Pre GE2025 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akamatwa uwanja wa Ndege Songwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Mhe. John Pambalu wamekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege Songwe wakijiandaa kuelekea Mbeya, Ukamataji huu umeongozwa na RPC wa Mbeya.

========================

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema anasema “Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu tangu akamatwe (jana Agosti 11, 2024) hatujui yuko wapi, Polisi hawasemi, hatujui kama yeye na wenzake wamekula au la, pia Lissu ana dawa anazotumia kila siku kutokana na majeraha ya risasi na sijui kama amekunywa dawa.”

Ameongeza “Kutokana na hali hiyo, Mbowe alilazimika kusafiri kwenda Mbeya kukutana na Polisi, alipowasili Saa 4 Asubuhi akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, John Pambalu, Polisi wakawakamata na hatujui wako wapi.”

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Benjamin Kuzaga simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyesema “RPC yupo kwenye kikao”

Pia soma=> Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Pamoja na kwamba siungi mkono
Kitendo Cha Mbowe kungangania madaraka au kutengeneza loop ya kumiliki chama Kama kampuni

Lakini nalaani vitendo vya kuanza kukamata viongozi wa upinzani

Police inaonesha kujaribu kundoa utulivu na siasa safi zilizoanza
 
Mda wa kufanya kazi sio maandamano yasiyo na Tija Wala yasiyoisha.

Uchumi uliodumaa hauleti pesa 👇👇

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1822538145541259454?t=rxq83rlcvJMiBDRHy9Jh9w&s=19

..masikini wanaongezeka kwa kasi kuliko ukuaji wa mapato na fursa za ajira.

..kwa taarifa yako hakuna serikali ya Ccm tangu Mzee Mwinyi haikuongeza ukusanyaji wa mapato, miundombinu, uwekezaji, au ajira.

..Tatizo ni kwamba wote wameshindwa kukidhi MAHITAJI ya wakati. Uchumi wetu haukuwi kwa kasi itakayoweza kuondoa umasikini.
 
Weka data zinazothibitisha madai Yako ya ujinga na chuki
 
..data ulizozileta zinathibitisha hoja yangu.

..vijana hawana ajira, na umasikini unaongezeka.

..ndio maana Chadema wakikohoa kidogo tu, serikali inaanza ku-panic, na Polisi wanafanya mambo ya ajabu.
 
Ndugu yangu John Mrema, vipi Mh. Tundu Lisu amekupa mamlaka ya kuisemea hali ya afya yake? Au baadae mtayamaliza kichama.
 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Mhe. John Pambalu wamekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege Songwe wakijiandaa kuelekea Mbeya, Ukamataji huu umeongozwa na RPC wa Mbeya.

========================

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema anasema “Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu tangu akamatwe (jana Agosti 11, 2024) hatujui yuko wapi, Polisi hawasemi, hatujui kama yeye na wenzake wamekula au la, pia Lissu ana dawa anazotumia kila siku kutokana na majeraha ya risasi na sijui kama amekunywa dawa.”

Ameongeza “Kutokana na hali hiyo, Mbowe alilazimika kusafiri kwenda Mbeya kukutana na Polisi, alipowasili Saa 4 Asubuhi akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, John Pambalu, Polisi wakawakamata na hatujui wako wapi.”

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Benjamin Kuzaga simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyesema “RPC yupo kwenye kikao”

Pia soma=> Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Nimeipenda hii inaamsha hasira za wananchi
 
Samia nchi imemshinda asaidiwe atuachie Tanganyika yetu arudi kwao akale urojo
Hahahaha mlivyokuwa mnashangilia kusema Dkt Magufuli alikuwa katili na mkafanya sherehe mnadhani wenye mamlaka walifurahia??? Hahaha Mbowe na genge lake mlikosea sana. Mlipaswa kuomboleza
 
..hata Mama Abduli alifurahia mpaka akamtangaza kuwa ameondoka kwa covid.

..mambo haya hayana uhusiano na Jiwe.

..Serikali inawaogopa wananchi, na wana hofu wakikutana na Chadema watapewa elimu.
 
Samia nchi imemshinda asaidiwe atuachie Tanganyika yetu arudi kwao akale urojo
Mimi naunga mkono kukamatwa kwa hao watu wanaochanganya siasa na mambo ya kihuni. Hatutaki vurugu . Wanaotaka vurugu wahamie Kenya.
 
Samia nchi imemshinda asaidiwe atuachie Tanganyika yetu arudi kwao akale urojo
Hao chadema watuache na amani yetu. Kama wanaotaka kuandamana waende Kenya ndio nchi ya maandamano. Hapa TANZANIA MTU MZIMA HATISHIWI NYAU. Waziri mkuu pinda alishasema :" Wapigwe tuu" hamna namna.
 
Hahahaha mlivyokuwa mnashangilia kusema Dkt Magufuli alikuwa katili na mkafanya sherehe mnadhani wenye mamlaka walifurahia??? Hahaha Mbowe na genge lake mlikosea sana. Mlipaswa kuomboleza
Tuliomboleza kifo cha ben sanane na kushambuliwa lisu ilitosha.
 
Back
Top Bottom