TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Tufanye siasa za majukwaani. Tusifike mahali pa kupoteza maisha ya vijana ambao ni hazina ya Taifa hili kama marehemu Alfonce Mawazo. Huyu ndiye aliyekuwa nguzo ya chadema kanda ya ziwa.
Uccm na uchadema uwe majukwaani tu. Usiende mpk kwenye maisha binafsi ya watu.
Kamanda Mbowe ametulia, sina shaka anasubiri tamko la kalipio toka kwa Makomeo. Endapo Makomeo hatosema chochote, chondechonde kamanda Mbowe toa kauli mujarabu itakayotoa dira na mustakabali wa makamanda wako wote walioko pande zote za nchi hii. Inatia shaka, inatia woga lakini pia inatuamsha.
Kwa mwenye upeo amenielewa. R.I.P kamanda Mawazo. Your name shall be young forever.
 
Jamani hili ni jinamizi au nininii? Si juzi tu ITV wametuonyesha migambo wamechoma nyumba za watu geita bila kuuliza wala kumsikiliza mtu? Au hii ni Geita nyingine?

Ah where are going?
 
Vifo vya wanasiasa ni mtaji kwa baadhi ya wanasiasa! Sipati picha Filikunjombe, Mtikila, Kombani, Kigoda, R.I.P wote, kama wangekuwa ukawa sijui ingekuwaje!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mbona kamanda Chacha Wangwe hakuzikwa kitaifa na chama wakati alikuwa makamu mwenyekiti wa chama. Mpaka leo hata familia yake mmeitelekeza bila msaada wowote. Acheni uhuni huu.

Ingawa mimi sina chama, ile ilikuwa accident, na viongozi waandamizi walifika tarime ili kufanya utaratibu wa mazishi na kufukuzwa na watu walioandaliwa na chama fulani.
Note:
Alphonce ameuwawa kikatili, lengo la mtoa mada ni viongozi kufika hapa katoro na kutoa kauli zao pamoja kumfariji mjane na kupaza sauti zao juu ya kifo cha mtanzania. Najiuliza, lengo la kutoa roho ya mtu ni udiwani tu?
Hata huyu aliyewatuma asipokamatwa moyoni mwake atakuwa na amani? Udiwani imekuwa dilli kiasi cha kuuwa mtanzania mwenzio kwa kumshambulia kwa silaha za jadi kama jambazi?
 
Rip,hakua na visasi na watu kweli?

Hata kama ni visasi ndio itokee kwenye mkutano wa hadhara? Polisi walikuwa wapi mpaka itokee hivyo? Hii imepangwa bila kupepesa macho. Muhimu huyo diwani wa CHADEMA apigiwe kura kwa hasira ashinde
 
Na naona wafuasi na viongozi wao wanafurahia haya matendo haramu kwa kudhani kwamba wao wako salama.Wamewageuza Watanzania kama Nyumbu ambao mwenzao anakamatwa na kuliwa na Simba halafu wengine wanaendelea na taratibu za maisha kana kwamba kilichotokea ni jambo la kawaida lisilo na athari za kimaisha.Wanashindwa katambua ya kwamba unapotajwa kuwa kiongozi wa Tanzania moja ya dhamana kubwa uliyo nayo ni kulinda uhai wa kila Mtu awe Mtanzania au yeyote aliyomo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akili, mwili vikishachoka hata roho ya binadamu inachoka so Maamuzi yanakuwa ni hohehahe, unatafuta kilicho karibu na rahisi kumsulubu mtu unayeona anakusumbua lkn kumbe hakusumbui, ni mtoto anakijulisha kalamu linakaribia kuisha wewe unaona unasumbuliwa, shoka likiwa karibu unampa la kichwa akifa unafurahi umepunguza matatizo kumbe ndiyo umeongeza
 
barafuyamoto hao wote uliowataja hakuna hata mmoja kati yao aliyeuawa kwa kupigwa mapanga!! Maziwa na Tui la nazi vinafanana kwa rangi lakini ladha na uasili wake wala si kitu kimoja!!
 
Last edited by a moderator:
Jamani hili ni jinamizi au nininii? Si juzi tu ITV wametuonyesha migambo wamechoma nyumba za watu geita bila kuuliza wala kumsikiliza mtu? Au hii ni Geita nyingine?

Ah where are going?

Unausianisha mambo yasiyokuwa na ufanano
 
Mleta uzi, Subiri kuwasikia ukawa wakitiririka at their best! If you know what i mean, their pukes are the result of God's wrath on them!
 
Mbona watu hao hao wa kanda ya ziwa walimuua Mabina na sisi CCM hatukunyooshea kidole kuwa ni CHADEMA ndio walihusika na mahuaji na badala yake tuliviacha vyombo vya dola vitoe taarifa? Ningeomba na nyinyi pia muwe na subira wakati vyombo vya dola vikiendelea kufanya upelelezi.

TUMIA AKILI KUTAMBUA MAZINGIRA YA VIFO VYOTE VIWILI KATI I YA MABINA NA MAWAZO!
-Mabina alikuwa mnyang'anyi wa viwanja na alienda na MABAUNSA.
-MAWAZO ALIKUWA KWENYE SHUGHULI YA KISIASA NA TAARIFA ZINASEMA MA GREEN GUARD WAKAMKILLL KAMANDA......r.i.p mawazo!
 
