Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Arusha (Baba yake Sabaya): Ukichagua upinzani serikali haitakuletea maji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM kauli za kijinga kama hizi kwao ndio sifa , yaani ujinga ni kigezo kikuu cha uongozi huko ccm
 
Huu ujinga sijui hatakama unavumilika,unasema nikichagua mpinzani huleti maendeleo ilhali KODI ya kufanyia maendeleo inakusanywa kutoka kwa wafuasi wa vyama vya upinzani na wafuasi wa chama tawala,huo si ujinga?
Mzee na baadhi ya wanachama wa CCM,watanabaishe kua MKICHAGUA viongozi wa vyama vya upinzani,muwalipe kodi hao viongozi,wawaletee maendeleo,uone kama kutakua kelele.
Haiwezekani wakusanye pesa kwa kina la KODI,halafu hizo pesa ukafanyie maendeleo kwingine,huo ni uporaji.
Wabadilike.Sisi tusiokua na vyama,ikitokea mpinzani akapita maeneo yetu,tukose huduma muhimu kisa wapinzani wamechaguliwa halafu kodi tulipe,ni haki kweli?
 
Ameshaonesha upande wa CCM inaouficha usionekane.

Kama angelikuwa ameikera CCM, angeshaitwa Kamati ya Nidhamu Dodoma
 
Halafu kuna mpumbavu anasema Sabaya ateuliwe kuwa RC Dar. Majitu kama haya huwa yanafanya CCM wote tuonekane wajinga. Huyu mzee kwa historia yake alikuwa katili kuliko mwanae Sabaya.
 


hii kauli huwa ni ya kijinga sana.maendeleo hayaletwi na serikali bali na wananchi wenye kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kulipa kodi ,na kwa kuchagua viongozi sahihi ambao siyo mafisadi bali wacha MUNGU
 
Simply
CCM haikujiandaa na mageuzi ya vyama vingi
 
Kwa kauli kama hizi.binafsi nazichukulia kama za ubaguzi
Viongozi wanaotoa kauli kama hizi wanapaswa kufunguliwa mashitaka mahakamani ili kuwa funzo.
Haiwezekani kiongozi mmoja anatoka huko anakotoka na kutumia lugha ambazo bila shaka ni ubaguzi na uchonganishi
 
Aibu hii kwa kiongozi wa karne ya 21 Tanzania hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…