Masahihisho kidogo: Ni mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Rorya.
Kosa: Wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2020; alishtakiwa kua alimtusi kada wa CCM. Kesi iliamriwa mwaka huu mwezi wa tatu kama sijakosea mahakama ya mwanzo Shirati na Hakimu alitoa hukumu ya kua mwenyekiti wa Chadema alishinda kesi.
Baadae kada wa ccm alikata rufaa mahakama ya Hakimu mkazi Tarime.
Leo ukumu imetoka na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya Rorya amekutwa na hatia ambapo amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini TZS 200,000/. Hivyo amelipa faini na anaendelea na maisha mengine.