TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Hii ikataliwe kabisa, hii sasa iwe jino kwa jino.

hii imenikumbusha yale ya nyororo, igunga, na arumeru.

Hii nchi kunani, kila wakati wapinzani wanaonewa tu, hii Hali itakuwa mpaka lini?
 
Hizi ni siasa za kipuuzi. Basi watangaze tz hakuna vyama vingi. Wabakie ccm peke yako.Mungu tupe nguvu.
 
Katika mategemeo ya hata watu walio nje ya Tanzania, watanzania hawana Tabia hizo mbona tunanatoa picha tofauti na jinsi tulivyo?Siasa name kumpiga MTU kama nyati alieasi! Basis INA haja gani kusema CCM in chama tawala kama vibaraka wake wanaweza kutenda hayo?
 
Mbona watu wamekuwa kama wanyama pori WA Serengeti hawana hata ufahamu WA kibinadamu? Natumaini hao wahalifu watashughulikiwa na sheria r.i.p kamanda
mbona Tanzania imebadilika hivi??ndiyo Tanzania ile nayoifahamu mimi kisiwa cha amani na kuvumiliana au Ni nchi mpya hii ?? Uwiiiiiiii mpaka machozi yananitoka. Justice should prevail.

Hiyo tanzania unayoifikiria wewe ilishatoweka siku nyingi sana
 
Kwa kweli roho imeniuma sana.Hakika iko siku udhalimu huu utaisha.Roho ya marehemu ipumzike kwa amani,Amen.
 
Hakuna sababu ya kulipiza kisasi sababu hautakuwa tofauti nao.Tunahitaji kuwa tofauti nao.
 
eddy unaelewa nini unaandika? Mantiki ya bandiko lako ni kwamba unahalalisha kuuawa kwa Mawazo? Kama ni kweli basi ujinga huu na ukutoke!!
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii imefika hatua ya mauaji kuwa jambo la kawaida, mauaji yanafanywa na Vijana wa Ccm hatua haichukuliwi, Mioyo wa Watanzania iko mikononi mwa wana Siasa, mwana siasa anaweza kuamua aidha kuishi ama kutokuishi wa mtu mwingine (Mpinzani), kwa kuwa hawataki waiishi.

Alphonce Mawazo anauliwa na Green Guard halafu Serikali iko kimya, hatari sana, naomba tukumbuke haya yaliyotokea Ugiriki.

Tunasafari ndefu nchini kwetu. Ugiriki alipouawa mwanafunzi na polisi nchi nzima ili protest kwa miezi 6 mpaka serikali ikaangushwa.

Watanzania manyanyaso haya mpaka LINI?
 
so sad tuko kwenye kipindi kigumu sana kwa wakati huu lazima ujiulize kwanini itokee wakati huu .siasa za zanzibar bado ,mh lowasa anatoa statement kesho kisiasa hii ina tafsiri kubwa ,tafsiri yake ni kuwa ule mkazo wa kimawazo uhame kwa kuwa kuna tukio tayari limetokea ,swali ni je hawa green guard watachukuliwa hatua gani dhidi ya unyama waliotenda ,na je nani atasimamia hili,tunasikitika kwa kitendo hiki kiovu
 
Geita wamezoea kuuana.

Andrew wanauana kwa kulipiza kisasi sasa huyu kijana amewakosea nini???Ninaamini ni kifo kilichopangwa na wauaji wamelipwa.Serikali kupitia polisi ilibidi ifanye kazi ya ziada kuwatafuta wauaji na aliyewatuma.
Siamini kama vijana tu wameamua kuua hawa watakuwa wamelipwa ili kutekeleza.azma ya kuua.

Chuki hii ikiendelea sidhani kama.inatupeleka pazuri kama Taifa
 
Unavyo wajibu wenzako as if aliyeuawa si binadamu kama wewe.Angalia chuki haijengi bali kubomoa.Hakuna mahali kwenye katiba nimesema.ukiwa upinzani basi haki yako ni kaburi.Kama binadamu inasikitisha.Wala hufai kuitwa hivyo
Wewe ndo hufai kuitwa binadamu. Wapi nimeandika mpinzani haki yake kaburi?.. kama hujui kusoma omba msaada kwa jirani au kwa konda kama uko ndani ya daladala
 
......na walaaniwe wote waliofanya unyama huu pamoja na wanaowasapoti.....
 
so sad tuko kwenye kipindi kigumu sana kwa wakati huu lazima ujiulize kwanini itokee wakati huu .siasa za zanzibar bado ,mh lowasa anatoa statement kesho kisiasa hii ina tafsiri kubwa ,tafsiri yake ni kuwa ule mkazo wa kimawazo uhame kwa kuwa kuna tukio tayari limetokea ,swali ni je hawa green guard watachukuliwa hatua gani dhidi ya unyama waliotenda ,na je nani atasimamia hili,tunasikitika kwa kitendo hiki kiovu
Hao vijana wamelipwa kufanya mauaji hayo.Na polisi wanafahamu.ndiyo sababu hawakufika hata kwenye tukio kupata Maelezo ya kifo hicho.Ila amekufa kifo Kibaha mno hakifai kuelezea.

Tunatengeneza jamii yenye ubaguzi wa itikadi na ukabila.Sintofahamu.hii kama.Serikali haitalichukulia hatuna stahiki basi tutegemee mabaya zaidi
 
Aisee Tena kauawa kwa mapanga as if jamaa alikuwa jambazi vile
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom