Mwenyekiti Ulinzi na Usalama (W) anaporatibu vurugu wilayani

Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
Mkuu Chakaza, hicho kijamaa Ole kwanini kisipigwe ambush tukifundishe adabu
 
mie najiuliza sipati jibu swali jepesi kbs, kama serikali (ccm) haitaki ushindani wa vyama vingi ni kwann wasiufute huu mfumo...mbona kwao kwakuwa wana dola na mamlaka ni jambo jepesi sana!.
Wezi wakubwa wataiba nini wakiufuta? Maana kama serikali wanaiendesha kwa 40% misaada toka nje na itafutwa?
Hakuna kukopeshwa wala kusaidiwa watafanyaje?
 
Ikiwa walikuwa nyuma police, kweli ni jambo la ajabu na amani tuliyo nayo haina muda itaondoka inatakiwa akili kubwa itumike kulinda hili
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
Jana nilusema mapema kabisa kwamba ile ilikua organised scene.. Na alie organise ile ndie kachoma ofisi Arusha.. Sasa kama JPM ana taka uchaguzi huru na wa haki OCD na DC wa Hai wakae pembeni kulinda heshima yake na chama chake CCM
 
Kila jambo na wakati wake na muda wake, kuna taarifa za wale vijana waliokuwa wametumwa kurusha mawe kwenye mkutano wa chadema huko Arusha wanajisifia kuwa wametumwa na mkuu wa wilaya wa Hai Ole Sabaya hivyo wanamlinda yeye na wao

Je, kama Taifa tunakubali mtu mmoja mkuu wa wilaya wa Hai kuanza kutugawa,

Je, ole Sabaya anafahamu gharama za kujenga nchi hii ,Tulipoteza ndugu na jamaa vita vya uganda bado tuna maumivu,Tulipoteza wazee vita vya majimaji,Tulipoteza wazee wetu hapo Iringa Chifu Mkwawa akitetea nchi hii,Yeye ni kijana wa juzi tu sasa amejigeuza amiri jeshi mkuu wa nchi kuidhinisha mapigano kati ya ccm na chadema

Huyu adhibitiwe mapema,Anafahamu gharama ambazo watu wametumia kujenga nyumba zao na familia sasa yeye anataka kuziteketeza kwa masaa machache nyumba na Familia za watanzania mitaani

Je sasa ni mapambano kati ya chadema na ccm mitaani tunamoishi ,Kweli familia zitapona au ndio mambo ya wahutu na watusi sabaya mkuu wa wilaya anayaleta Tanzania

Je ?Mkuu wa wilaya Hai ole sabaya pamoja na polisi wa eneo hilo sasa rasmi wao ndio kitovu cha vurugu zitakapotokea nchi nzima

Kwa maslahi ya Taifa na tunaoona mbali historia itaandika kuwa mbegu ya fujo ya haradani iliyopandwa na mkuu wa wilaya Hai Ole Sabaya sasa inakwenda kumea fujo nchi hii

Kwa maslahi ya Taifa mtu huyu hafai kuwa kiongozi,Yeye na OCD wa Hai wafukuzwe kazi

Je, Vijana wa chadema wakianza kuchoma moto nyumba za wanaccm na ccm kuchoma moto nyumba za chadema nani atapona huku mitaani

Kwa taarifa ni kwamba watu wanapanga kulipa visasi mitaani,Je nyumba na Familia zetu zitapona

Hii chuki ya ole sabaya ni kwa maslahi ya nani?

Tulizoea kusemana mitaani kama simba na Yanga hata siku moja mitaani hatujawahi tupiana mawe kisa simba au Yanga

Hizi amri za Ole sabaya za kutengeneza vita anazitoa wapi na kwa mamlaka ipi?

Je kitendo cha ole sabaya kukusanya vijana wa ccm na kuwajaza upepo wapigane na vijana wa chadema nchi hii itakalika
 
Kama vijana wamepata ajira kuna ubaya gani?.
Kurusha mawe pia ni zoezi,na tunahitaji watu wafanye mazoezi
 
Ilikuwa inaitwa tume ya judge Robert Kissanga.
Ilichunguza sakata la Wananchi wa Nyamuma wilaya ya SERENGETI.
Very sad and unforgettable.
 
Hadi muda huu hakuna taarifa iliyo tolewa sii na OCD, RPC wala IGP. Lakini ingekuwa ni Chadema waliharibu unge kuta labda hata Rais wa nchi amesha toa tamko.

Kuna kitu kwenye hii nchi hakiko sawa na viongozi wa dini badala ya kutupumbaza kutoa tunzo tunatakiwa kukemea kwa nguvu zetu zote. Amani ya hii nchi haiko mikononi mwa Rais na Ccm peke yao bali iko mikononi mwa Watanzania wote.

Niaibu mkuu wa wilaya kuratibu uvamizi halafu hakuna kukemea.. Yana karibia masaa 24/sasa hakuna kauli ya serikali kuhusu hili jambo.
Au mna andaa taarifa kwamba walijivamia wenyewe kama mlivyo tuaminisha Mbowe alijibunja mguu mwenyewe??
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
Jitihada za makusudi zifanyike kuweka ushahidi wa matukio yote wanayotendewa wapinzani. Kule Mbeya inasemekana wamempora Mh.Sugu form ya kugombea ubunge.
Vyombo vya ulinzi vinapojigeuza kuwa wahalifu,tusitegemee Amani kudumu.
 
Kile kikundi katika video wanajitapa kuwa wapo tayari kumlinda Magufuli na DC wa Hai

Kwa ushahidi huu ni kuwa kile kikundi kimetumwa na Ole Sabaya kuvuruga mkutano wa CHADEMA

Ole Sabaya ameshindwa siasa za kiistaarabu,na mamlaka ya uteuzi bado inaendelea kumuangalia tu

IGP Sirro usipokuwa makini ,ukicheka na nyani utavuna mabua

Ole sabaya na kikundi chake wafikishwe kwenye vyombo vya dola kujibu mashtaka,hakuna aliye juu ya sheria za nchi
 
Back
Top Bottom