Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu leo Desemba 31, 2022

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu leo Desemba 31, 2022

Approach ya mbowe naielewa sana ila kutokana na ulafi wa baadhi ya wenzake ndani ya chama wanahisi kama kuna namna anafaidika na ikulu ya mambuzi.
CHADEMA kinafaidika nini na hizo picha za Mbowe na wenzake.

Au ndiyo rasmi wameshajisajili kwenye kundi la vyama shikizi ???
 
Wapinzani wasipoweza kufanya angalau mikutano ya hadhara, wajue wanachezewa tu.
Wameshaanza kuchezewa siku nyingi ila bado hawajalijua hili.

Majibu ya kikosi kazi yalistahili waamue kuondoka kwenye mazungumzo.
 
Chadema mvimbe na mpasuke, Mbowe anafanya Siasa za kisasa, sio za Mdude Wala maranja Masese.

Tanzania hoyeee..

Nisikie mtu anasema mbona hakutuambia anaenda huko

Hakuna maridhiano hapo bali ni utapeli wa mchana kweupe. Hao akina Mbowe ndio vinara wa kuua upinzani. Hakuna maridhiano huku bado unanyimwa uhuru, hayo sio maridhiano bali ni dawa ya usingizi ili kulaza upinzani.
 
Hizi ndiyo siasa. Vyama vya upinzani viko kikatiba na wapinzani ni wananchi wenzetu.

Ila yule shetani wa Chato aliufanya upinzania ni uadui. Asante Mungu kwa kusikia maombi yetu hatimaye akasepeshwa jehanam mnamo 17/ 03/ 21
Hamna kitu hapo wenzio walushalamba hasali. Ww baki kupiga domo humu. Alafu usijisahaulishe Mbowe alipigwa kesi ya ugaidi kipindi cha maza
 
Hakuna maridhiano hapo bali ni utapeli wa mchana kweupe. Hao akina Mbowe ndio vinara wa kuua upinzani. Hakuna maridhiano huku bado unanyimwa uhuru, hayo sio maridhiano bali ni dawa ya usingizi ili kulaza upinzani.
Na ndicho walichokitaka wenzao wameshakipata.

Vuguvugu la katiba mpya limekufa kifo cha Mende

Vuguvugu la tume huru ya uchaguzi pia limekufa kifo cha mende

Halafu wafuasi wao wanafurahi picha za Mbowe kuwa ikulu tu.

Wonders shall never cease.
 
HISTORIA KUELEKEA KUIHUKUMU CCM KWA MATENDO YAKE

Leo tarehe 31.12.2022 dhamira ya CCM imewekwa kikaangoni kupitia viongozi wao wa juu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan na makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu. Abdulrahman Kinana.

Hii ni kumbukumbu katika maktaba ya online kuwa tarehe 31.12.2022 CCM inatamani kuleta maridhiano na kuwa CCM ambacho ni chama dola isipofanya hivyo kubadilika kuwa chama cha kweli cha kisiasa ili kushindana kupitia ushawishi na siyo kutegemea vyombo vya dola na katiba hii mbovu ya viraka viendelee kuwaweka madarakani, basi historia na nguvu ya umma vitachukua mkondo wa asili wa mabadiliko hivyo utawasomba na kuwatupa nje ya siasa na CCM kusahaulika katika historia ya kweli ya vyama vya siasa Tanzania

PICHA KATIKA MAKTABA YA ONLINE TAREHE 31.12.2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu. Abdulrahman Kinana wakati akipokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.
 
IMG-20221231-WA0051.jpg
 
Back
Top Bottom