana ndio maana Rais Kwa kutambua Hilo alipokuja na falsafa za 4R, R mojawapo ni Uvumilivu( Resilience).

Ndio maana napata shida sana kuamini upinzani unafaa kushika dola Kwa sababu Kuna kichaka kimeuficha upinzani na wakishika dola kichaka hicho kitaondolewa na kubaki na sura zao halisi ambazo naona ni za hatari sana.

Kusema kweli nami pia sijafurahishwa na kauli ya Mwenyekiti Sabaya lakini Hilo haliondoi ukweli ni kauli ya kisiasa tu ,Serikali makini haiwezi kuifuata hivyo kama ni kauli tu aliyetoa kauli hiyo anahitaji kuonywa ,kukaripiwa na kukemewa tu. Mwenyekiti wa CCM Mkoa ni mwanasiasa na kauli zake hazina utendaji wala maamuzi ,kama kauli hiyo ingetolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa hapo isingekuwa kauli ya kisiasa tu bali ni agizo ,ni amri na ni shuruti.

Kama Upinzani una mtazamo kama wako wa Kila anayetoa kauli anatakiwa kuadhibiwa Kwa adhabu Kali basi inatosha kusema kama siku upinzani wakishika dola magerezani wataenda wengi na uhuru wa kutoa maoni utadhibitiwa vilivyo
 
Afrika, Afrika.
Kauli kama hizi Ulaya unafunguliwa mashitaka na unafungwa.
Kweli mwafrika ni nyani aliyechangamka
Ulaya ipi na ya mwaka gani unayozungumzia?

PM wa Nertheland wakati wa Kampeni kazungumza lugha za chuki na za kibaguzi kweli kweli dhidi ya Raia wa Nchi hiyo wenye asili ya Indonesia na maeneo mengine jee kesi yake inaendeleaje ?

Huko Marekani wakati wa Uchaguzi wa 2016 tulishuhudia lugha za Shari na za kibaguzi dhidi ya watu weusi kuliko eneo lingine lolote Duniani, jee hukumu ya Trump ilishatoka ?

Acheni kuabudu watu weupe, nao wanakosea kama wengine

wakati wa kura ya kujitenga na EU tumeshuhudia ufedhuli wa Waingereza kuliko tunaoushuhudia maeneo mengi tu
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.

Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.
View attachment 2922327
Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.

Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.
Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.

Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo.
Huu ndio uhaini halisi sasa.

Kiongozi mwenye akili timamu anawezaje kutoa kauli hiyo ya kibaguzi hadharani?

Na hii ndiyo sera na tabia ya viongozi wa CCM.

Hawana hoja yoyote ya kuweza kuwashawishi watu ili waendelee kuwaamini na kuwachagua tena.

Na badala yake wanatumia vitisho vya kipuuzi na kijinga tu kama mbadala wa sera zao zilizoshindwa toka mwaka 1961 kwa viongozi wao wajinga kama huyu mzee..

Huyu akamatwe na kushitakiwa kwa uhaini!
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akizungumza na Wanachama wa chama chake amenukuliwa akidai kuwa Katiba Mpya haiwezi kuwa na faida ya kuwaletea huduma ya maji.

Kupitia video iliyotolewa na Mtandao wa Siasa za Bongo, amenukuliwa amesema “Katiba Mpya italeta maji hapa? Mnakuja kuleta uchafu tu, na sisi tutakaa hivihivi, tutaendana na wale wa chama chetu, wale mtakaoenda pembeni tuone Mkuu wa Mkoa aje akulete maji, (anageuka kumtazama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella) unajipenda Mkuu? Rais Samia atakukubali tena?”

Chanzo: Siasa za Bongo
Hivi huyo mzee ni mzima kweli ?
 
Huyu alitakiwa awe ameshafukuzwa chamani. Anaelewa hata zile R4 za Rais Samia?
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.

Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.
View attachment 2922327
Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.

Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.
Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.

Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo.
Huyo anaweweseka, je, kama mkoa mzima utachagua wapinzani ugeuke nchi huru?
 
Inaonesha hauna uvumilivu na kukosekana uvumilivu ni hatari sana ndio maana Rais Kwa kutambua Hilo alipokuja na falsafa za 4R, R mojawapo ni Uvumilivu( Resilience).

Ndio maana napata shida sana kuamini upinzani unafaa kushika dola Kwa sababu Kuna kichaka kimeuficha upinzani na wakishika dola kichaka hicho kitaondolewa na kubaki na sura zao halisi ambazo naona ni za hatari sana.

Kusema kweli nami pia sijafurahishwa na kauli ya Mwenyekiti Sabaya lakini Hilo haliondoi ukweli ni kauli ya kisiasa tu ,Serikali makini haiwezi kuifuata hivyo kama ni kauli tu aliyetoa kauli hiyo anahitaji kuonywa ,kukaripiwa na kukemewa tu. Mwenyekiti wa CCM Mkoa ni mwanasiasa na kauli zake hazina utendaji wala maamuzi ,kama kauli hiyo ingetolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa hapo isingekuwa kauli ya kisiasa tu bali ni agizo ,ni amri na ni shuruti.

Kama Upinzani una mtazamo kama wako wa Kila anayetoa kauli anatakiwa kuadhibiwa Kwa adhabu Kali basi inatosha kusema kama siku upinzani wakishika dola magerezani wataenda wengi na uhuru wa kutoa maoni utadhibitiwa vilivyo
Hizo lugha za huyo mzee hata Magufuli alikuwa anazitumia hadharani, na kweli aligoma kupeleka maendeleo sehemu za wapinzani, aidha kwa ufinyu wa bajeti, au kwa kusukumwa na huo utashi wake wa kisiasa.

unapokuwa kwenye mabadiliko kisha lugha hizo hizo zikaendelea kutumuka unategemea Nini? Inatakiwa hatua za wazi Ili kuonyesha hatuko kwenye zama hizo. Na adhabu ya kumtoa kwenye nafasi yake itafikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akizungumza na Wanachama wa chama chake amenukuliwa akidai kuwa Katiba Mpya haiwezi kuwa na faida ya kuwaletea huduma ya maji.

Kupitia video iliyotolewa na Mtandao wa Siasa za Bongo, amenukuliwa amesema “Katiba Mpya italeta maji hapa? Mnakuja kuleta uchafu tu, na sisi tutakaa hivihivi, tutaendana na wale wa chama chetu, wale mtakaoenda pembeni tuone Mkuu wa Mkoa aje akulete maji, (anageuka kumtazama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella) unajipenda Mkuu? Rais Samia atakukubali tena?”

Chanzo: Siasa za Bongo
Hz lugha tlishazsikia huko nyuma, za kibaguzi. Katiba mpya = uchafu! Ndo mawazo ya mkuu wa Chama ktk hiyo ngazi! Wanachagliwaje!
 
Huyu mzee anaogopeka mno huko kwenye himaya yake. Naskia ni kipengele kuliko damu yake ile iliosoteshwa jela.
 
Back
Top Bottom