Bingwa wa "Mizungu"(mizungu kwenye mchezo wa karata) yupo uwanjani. The Master of manipulation. Haamini wala hakubali katika ushindani, changamoto au kupingwa. Sio sasa bali tangia enzi hizo akiwa anaingia kwenye uwanja wa "mchezo mchafu". Wakaribu yake wanajua na washindani wake wanajua zaidi
Nyavu zimetandazwa kila mahali, mitego ya kila aina ili atakayeonekana anafurukuta kuleta changmoto kwake anaswe na akwame! Vyombo vilivyoundwa na kupewa jina la 'mamlaka za udhibiti" ziwe kwenye mapato, mawasiliano,, mafuta na nishati, na kila unayoijua ndio mitego yenyewe
Kubwa kuliko yote ni "mfumo". Ama anatumia kitengo au baadhi ya kitengo kina mtumikia kwenye jambo ambalo anatakiwa apambane mwenyewe na "kampuni" inayomdhamini kupeperusha bendera yao, tena wanafanya hivyo kinyume kabisa na kiapo chao na miiko ya kazi na majukumu yao
Hakuna namna huyu atatoroka na kombe. Ashinde uwanjani au mezani, haijalishi! Yeye ndio bingwa