Mwenyekiti Ulinzi na Usalama (W) anaporatibu vurugu wilayani

Mwenyekiti Ulinzi na Usalama (W) anaporatibu vurugu wilayani

Huyo mkuu wa wilaya hiyo nafasi kalazimisha.ni muhuni kama wahuni wengine
 
Kile kikundi katika video wanajitapa kuwa wapo tayari kumlinda Magufuli na DC wa Hai

Kwa ushahidi huu ni kuwa kile kikundi kimetumwa na Ole Sabaya kuvuruga mkutano wa CHADEMA

Ole Sabaya ameshindwa siasa za kiistaarabu,na mamlaka ya uteuzi bado inaendelea kumuangalia tu

IGP Sirro usipokuwa makini ,ukicheka na nyani utavuna mabua

Ole sabaya na kikundi chake wafikishwe kwenye vyombo vya dola kujibu mashtaka,hakuna aliye juu ya sheria za nchi
Ushahidi gani atakalo mwaka Sabaya papaya. Tanzua taarifa yako ili ipate mashiko
 
Daah Inavyoonekana hao watu waliletwa na Lisu kuwafanyia fujo wakazi wa hai.

Ni ajabu sana mgombea wa nafasii ya Urais kutembea na vikund vya wahuni
We ulishapigwa stroke wala huna madhara yeyote
 
Jitihada za makusudi zifanyike kuweka ushahidi wa matukio yote wanayotendewa wapinzani. Kule Mbeya inasemekana wamempora Mh.Sugu form ya kugombea ubunge.
Vyombo vya ulinzi vinapojigeuza kuwa wahalifu,tusitegemee Amani kudumu.
Ni hivyo? Mbona habari za awali zilisema kuwa mpango ulikuwa huo lakini hawakufanikiwa na fomu ziko salama?
 
Aisee...
Sasa hao wanaojiita "makamanda"huko cdm wao walikaa kimya tuu.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
Binafsi naona kama kuna mipango dola inajaribu kufanya hivyo ili cdm waonekane ni watu wa fujo ili kukipa doa cdm kuwa ndio wanaochangia uvunjifu wa amani
 
YULE ALIEFANYA HIVYO ALISHAZAWADIWA UKUU WA MKOA WA MTWARA.
Yaani hii ndio inaonyesha wazi kuwa uchafuzi huu wa hawa ma DC Rais Magufuli anamkono wake wa baraka. Mbona wale wote wafanyao mambo ya ajabu dhidi ya upinzani wanazawadiwa vyeo? Halafu huyu ndio TAG kama taasisi ya dini inamzawadia Tuzo? Nasikia na ile kamati ya kihuni ya Amani nayo kesho kutwa wanampa tuzo, wanashindana.
Magu hastahili kabisa kupewa kura hata ya huruma, ni mharibifu wa Amani na tungekuwa nchi hii tuna asili ya visasi na chuki basi sasa hivi tungekuwa zaidi ya Burundi
 
sasa matokeo yake green guard wawili wamekufa kwenye hilo tukio, nadhani Ole Sabaya atazihudumia familia zao.
 
Yaani Ni Sawa Na Mwizi Akatukio Na KITAMBULISHO chake Cha Kupiga Kura...

Maandishi Ukutani Yanatutanabahisha kuwa WALE VIJANA wametengenezwa na CHADEMA....
Ni movie....
Ni Setup Ya KISIASA...
 
Mh Rais wangu Magufuli, Mwenyekiti wangu mpendwa, nakupenda sana, kwa hili la Wilaya ya Hai, tunakuomba chukua hatua, DC mtimue kabisa, Sabaya atakuharibia kabisa kabisa, na atasababisha watu watuchukie kabisa na kupunguza kura zetu, mtimue DC, anakuharibia kabisa Mh. Rais wangu.. Mm sisemi tena.
Bora hata wewe umeliona hili na kuamua kusema ukweli.
Na sio hili moja tuu, sema ukweli kwenye yote utabarikiwa. Nakuhakikishia siku yako ya Leo utajisikia tofauti Fulani moyoni, maandiko yanasema UKWELI UTAKUWEKA HURU.
 
Kwa vile bongo zenu zilivyo BASHITE angekuwepo mngesema ndiye aliyeratibu.