Ni hatari kweli huko tunakoenda. Haya yanatokea wakati tuna Masheikh wanaozea gerezani. Amani tutaiimba sana lakini kama haki haitotendeka basi tutarajie mgeuko. Wale masheikh walivyodhalilishwa wengi tulishangilia na hata kuona wale ni magaidi. Hawana haki ya kusikilizwa. Tukasahau tatizo kubwa la kimfumo ambalo wachache kwa kutumia pesa na mamlaka wana maamuzi juu ya uhai na haki za wengine. Isingedhaniwa siasa tena katika ngazi ya ubunge au udiwani ufikie watu Kutoana roho .Hizi roho ngumu za kuua zinatoka wapi ikiwa wauaji na waliouliwa sio Waislamu?. Sasa hapa najiuliza; Ni UPI UGAIDI NA NANI GAIDI? Yule aliyemuua Mawazo au yule aliyemtuma muuwaji? Haki itendeke kwa nani hasa??.
Lazima kufuata sheria za nchi. Tukio la Geita lina utata. Mimi wasi wasi wangu mkulima wa kijijini hawezi piga picha nzuri kiasi hicho. Hili tukio halina tofauti na mtikila ndiyo maana inawezekana ni hao hao chadema. Ndiyo maana tusikurupuke tusubiri uchunguzi. Maana mke wa mtikila aliomba tume na sijui kama iliundwa.
 
barafuyamoto hao wote uliowataja hakuna hata mmoja kati yao aliyeuawa kwa kupigwa mapanga!! Maziwa na Tui la nazi vinafanana kwa rangi lakini ladha na uasili wake wala si kitu kimoja!!
Mbona wafugaji na wakulima wanachinjana kwa mapanga na mishale? Hili huwa hamlioni? Report ya polisi inasemaje? Na wewe unasemaje kuhusu 'ushahidi' wako?
R.I.P huyu Kamanda Mawazo, ila watu kuanza kumtumia kama chambo ya kupata kick ya siasa, sio vizuri!
 
Last edited by a moderator:
Nakumbusha machungu yalipoanzia
1,chacha wangwe
2,Mtikila
3,filipolunjombe

Mimi nawakumnuka hawa shujaa wa taifa,
 
CCM mnadhani nyie ndiyo wenye hatimiliki ya nchi hii.
Mtaweza kutuua wote mkatumaliza?
Tusikurupuke kushutumu chama. Mbona nyie chadema mlimuua chacha wangwe. Mbona nyie chadema mlimtishia kumuua Dr Slaa mpaka akakimbia nchi? Mbona nyie chadema inasemekana ndiyo mmehusika na kifo cha mtikila. Kwa nini marehemu apigwe picha style sawa na zile za mtikila? Kwa nini mpiga picha kapiga picha zenye ubora hivyo? Sidhani kama kuna hao vijana wa ccm wana kamera nzuri kiasi hicho zaidi yenu nyie chadema. Hivyo tuache kukurupuka tusubiri uchunguzi.
 
Kadri siku zinavyoyoyoma ndivyo amani inavyotoweka ndani ya mioyo ya wapenda haki wengi wa nchi hii.
Hapa nchini Kila Mara Uchungu unawekwa kwenye akiba ya UCHUNGU MKUU!
Usipokuja asubuhi basi utegemea jioni.

Jana maadui wa Amani wameongeza tena UCHUNGU kwenye account ya mioyo ya wengi kwa Mauaji ya Alfonce Mawazo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa Wa Geita.

NIMEKUWA NAJIULIZA SWALI HILI JADIDI,
Hivi kweli Dola hili kubwa limeridhika kabisa kuwa taifa la watekaji na wauaji?
Kama si hivyo naomba niambiwe,
Nani alimuua Daudi Mwangosi?
Nani walimuuwa Dr Mvungi
Nani walimteka na Kumpiga vile Dr Ulimboka
Vipi kuhusu Absalomu Kibanda; na wengine wengi walioteswa na kuuawa vilevile kama hawa!

Mpaka sasa ni hatua gani zilichukuliwa na vyombo husika ili haki itendeke, na ionekane wote kutendeka.

Hofu yangu hapa ambayo kwa kweli sijui kama wenzangu wanayo ni pale
Kikombe cha Uovu na Ubaya wa taifa kinapojaa na kumwagika sana!

Yaani ni kana kwamba foleni imesogea na zamu yetu imewadia!
Swali ni kuwa ili msambaratiko huu utimie je utapelekewa na mauaji ya nani, wapi, na lini?

Na je tokea sasa zimebaki hatua ngapi ili tuvuke mstali na kuvuna kile tulichokipanda wenyewe kwa gharama ya ujinga na ulevi wetu!

Napatata mashaka makubwa juu dhamira ya watesaji na wauaji hawa! Hivi kwani wao hawaoni kuwa wanalipeleka taifa hili kusiko?

Najua wakurupukaji watakuja na mengi lakini
Huu si Utabiri wa kiganga la!
Hii ni kanuni ya asili tu!
Mtu huzaliwa na baadaye hufa.
Taifa huundwa hatimae huparanganyika.

Mwisho kabisa,
Ukimwona mtu mzima juu ya mti, anaelekea kwenye tawi kavu; ukamwonya asikubali; akianguka chini, je ni wewe uliyemsababishia anguko lake? Hapana!
Ukivunja kanuni ya asili ni lazima upate stahili yako.

Ongezea
1,chacha wangwe
2, mtikila
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom