Uchaguzi 2020 Mwenyekiti NEC: Uteuzi wa wagombea Urais utafanyika tarehe 25/08/2020 kwa wale wenye Sifa!

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti NEC: Uteuzi wa wagombea Urais utafanyika tarehe 25/08/2020 kwa wale wenye Sifa!

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Kaijage amesema uteuzi wa wagombea Urais wa JMT utafanyika tarehe 25/08/2020.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa ni wagombea wenye sifa ndio watakaoteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Chanzo: ITV habari!
Sifa za kaijage ni mgombea kuwa na PhD ya uonevu uovu uchakachuaji unyanyasaji kwa wapinzani
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Kaijage amesema uteuzi wa wagombea Urais wa JMT utafanyika tarehe 25/08/2020.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa ni wagombea wenye sifa ndio watakaoteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Chanzo: ITV habari!
Huyu mwanajumuiya mwezangu asijichanganye
 
Nafikiri ni wakati muafaka wa kumchuja jiwe hapo, majaji wanatakiwa kuwa makini kabisa na hili.
Jaji kaijage ajiandae kuwa na kesi kwenye mahakama za kimataifa na Pia ajiandae kusomewa Albadiri endapo atawahujumua chadema kama alivyopanga
 
Moja ni kudhaminiwa na watu 2000 katika mikoa 10, walau 2 iwe kutoka Zanzibar!
kwa kutumia sababu hii, basi ni vyama vitatu pekee vina uwezo wa kutimiza hili... ACT, CCM na CHADEMA...

kama itatokea chama ambacho hata hakina impact yoyote mgombea wake akapitishwa... basi haitaleta picha nzuri na yenye kueleweka.
 
Bingwa wa "Mizungu"(mizungu kwenye mchezo wa karata) yupo uwanjani. The Master of manipulation. Haamini wala hakubali katika ushindani, changamoto au kupingwa. Sio sasa bali tangia enzi hizo akiwa anaingia kwenye uwanja wa "mchezo mchafu". Wakaribu yake wanajua na washindani wake wanajua zaidi

Nyavu zimetandazwa kila mahali, mitego ya kila aina ili atakayeonekana anafurukuta kuleta changmoto kwake anaswe na akwame! Vyombo vilivyoundwa na kupewa jina la 'mamlaka za udhibiti" ziwe kwenye mapato, mawasiliano,, mafuta na nishati, na kila unayoijua ndio mitego yenyewe

Kubwa kuliko yote ni "mfumo". Ama anatumia kitengo au baadhi ya kitengo kina mtumikia kwenye jambo ambalo anatakiwa apambane mwenyewe na "kampuni" inayomdhamini kupeperusha bendera yao, tena wanafanya hivyo kinyume kabisa na kiapo chao na miiko ya kazi na majukumu yao

Hakuna namna huyu atatoroka na kombe. Ashinde uwanjani au mezani, haijalishi! Yeye ndio bingwa
 
Form anapewa yeyote atakaye pitishwa na chama chake ,ata wewe Kama hauna sifa chama chako kikikupitisha Basi unachukua form,.kazi inabaki kwao kuangalia sifa zao
Kama ni hivyo nadhani utaratibu huu sio sahihi,kwanini wapoteze mda na rasilimali kumpatia mgombea form kama hana sifa sitahiki? Nadhani mchujo ulitakiwa uanzie hapa kwenye kuwapa form wagombea,,wapewe wenye sifa pengine kama ni kumuengua mgombea iwe kwa pingamizi.
 
Watu waache uzushi, kwenye hii hatua hakuna wa kukatwa ila baada ya huo uteuzi ndipo kuna nafasi kwa wenye kutoa pingamizi kwa mgombea yeyote kuweza kufanya hivyo.

Na atakayewekewa pingamizi lazima tume imsikilize na hata akipigwa chini na hiyo tume bado ana haki ya kwenda mahakamani.

Lakini endapo Lissu atafanyiwa figisu na vyombo vyote hivyo ni Tanzania ndiyo itakayokuwa kikaangoni baada ya huo "Uchaguzi" pamoja na huyo atakayekuwa anafagiliwa aupate urais kiulaini. Itaonekana wazi kuwa yoote hayo yamekuwa "Premeditated", itakuwa ni hatari kwa mustakabali wa taifa hili. Let us wait and see.
 
Sio utaratibu mzuri. Uteuzi wa Tume ni 25.08.2020. Kampeni zinaanza 26.08.2020. Kwahiyo wakati mgombea/mtia nia aliyekatwa akihangaika na rufaaa au hadi huko mahakamani ikiwa atalazimika kwenda waliopitishwa wanaendelea na kampeni!!!?
 
Kama kuna wakati nchi inahitaji maombi na inteligency ya hali ya juu basi ni wakati huu
 
Jibu unalo wewe kwamba kama unajiona unaongozwa n kichaa basi wewe una hali mbaya sana kiakili.
Watanzania wote hali zetu ni mbaya, anaetuongoza alishatamka hadharani kwamba yeye ni kichaa.
 
Jaji kaijage ajiandae kuwa na kesi kwenye mahakama za kimataifa na Pia ajiandae kusomewa Albadiri endapo atawahujumua chadema kama alivyopanga
Kumbe mnajua kabisa kua Mgombea wenu Hana sifa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kumbe mnajua kabisa kua Mgombea wenu Hana sifa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kujipanga kufeli kabla ya mtihani tayari kuna tafsiri nyingi... ila tukumbuke kufaulu ni matokeo ya usikivu, kufata sheria na miongozo pamoja bidii ya muda mrefu, hakuna miujiza hapo
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Kaijage amesema uteuzi wa wagombea Urais wa JMT utafanyika tarehe 25/08/2020.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa ni wagombea wenye sifa ndio watakaoteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Chanzo: ITV habari!

Kwani si ndio jambo la kawaida kuteua mwenye sifa, sasa msisitizo wa nini?
Halafu anayetetea kiti ndio rahisi kuangalia kama ana sifa, je hajavunja katiba ndani ya miaka mitano iliyopita?
 
Back
Top Bottom