Yaani ngome ya MWENYEKITI WA CHAMA kikuu anayependwa watu wanapata wapi ujasiri wa kufanya hayo waliofanya?
 
Chadema Wamekuwa Kama Marekani Kipindi Walipoishambulia Meli Yao Iliyokuwa Pwani Ya Guantanamo Halafu Wakamsingizia Fidel Castro na CUBA yake...

WAFANYE Chadema halafu wawasingizie Sabaya na CCM...

Daah Mmetufikisha Pabaya Nyinyi Chadema looh hatareee...
 
Kw
Wewe umeona hilo, angalia na hili, Chadema wana habari kuwa watafanyiwa fujo Hai, kabla hawajaenda Hai, Wanachomewa Office yao ya Kanda.

Maswali: kama walikuwa na habari ya fujo, mbona wasipeleke mashtaka polisi, Pili: Ofisi nzima ya kanda Haina walinzi , jamani hii ikoje?????

Tatu: kwanini matukio yote haya yatokee kanda hii tena Arusha mjini na Hai, kwanini isitokee Ddma,Singida,Shinyanga, Musoma etc......

Chadema hii michezo yenu ni ya kizamani imeshapitwa na wakati.
Kwa hiyo unataka kusema kuwa wamechoma ofisi yao wenyewe, na kule Hai wamejiletea fujo wenyewe?
 
Wewe umeona hilo, angalia na hili, Chadema wana habari kuwa watafanyiwa fujo Hai, kabla hawajaenda Hai, Wanachomewa Office yao ya Kanda.

Maswali: kama walikuwa na habari ya fujo, mbona wasipeleke mashtaka polisi, Pili: Ofisi nzima ya kanda Haina walinzi , jamani hii ikoje?????

Tatu: kwanini matukio yote haya yatokee kanda hii tena Arusha mjini na Hai, kwanini isitokee Ddma,Singida,Shinyanga, Musoma etc......

Chadema hii michezo yenu ni ya kizamani imeshapitwa na wakati.
Na wew usiwe box!Huoni wanajaribu kuonesha kuwa CDM haikubaliki kwenye eneo ambalo ilikuwa ngome yake?Kanda ya kaskazini imekuwa ngome ya CDM kwa miaka mingi,sasa uhuni unafanyika kuwaondolea imani kwa wananchi!
Jaman kama hukipendi chama au mgombea,kaoneshe hizo hasira kwenye sanduku la kura!
Hawa wahuni akina Sabaya wanafanya michezo hii ili CCM iendelee kubaki madarakani maana wananufaika nayo kimaslahi!Sasa wewe kijana mlalahoi unatumwa kufanya vurugu nawe unapeleka tumbo,jinga kabisa!
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
Igo Sirii Andakava bado hajakutana na wahuni wa kanda maalum huyo.
 
Sasa wale mabaunsa walikuwa wapi? walinzi wa mbowe walikuwa wapi? hai bila kutoa hela ya mbege watakudunda tu, hata mbowe analijua hilo,
Mbowe amekua mbunge wa Hai kwa mihula tofauti, hakuwahi kufanyiwa vurugu wakati wowote ule ila katika kipindi hiki ambacho Sabaya ni DC ndicho alifanyiwa vurugu sawa walizofanya jana kwa Tundu Lisu.

Hiyo Mbege wachaga wa Hai wameanza kuinywa 2016 hadi leo au ilikuwepo toka enzi za mababu!!?
Mbuyu ulianza kama mchicha, hii chuki tunayo ipanda miongoni mwa vijana itakuja kuzalisha kilicho tokea 1994 kule Rwanda , halafu tunajidai tuna amani na utulivu.

Amani ni TUNDA la HAKI kama hakuna HAKI hakutakua na AMANI
 
Chadema Wamekuwa Kama Marekani Kipindi Walipoishambulia Meli Yao Iliyokuwa Pwani Ya Guantanamo Halafu Wakamsingizia Fidel Castro na CUBA yake...

WAFANYE Chadema halafu wawasingizie Sabaya na CCM...

Daah Mmetufikisha Pabaya Nyinyi Chadema looh hatareee...
Wewe ni mpumbav!Hao waliofanya fujo wangekuwa CDM ,polisi isingewaacha!
 
Miaka 5 ya kufanya kampeni wao tu haijawatosha?
 
Back
Top Bottom