Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akutana na Rais Samia Ikulu leo Desemba 31, 2022

View attachment 2464661

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

View attachment 2464667
======

Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi , ambapo Rais Samia amepokea Taarifa ya Maridhiano hayo

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
Wanaridhiana nini kama wao ccm ndio chama chenye ridhaa ya wapiga kura? Kama nchi imewashinda bora waitishe uchaguzi wa mapema sio kuwasikiliza chadema wakati hawana ridhaa ya wananchi.
 
Ulambaji wa asali unaendelea kimya kimya! Ruling class wanafakamia mzinga. Kijana wa masikini anajifanya anapigania chama, anadakwa na polisi. Anavunjwa miguu eti anakipigania chama😂😂😂😂
 
pande mbili za majadiliano

Mwenyekiti + Makamu VS Mwenyekiti

#AsaliAsali
 
Hizi ndiyo siasa. Vyama vya upinzani viko kikatiba na wapinzani ni wananchi wenzetu.

Ila yule shetani wa Chato aliufanya upinzania ni uadui. Asante Mungu kwa kusikia maombi yetu hatimaye akasepeshwa jehanam mnamo 17/ 03/ 21
Na wewe kila siku shetani wa chato,shetani wa chato utakufa mdomo upande huku unasema shetani wa chato wakati mwenyewe ni shetani.
 
Hizi ndiyo siasa. Vyama vya upinzani viko kikatiba na wapinzani ni wananchi wenzetu.

Ila yule shetani wa Chato aliufanya upinzania ni uadui. Asante Mungu kwa kusikia maombi yetu hatimaye akasepeshwa jehanam mnamo 17/ 03/ 21
Ndioooooo
 
View attachment 2464661

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

View attachment 2464667
======

Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia leo 31/12/2022

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba huu ndio ule ule mwendelezo wa Majadiliano ya Maridhiano kuelekea Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi , ambapo Rais Samia amepokea Taarifa ya Maridhiano hayo

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana
Ni Mbowe pekee anayeaminiwa huko CHADEMA kuhusu maagizo anayopewa. Hairuhusiwi kuwepo mtu mwingine yeyote toka chama hicho akiambatana na Mbowe.
Tatizo linaanzia hapo!
 
Kesi ya ugaidi imemtoa kwenye reli Mbowe.

Mpaka sasa CCM wanamchezea pengine akiwa anajua au bila kujua.
Hapana.
Ni zaidi ya "kesi ya ugaidi"; kuna mambo ya kisiasa anayofanya Samia yanayomwondoa upepo Mbowe.

Hana namna, bali tutaona njia atakazotumia kujisalimisha yeye na chama chake, muda siyo mrefu toka sasa. Hii itakuwa ndani ya mwaka huu huu wa 2023.

Sasa baada ya kufanya hivyo, sijui kama CHADEMA, kama tuijuavyo itaendelea kuwepo.
 
Hapana.
Ni zaidi ya "kesi ya ugaidi"; kuna mambo ya kisiasa anayofanya Samia yanayomwondoa upepo Mbowe.

Hana namna, bali tutaona njia atakazotumia kujisalimisha yeye na chama chake, muda siyo mrefu toka sasa. Hii itakuwa ndani ya mwaka huu huu wa 2023.
Mambo yapi hayo ?
 
Ni Mbowe pekee anayeaminiwa huko CHADEMA kuhusu maagizo anayopewa. Hairuhusiwi kuwepo mtu mwingine yeyote toka chama hicho akiambatana na Mbowe.
Tatizo linaanzia hapo!
Chadema ilishajadili jambo hili na kuweka msimamo , Mbowe ni mbeba faili la chama tu
 
Hizi picha wenzake wanazitumia vibaya. Bora akutanenao kimyakimkya tu na matokeo yakiwa mazuri, ndio ajitokeze hadharani kupiga nao picha.

Pia, Mbowe akumbuke kauli za Makamba na kikwete za hivi kariibuni kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.

Kinachofanyika hapa ni sawa na kile ambacho CCM hukifanya kwenye uzinduzi wa miradi mbalimbali ambapo miradi husika hupambwa na watanzania kujazwa matumaini kupitia camera za tv, lakini mwisho wa siku miradi hugubikwa na makandokando tofauti na ahadi za majukwaani.

Utasikia Mama anaupiga Mwingi kwa kuongea tu na Wapinzani(Mbowe).
Sasa sijui mkuu 'Erythrocyte' atachukuliaje ushauri wako huu makini kabisa!

Mbowe anatumika sasa kama kifaa!
 
Chadema hawajajua kuwa ccm ya awamu hii inafanya siasa za picha na wapinzani.
 
Back
Top Bottom