Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Arusha (Baba yake Sabaya): Ukichagua upinzani serikali haitakuletea maji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.

Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.
View attachment 2922327
Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.

Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.
Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.

Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo.
Anataka kuturudisha nyuma huyu mzee.
 
mkoa wetu, hatuna hata mjumbe wa upinzani. Wote ni CCM lakini maisha bado magumu, barabara mbovu, maji hakuna tabu tupu.
 
Kila nikiirudia hii makala, najisikia kichefu chefu kweli kweli.haiwezekani nchi yetu iwe ya matamko kama haya.huu ni UCHOCHEZI
 
Thomas Ole Sabaya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha amesema Chama hicho kamwe hakitapeleka maendeleo na Huduma zingine za jamii kwenye maeneo ambayo Wapinzani watashinda kwani Kila chama kitekelezea Ilani ya chama Chao.

View: https://www.instagram.com/p/C4BY9OorIia/?igsh=MWlhbG56aGlwY3dlcA==

Mzee Sabaya ametoa hadhari hiyo huko Longido.

My Take
Ukitafakari Mzee Sabaya Yuko sawa maana huwezi chagua Chadema harafu udai maendeleo Kwa Ukweli Huwa unauma.

Hata hivyo Hii inge make sense kama tungekuwa na Serikali za Mikoa au Wilaya ambazo zinajitegemea ila Kwa muundo wa Sasa haitekelezeki.

Damu ya Mwendazake Pombe M Bado ipo 😂😂😂😂
 
hii ni kutokana na eneo lenye upinzani hua na uhujumu wa makusudi wa miradi mikubwa na kupelekea hasara kwa taifa nafikiri
 
Like father like son.Mlitarajia nini kutoka kwa kinywa Cha akina sabaya?Ni yaleyale:Ubaguzi,utekaji,ubabe,jeuri dharau.Funy enough ,hawa ndio CCM inaona wanafaa kuongoza watanzania.Wanapewa Kila fursa na vyeo.
 
hii ni kutokana na eneo lenye upinzani hua na uhujumu wa makusudi wa miradi mikubwa na kupelekea hasara kwa taifa nafikiri
Sio uhujumu ni ukweli wa wazi.Yaani watu wachague Chadema harafu wakadai maendeleo ccm,hiyo inaingia akilini?
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.

Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.

Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.

Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.

Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.

Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo.
Mzee anatakiwa ajifunze kwa mwanae. Dunia hii haina ubia na mtu. Ikikukupa mgongo unaweza kutembea uchi
 
Hao ndio ccm sasa tunao wajua, kama wangekua hawaungi mkono hii kauli wangetoka hadharani kumkana na kumchukulia hatua kali za kisheria kwa sababu hii kauli ya kibaguzi Sana, lakini shida kubwa ni kwamba Watanzania hua hatujifunzi ndio maana ccm wanaongea na kufanya wanavyo penda wao,
 
Mbona alipingana na zile 4Rs za mwenyekiti wake taifa huy!
 
Back
Top Bottom