Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekamatwa na Polisi baada ya kuwasili Magomeni Mapipa akiwa anazungumza na wanahabari kuhusu maandamano
Ikumbukwe kuwa Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, akiwemo kada wake, Ali Kibao.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.
Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo kuhusu suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.
Amesema jambo lingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho, waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo.
Soma Pia: LIVE Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024