SOURCE WASAFI TV
Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.
Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhan wakati wa ziara yake wilayani Ngara alipokutana na viongozi pamoja na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge Aprili 16, Mwaka huu.
Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia pamoja na viongozi wengi huku wengine wakiwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambapo amelitaka jeshi la polisi kutowatafuta watu hao pindi watakapopotezwa.
Pia soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri