TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Tufanye siasa za majukwaani. Tusifike mahali pa kupoteza maisha ya vijana ambao ni hazina ya Taifa hili kama marehemu Alfonce Mawazo. Huyu ndiye aliyekuwa nguzo ya chadema kanda ya ziwa.
Uccm na uchadema uwe majukwaani tu. Usiende mpk kwenye maisha binafsi ya watu.
Kamanda Mbowe ametulia, sina shaka anasubiri tamko la kalipio toka kwa Makomeo. Endapo Makomeo hatosema chochote, chondechonde kamanda Mbowe toa kauli mujarabu itakayotoa dira na mustakabali wa makamanda wako wote walioko pande zote za nchi hii. Inatia shaka, inatia woga lakini pia inatuamsha.
Kwa mwenye upeo amenielewa. R.I.P kamanda Mawazo. Your name shall be young forever.
 
Jamani hili ni jinamizi au nininii? Si juzi tu ITV wametuonyesha migambo wamechoma nyumba za watu geita bila kuuliza wala kumsikiliza mtu? Au hii ni Geita nyingine?

Ah where are going?
 
Vifo vya wanasiasa ni mtaji kwa baadhi ya wanasiasa! Sipati picha Filikunjombe, Mtikila, Kombani, Kigoda, R.I.P wote, kama wangekuwa ukawa sijui ingekuwaje!
 
Reactions: nao
Mbona kamanda Chacha Wangwe hakuzikwa kitaifa na chama wakati alikuwa makamu mwenyekiti wa chama. Mpaka leo hata familia yake mmeitelekeza bila msaada wowote. Acheni uhuni huu.

Ingawa mimi sina chama, ile ilikuwa accident, na viongozi waandamizi walifika tarime ili kufanya utaratibu wa mazishi na kufukuzwa na watu walioandaliwa na chama fulani.
Note:
Alphonce ameuwawa kikatili, lengo la mtoa mada ni viongozi kufika hapa katoro na kutoa kauli zao pamoja kumfariji mjane na kupaza sauti zao juu ya kifo cha mtanzania. Najiuliza, lengo la kutoa roho ya mtu ni udiwani tu?
Hata huyu aliyewatuma asipokamatwa moyoni mwake atakuwa na amani? Udiwani imekuwa dilli kiasi cha kuuwa mtanzania mwenzio kwa kumshambulia kwa silaha za jadi kama jambazi?
 
Rip,hakua na visasi na watu kweli?

Hata kama ni visasi ndio itokee kwenye mkutano wa hadhara? Polisi walikuwa wapi mpaka itokee hivyo? Hii imepangwa bila kupepesa macho. Muhimu huyo diwani wa CHADEMA apigiwe kura kwa hasira ashinde
 

Akili, mwili vikishachoka hata roho ya binadamu inachoka so Maamuzi yanakuwa ni hohehahe, unatafuta kilicho karibu na rahisi kumsulubu mtu unayeona anakusumbua lkn kumbe hakusumbui, ni mtoto anakijulisha kalamu linakaribia kuisha wewe unaona unasumbuliwa, shoka likiwa karibu unampa la kichwa akifa unafurahi umepunguza matatizo kumbe ndiyo umeongeza
 
barafuyamoto hao wote uliowataja hakuna hata mmoja kati yao aliyeuawa kwa kupigwa mapanga!! Maziwa na Tui la nazi vinafanana kwa rangi lakini ladha na uasili wake wala si kitu kimoja!!
 
Last edited by a moderator:
Jamani hili ni jinamizi au nininii? Si juzi tu ITV wametuonyesha migambo wamechoma nyumba za watu geita bila kuuliza wala kumsikiliza mtu? Au hii ni Geita nyingine?

Ah where are going?

Unausianisha mambo yasiyokuwa na ufanano
 
Mleta uzi, Subiri kuwasikia ukawa wakitiririka at their best! If you know what i mean, their pukes are the result of God's wrath on them!
 

TUMIA AKILI KUTAMBUA MAZINGIRA YA VIFO VYOTE VIWILI KATI I YA MABINA NA MAWAZO!
-Mabina alikuwa mnyang'anyi wa viwanja na alienda na MABAUNSA.
-MAWAZO ALIKUWA KWENYE SHUGHULI YA KISIASA NA TAARIFA ZINASEMA MA GREEN GUARD WAKAMKILLL KAMANDA......r.i.p mawazo!
 
Lazima kufuata sheria za nchi. Tukio la Geita lina utata. Mimi wasi wasi wangu mkulima wa kijijini hawezi piga picha nzuri kiasi hicho. Hili tukio halina tofauti na mtikila ndiyo maana inawezekana ni hao hao chadema. Ndiyo maana tusikurupuke tusubiri uchunguzi. Maana mke wa mtikila aliomba tume na sijui kama iliundwa.
 
barafuyamoto hao wote uliowataja hakuna hata mmoja kati yao aliyeuawa kwa kupigwa mapanga!! Maziwa na Tui la nazi vinafanana kwa rangi lakini ladha na uasili wake wala si kitu kimoja!!
Mbona wafugaji na wakulima wanachinjana kwa mapanga na mishale? Hili huwa hamlioni? Report ya polisi inasemaje? Na wewe unasemaje kuhusu 'ushahidi' wako?
R.I.P huyu Kamanda Mawazo, ila watu kuanza kumtumia kama chambo ya kupata kick ya siasa, sio vizuri!
 
Last edited by a moderator:
Nakumbusha machungu yalipoanzia
1,chacha wangwe
2,Mtikila
3,filipolunjombe

Mimi nawakumnuka hawa shujaa wa taifa,
 
CCM mnadhani nyie ndiyo wenye hatimiliki ya nchi hii.
Mtaweza kutuua wote mkatumaliza?
Tusikurupuke kushutumu chama. Mbona nyie chadema mlimuua chacha wangwe. Mbona nyie chadema mlimtishia kumuua Dr Slaa mpaka akakimbia nchi? Mbona nyie chadema inasemekana ndiyo mmehusika na kifo cha mtikila. Kwa nini marehemu apigwe picha style sawa na zile za mtikila? Kwa nini mpiga picha kapiga picha zenye ubora hivyo? Sidhani kama kuna hao vijana wa ccm wana kamera nzuri kiasi hicho zaidi yenu nyie chadema. Hivyo tuache kukurupuka tusubiri uchunguzi.
 

Ongezea
1,chacha wangwe
2, mtikila
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…