Mwenyekiti CCM Nyamagana: Tunawataka DP World bandari ya Mwanza, watoto wa kiarabu wajae

Mkuu mbona huyo mwenyekiti "mnyamagana" kaongea ukweli mtupu?
Kasema " kazi yetu sisi ni hamasa na hamasa mnaiona; Ccm hoyeee!"
Ni mkweli na hajamung'unya maneno.
Tatizo tunapenda kudanganywa ili masikio yetu yafurahi.
 
Kazi ya MC hata ikiwa msibani yeye jukumu lake ni kuleta hamasa tu, hayo mengine mtajua wenyewe
 
Uwekezaji twautaka tena kwa sana tu, tatizo ni pale utaambiwa nipishe ili nikuwekeze!

Chama kinapowatuma makada wake, wawapime na uwezo wao akili.

Sophia Mjema nina uhakika hajui tofauti ya mwalo na bandari, na huyo mwingine sijui zuzu la wapi, anaachoongea anakijua mwenyewe.

Your browser is not able to display this video.
 
duuu! ujinga ni mzigo sana. hivi kweli umeaminiwa kwenye nafasi kama hii unaweza kuongea upuuzi kama huo. yaani uhuru na maslahi ya nchi yeye kipa umbele na dhumni lake ni kuchanganya damu na waarabu. Nyerere na wenzake wangelijua wanapigania uhuru kukomboa watanzania wenye akili kama hizi basi wasingefanya kazi hiyo.
leo ni 2023, akina mkwawa miaka ya 1892 wamepambana kuondoa ukiritimba na unyonyaji. leo anajitokeza mtanzania wa akili za namna hii. ni wajinga ni wajinga na hawafai hata kidogo kuchekewa.
 
Kazi ya MC hata ikiwa msibani yeye jukumu lake ni kuleta hamasa tu, hayo mengine mtajua wenyewe
Mwenyekiti wa chama tawala wilaya unamwita MC? unajuwa mamlaka aliyo nayo ndani ya wilaya na athari zake akiropoka?
 
Tatizo hata hao wanaomtetea Raisi na dp world hawaelewi kilichopo, kinachoendelea kwaiyoo wanaropoka tuu ili waonekane na Mheshimiwa.

Asilimia 90 ya wana CCM wanaotetea uwekezaji huu wa dp World hawana hoja ni mwendo wa kuropoka tu uonekane basi.
 
Aibu! Aibu!
Nafikiri hawakuandaliwa nini wakaongee na wananchi!
Ndio maana wanachoongea ni utumbo mtupu!
Hivi kwanini wasiwe na hiyo mikataba wachambue kama hawa wazalendo wanavyofanya?
 
kuna kale kabibi faiza hapa jf kamekalia ujinga itabidi tumtafutie mwarabu wa kumstili mada zake kama kakosa mume.
 
Mwenyekiti wa chama tawala wilaya unamwita MC? unajuwa mamlaka aliyo nayo ndani ya wilaya na athari zake akiropoka?
Wewe ulitaka ajibu hoja gani kuhusu mkataba wa DP?
Hawana hoja huyo kuamua kuongeza na faida zingine za DP
 
Bado nitaendelea kusimamia hoja yangu kuwa ni wakati sasa Serikali kuwekeza kwenye kuwawezesha Wazawa kuendeleza nchi yao na Wageni watumike tu kama wabia. Historia ya uwekezaji nchini kupitia wageni, hasa kwenye rasimali za Taifa, anayenufaika ni huyo mwekezaji, km makampuni ya uchimbaji madini. Kuendelea kutegemea wageni kwa maendeleo ni moja ya njia kuu ya kudumisha ukoloni-mamboleo.

Hivyo basi, nawasihi Viongozi wa vyama vya Siasa na Serikali kuwa na maono yenye kuondokana na UTEGEMEZI kifikra na vitendo.
 
Kwa upuuzi huu wa watu hawa wa ccm hauna tofauti na mgonjwa mwenye makandokando mengi anaekaribia kufa kwani kuongea vitu visivyoeleweka ndio jadi ya watu wenye makandokando!
 
Mwenyekiti wa chama tawala wilaya unamwita MC? unajuwa mamlaka aliyo nayo ndani ya wilaya na athari zake akiropoka?
mwenyekiti wa chama tawala hana mamlaka yoyote. wala katiba ya nchi haimtambui,badala yake ni chama husika tu ndiyo kinatambua nafasi yake na majukumu yake. kama tutaendelea kuamini kwamba mwenyekiti wa chama ana mamlaka basi tutajifedhehesha mbele ya haki zetu na ni ujinga mkubwa. pili tutawakweza wasiokwezeka. mwenyekiti wa chama ni chamani tu na si umma. mwajiri wake ni chama na anatekeleza ilani ya chama. hapaswi kuingilia wala kuamulisha vyombo vya dola, na wasaidizi wa serikali ngazi zote za mkoa na wilaya. ujinga wetu ndiyo unawapa nguvu hiyo.
 
Ushamba wa maendeleo kwa viongozi wengine ni mzigo kwa wananchi.
 
Tanzania ndo nchi ambayo wajinga wanajiona wenye akili ya kuamua mambo yenye msingi katika taifa
 
Hapa wananchi wanaongelea suala la bandari zetu. Shangaa wapiga debe wanaingiza mambo ya kutoa waarabu. Hivi kweli Mkara angependa kuoa mwarabu badala ya binti mrembo wa Kikara?
 
Kwa pigo hizi 👇👇 unategemea nn!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…