Mwenyekiti CCM Nyamagana: Tunawataka DP World bandari ya Mwanza, watoto wa kiarabu wajae

Mwenyekiti CCM Nyamagana: Tunawataka DP World bandari ya Mwanza, watoto wa kiarabu wajae

Ushamba wa maendeleo kwa viongozi wengine ni mzigo kwa wananchi.
Watawala wakumbuke falsafa ya Baba wa Taifa Maendeleo ni Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora wakati wanapofanya maamuzi yao kuhusu maendeleo.

Kwa mwenendo wa sasa, uongozi uliopo siyo bora maana hauna maono yakuwawezesha watu waitumie ardhi kwa maendeleo yao, badala yake wanaishi na kutenda kitegemezi.
 
Wapumbavu wapo kazini

"Tutakapolimaliza ya bandari ya Dar es Salaam hata Mwanza hapa tuna bandari, tunawataka Waarabu hapa, waje Waarabu DP world sijui na nani, waje hapa watuendelezee bandari ya Mwanza.

"Tukitoka hapa tunahamia Ukerewe, tukitoka hapo ni visiwa vyote vya ukala, wape Waarabu. Waarabu oyeee.

"Tunataka hata watoto wa Kiarabu wajae Mwanza hapa jamani, kuchanganya rangi raha. Waarabu safii, DP World oyeee!


"Kazi yetu sisi ni hamasa, na hamasa mnaiona. Asanteni sana kwa kunisikiliza, Mungu Baba wa Mbinguni awabariki. Chama Cha Mapinduzi kipo madarakani, kitaendelea kuwa madarakani mpaka utukufu wa Yesu Kristo utakapokuja mara ya pili. Hapo vipi?"

Wahamasishaji kazini, kazi kwelikweli!
 
Afunge kirago chake na Familia yake waende wakapige Deki Uarabuni kwanza. Hovyo kabisa. Akirudi atupatie mrejesho.
 
mwenyekiti wa chama tawala hana mamlaka yoyote. wala katiba ya nchi haimtambui,badala yake ni chama husika tu ndiyo kinatambua nafasi yake na majukumu yake...
Majibu umetoa kwa maneno mengi bila sababu yeyote.

Usijifute data, huyo hana mamlaka yeyote ya kidola lakini ana athari za kiutawala kama Ata kuwa mjinga kama alivyo huyo wa Nyamagana.

Utendaji kiutawala unasimamiwa na sera za chama tawala, hivyo katika ngazi ya wilaya mwenyekiti wao wa chama ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa wilaya ambayo huyo DC ni mjumbe tuu na amapokea maelekezo ya chama kupitia kikao ambacho mwenyekiti ni huyo. Jee hujaona athari za kuwa na mwenyekiti mwenye mawazo ya kijinga kama huyu?
 
Hoja zao kwenye mambo mazito, ni za hovyo sana kulikoni mtoto wa kidato cha kwanza!


Embu wasikilize hawa manguli wa ccm wanaotegemewa chamani kutetea mkataba tata wa bandari!
 

Attachments

  • IMG-20230721-WA0003.jpg
    IMG-20230721-WA0003.jpg
    37 KB · Views: 3
Back
Top Bottom