Pre GE2025 Mwenyekiti CCM Arusha (Baba yake Sabaya): Ukichagua upinzani serikali haitakuletea maji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huu uwe mwanzo wa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi kama hawa vinginevyo Wananchi wanaweza kuzichukulia kauli kama hizi kuwa wametumwa na kiongozi mkuu wa nchi, hivyo kumchonganisha na umma ambao umekuwa na malalamiko mengi hasa kipindi hiki
 
Kwani wapinzani siyo walipa kodi? wapinzani siyo watanzania?

Hivi watu wenye hizi mentality wanapataje uongozi? Huwa sielewi kabisa.

-Kaveli-
 
Kwani wapinzani siyo walipa kodi? wapinzani siyo watanzania?

Hivi watu wenye hizi mentality wanapataje uongozi? Huwa sielewi kabisa.

-Kaveli-
Wachunge midomo yao hata kama wanalipa kodi
 
Your browser is not able to display this video.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akizungumza na Wanachama wa chama chake amenukuliwa akidai kuwa Katiba Mpya haiwezi kuwa na faida ya kuwaletea huduma ya maji.

Kupitia video iliyotolewa na Mtandao wa Siasa za Bongo, amenukuliwa amesema β€œKatiba Mpya italeta maji hapa? Mnakuja kuleta uchafu tu, na sisi tutakaa hivihivi, tutaendana na wale wa chama chetu, wale mtakaoenda pembeni tuone Mkuu wa Mkoa aje akulete maji, (anageuka kumtazama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella) unajipenda Mkuu? Rais Samia atakukubali tena?”

Chanzo: Siasa za Bongo
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akizungumza na Wanachama wa chama chake amenukuliwa akidai kuwa Katiba Mpya haiwezi kuwa na faida ya kuwaletea huduma ya maji...
Yaani hiki kizazi kina laana.

Huyu mzee ndie baba yake Lengai Ole Sabaya

Limao halija wahi zaa papai.

Sijui Ccm huwa wana tokana wapi na hizi hewa za chooni
 
Kitendo cha CCM na wajumbe wake kumpitisha huyu Mzee kugombea nafasi yake, na kumpa ushindi kwa kupata kura nyingi, hili taifa lazima tuwe serious kujikomboa haya mambo tusiyachukulie kama utani.

CCM kuna DNA ya ushetani ambao lazima uondolewe kwa namna yoyote ile kwa kutumia nguvu ya umma, na wala sio masanduku ya kura.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

Kwani tatizo la nchi kuwa gizani uongozi ni chama gani?

Je wanaoathirika ni chama gani?
 
Yule Mwenyekiti wa CCM mkoa waTabora anazikwa lini?
 
Amchukulie hatua huyo mzee anayeiga tabia za Magufuli kwenye zama hizi.
Kuchukua hatua kupo Kwa namna nyingi ,Kuna namna nyingine zinabaki siri lakini Kuna nyingine sio siri.
Namna ya kwanza, kuonywa. Hii inaweza kuwa siri ama likawa onyo la hadharani
Namna ya pili, kuwajibika. Hapa mhusika anapima upepo na akiona upepo ni mkali anaamua kuwajibika. Kuwajibika pia kupo Kwa namna mbili, kuomba radhi ama kujiuzulu.
Namna ya tatu , kuwajibishwa. Ikibainika kitendo hiko kina athari za Moja Kwa Moja basi Kwa maslahi mapana anawajibishwa.

Sasa nije kwako, unataka hatua ya namna gani ichukuliwe?

Jibu lako tayari ninalo ila nataka nisikie kutoka kwako
 
πŸ‘πŸ€πŸ”Š
 
Piga chini ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine wa aina hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…