Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Najua tayari Mama ( Mwenyekiti Taifa ) ameshaandika jina lake na iwe isiwe Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Mpumbavu Faris Buruhan kwa Kitendo chake tu cha kusema kuwa CCM itawapoteza ( yaani itawaua ) wale Wakosoaji wote wa Serikali ya Rais Samia na kwamba Poilisi Tanzania wala Wasipoteze muda wao Kuwatafuta.
 
Viongozi wa UVCCM Kagera wametoa Onyo Kwa watu wote wanaomtusi Rais Samia Kwa kuwataka Polisi wasijihangaishe kuwatafuta watu ambao Wanaomtukana Rais Samia endapo watapotea.

Onyo Hilo limekuja huku pia Waziri wa mambo ya Ndani akionya watu waache matusi na wafanye siasa vinginevyo hatua Kali zitachukuliwa.

UVCCM wameapa kumlinda Rais na Mwenyekiti wao Kwa gharama zozote.

My Take
Naunga mkono hoja,matusi Kwa Viongozi sio siasa, wahusika washughulikiwe.
Acha upuuzi wewe! Kutusi mtu yeyote awe kiongozi au vuvuzela as you are ni kosa kisheria na kinyume na utamaduni wetu.
Lakini hata wakati wanawatusi viongozi wa upinzani kama Mbowe, Maalim Seif, Mbatia nk hatujawahi kusikia tamko la wafuasi wao kuwa watawapoteza watu, iweje leo kiongozi anayefahamika anatishia uhai wa wengine kwa matusi hayohayo?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Nani alikuwa anawatusi wewe ropo ropo? Matusi ni utamaduni wa Wapinzani sio CCM
 
Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.

Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhan wakati wa ziara yake wilayani Ngara alipokutana na viongozi pamoja na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge Aprili 16, Mwaka huu.

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia pamoja na viongozi wengi huku wengine wakiwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambapo amelitaka jeshi la polisi kutowatafuta watu hao pindi watakapopotezwa.

Pia soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

SOURCE WASAFI TV
Watawamaliza them wataanza kujipoteza wenyewe kwa wenyewe. Wana reason kama wapo UCHI...uchawa ni noma.
 
Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.

SOURCE WASAFI TV
Duuh..
Hao uvccm watatumia sumu au watateka na kuua?!
 
Elimu ya uongozi iangaliwe kwa jicho la pili,taasisi zinazotoa elimu ya uongozi Kama haya ndio yapo kwny mitaala yenu fumueni hiyo mitaala na Kama sio hayo mnayofundisha kuna tatizo kubwa Sana baadhi ya watu wanaopewa dhamana.Mungu atawalipa kwa matendo yenu .
 
Bora hata uvccm ya akina Nape Nnauye ilikuwa inajitambua. Siyo hii ya hawa watoto waliozaliwa kwenye yale matamasha yao haram ya mbio za mwenge.

Msameheni tu bure
Maana anaonekana hajui asemalo.
 
UVCCM mjitafakari. Hizi siasa za kupotezana sio maono ya mwenyekiti Mama Samia. Mama hana siasa za kipumbavu kama hizi.

TUKIWAPOTEZA WANAOMTUKANA RAIS SAMIA POLISI MSIWATAFUTE

Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.

Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhan wakati wa ziara yake wilayani Ngara alipokutana na viongozi pamoja na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge Aprili 16, Mwaka huu.

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia pamoja na viongozi wengi huku wengine wakiwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambapo amelitaka jeshi la polisi kutowatafuta watu hao pindi watakapopotezwa.

@sirallawi
#WasafiDigital
Pumbavu kabisa hilo jamaa!
 
Back
Top Bottom