Acha kupotosha
Logic yako ya kuwa Mungu hasikilizi maombi ya wenye dhambi si kweli
Hiyo ni sawa na kusema Mungu hasikilizi maombi ya mtu yoyote
Kwa maana Yesu mwenyewe anasema mahali fulan "wote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu "
Mahali pengine anasema "Mtakatifu ni mmoja tu "
Mkuu hapo penye red naomba nikusahihishe hakuna sehemu maandiko yanasema mtakatifu ni mmoja tu,naamini ulikuwa unarefer Marko 10:17-18,pale Yesu alisema hakuna aliye
mwema ila mmoja tu.
Kwa suala la utakatifu Mungu mwenyewe amesema "iweni watakatifu kwa sababu mimi Mungu wenu ni mtakatifu ( 1 Petro 1: 15-16 )na kuna andiko jingine linasema "tafuteni kuwa na amani na watu wote na huo
utakatifu ambao bila huo hakuna hawezaye kumwona Bwana(Waebrania 12:14."
Suala la Mungu hasikilizi maombi ya wenye dhambi ni somo pana,tatizo tukitaka kufanya mambo makubwa yawe madogo tutapotosha watu.Kwa wale ambao hamjampokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wenu fanyeni maamuzi muda huu,kisha mtafundishwa mafunzo kwa ajili ya kuwajenga.Katika makanisa mengi ay kipentekoste huwa kuna shule za jumapili utafundishwa na kuuliza maswali yako.
Hiki ni kipindi cha mavuno,Yesu yu karibu kurudi tegemeeni watu wengi watakufa Bwana anavuna na shetani naye anavuna,suala la utaenda kwenye ufalme upi kwa Mungu au kwa shetani liko mikononi mwako only ukiwa bado uko hai.hata hapo ulipo unajijua wewe ni wa ufalme upi kwani maisha yako na matendo yako yanakushuhudia utaenda wapi.Hakuna maombi ya kuwatoa watu kuzimu kwenda mbinguni hayo ni mapokeao ya wanadamu na siyo mafundisho ya biblia.
Maisha ni kuchanguia,ndugu yetu Dr.Mengi amemaliza kipindi chake cha hapa duniani,nimebaki mimi na wewe.Fanya maamuzi leo,mpokee Yesu afanyike kuwa Bwana na mwokozi wako ili hata ukifa hiki kifo cha kwanza hakuna shida kwani utaishi lakini kama ukifa uko dhambini jehanamu inakusubili na baadaye ziwa la moto ambayo ni mauti ya pili.
Unahitaji ushauri wa mambo ya kiroho njoo inbox unamaswali yanakutatiza njoo inbox.