TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Kuna kila dalili za sisa za CCM kuleta shida ndani ya nchi.Wana sasa za kugombnisha na kutenganisha Watanzania halafu kwenye majukwaa wanahubiri amani.Tunaona ambavyo wamehubiri kuhusu kuwatenga wa Kaskazini na sasa wamejenga kanda ya Ziwa.
 
.......siasa ni kushindanisha hoja......hawa vijana pamoja na wanowatuma sisi wote tutakufa na tutaenda kutoa hesabu ya mataendo yetu mbele ya kiti cha hujumu.......RIP kamanda
 
hapo utawasikia Polisi na kauli zao "uchunguzi unaendelea" na wanachama na viongozi wa CHADEMA ndio watakaokamatwa
 
Aisee si ujaribu tu kuwa muungwana kwenye hili jambo? Linapotokea jambo la msiba basi jaribu kumsitiri marehemu hata kama unayajua maovu yake kumbuka zuri lake hata moja tu

Unajisumbua bure tu kumshauri huyo mwendawazimu; wana ccm wengi wanadhani kwa kule kua kwao chama DOLA basi mauti haiwahusu; mambo kama haya yasipokemewa mapema na hatua stahiki kuchukuliwa ndio yanayoweza kuchochea kilichotoke Burundi na Rwanda miaka ya 90. Kama nitakumbuka vizuri serikali iliyokuwepo madarakani ilianza kuwaua Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani, kilichotokea wale waliokua wanauawa wakaanza nao kulipinza kisasi, kilichotokea ni HISTORIA ambayo kila mtu anaifahamu. RIP Mawazo, umekwenda lakini FIKRA zako bado zina ishi na zitaishi.
 
Hivi vijana wa CCM wako juu ya sheria? Mbona kama haki haitatendeka nchi itakwenda pabaya. Tukumbuke vita haitangalia nani yuko CCM au wapi. Jamani wazazi wawafundishe watoto wao maadili. Haiwezekani tukawa tunaimba amani huku tunatembea na mapanga kwenye suruali zetu. Haiwezekani.

hapa tanzania ukiwa ccm wewe ni raia daraja la kwanza. wengine ni daraja la pili. nakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu ccm walikuwa na kituo cha kujumlishia kura pale mlimani city lakini hawakukamatwa na polis. chadema nao walikuwa na vituo vitatu dar. walivamiwa na pilis na kuswekwa rumande na kupewa kosa lingine tofauti. kwa hili la geita hakuna hatua kali zitakazochukuliwa kamwe...
 
Mola amrehemu. Poleni wafiwa na wote walioguswa na msiba huu.
 
Chadema siku hizi imekuwa kama ya wasichana! Tunashindwa hata na wazanzibar!!!
 
Siasa za nchi hii mwelekeo si mnzuri yaani zina dhidi kutawala
 
Na kampeni zote zile ccm waje wamuue uchaguzi umeshapita na wameshinda?,aah wapi hapa kuna kitu,wote mliokula pesa ya laigwanan kaeni chonjo,,,

Unahitajika polisi kwa taarifa zaidi, maana inaonekana una habari zaidi za unyeti
 
Unamaana cdm na cuf ndiyo wauwaji

hustahili kuitwa mwanadamu maana uwezo wako kiajili ni duni kuliko mbwa.

Umeshasikia popote hao uliwataja wameuwa? Au wao ndio wanauwawa, kutiwa lockup na kupigwa.

Mkuu punguza mihemko na jazba utanielewa. Ata mie nimeskitika kumpoteza kamanda, ila logic yangu ilikuwa ni lazima tukubali matokeo ya tunachokihubiri. Hivi ukiwa unasema lazima damu imwagike? Watanzania tuache ujinga tupambane? Unakuwa unategemea nani damu yake ndio aina thamani ianze kumwagika?

Ulishawai kuskia Zitto kasweka ndani kwa kuhatarisha amani? Ushawai ona mnyika anapambana na polisi au wahuni mitaani? Ebu niambie awa watu kuna anaewafikia bungeni kwa sasa kwa uwezo wao wa kuwasilisha hoja? Tuache siasa za chuki, tukizipenda tukubali gharama zake.

Siamini kama huyu marehemu aliuawa kwa kuvamiwa tu na watu kisha wakamuua. Kuna mlolongo uliopelekea kutokea vurugu zilizopelekea kifo chake na chanzo lazima kipo.

Yote kwa yote Mungu amrehemu.
 
Sasa hamtaki kueleza,ilikuaje,kavamiwa au kulitokea,,,,,,,,,,,,,,,,aah kwanza hayanihusu..............
 
R.I.P kamanda. Sheria ichukue mkondo wake kwa wahusika. Hili la mauaji linapaswa kukemewa. Kama ni huyo kamanda ndo alikiwa chanzo, ukweli ubainishwe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom