TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
In?sikitisha sana nani anaehubiri siasa za mihemko kama siyo ccm, acheni hizo tambueni yupo Mungu anaehukumu kwahaki. R.I.P.ndugu yetu Alphonce Mawazo. Mungu atajibu tu poleni makamanda wote
 
Kwa Ishu kama hizi sidhani kama ni sahihi tuendelee kujiita TANZANIA kisiwa cha amani, napendekeza tuchapane tu, ili heshima iwepo! Napenda sana vita!
 
R.I.P,Alphonce Mawazo hakika harakati zako zitakumbukwa.
Duniani wote tunapita,
 
Nimeiona kwenye ITV wametangaza kuwa ameshafariki. Hii ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu, maana nimeona jinsi watu walivyo na hasira, hii si dalili njema. Watanzania ni lazima tufikie mahali tuwe na siasa za kiungwana. amani ya nchi yetu ni muhimu kuliko hata vyama vyetu. Ni kwanini tufikie huko? Ninawasihi wote walioumizwa na tukio hili kuwa wavumilivu na kuruhusu sheria ichukue mkondo wake. Wasijaribu kuchukua sheria mkononi kwani itakuwa ni kuharibu zaidi kuliko kutengeneza.
 
kwapamoja vijana wazee akina dada hizi siasa za chuki hadi tunatoana roho hazifai na hazilipeleki taifa letu mbele tusikubali kutumika vibaya kisiasa
 
Hili swala tunapolijadili tuondoe itikadi za kivyama..

Naamini hakuna chama kinachoruhusu mauaji... Wahuni wachache kwa maslahi yao.

Nimesoma toka mwanzo nashindwa kuelewa chanzo cha tukio kilikuwa nini ..

R.İ.P Aliphonce Mawazo.

Wamesema ni green guard sasa green guard ni unadhani ni watu gani?
 
Sioni faida ya TANZANIA yenye AMANI, kama MAWAZO umeuwawa na TANZANIA iko kimya, mimi sintanyamaza, Sioni faida yeyote ya kuendelea kuwa na AMANI pasipo haki, bora tufunzane adabu tu! Mwisho wa siku tutaheshimiana!
 
Ngoja niitume hii kwa Tcra,polisi makao makuu,na kwa kamishna wa upelelezi wa makosa ya jinai sasa hivi,una ushahidi wote tunaouhitaji,thanks in advance!!
Sidhani kama itatokea tcra, polisi au chombo chochote cha dola kitachukua hatua stahili dhidi ya kosa lolote ( liwe la matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ) linalotendwa na mfuasi wa ccm dhidi ya viongozi wa CHADEMA. Tulishuhudia na tunaendelea kushuhudia matusi ya nguoni toka kwa viongozi wa ccm na wafuasi wao lakini hamna mamlaka yoyote iliyochukua hatua. Hata hili la kamanda Mawazo ( R.I.P ) litapita hivihivi. Rejea mauaji ya kamanda Mbwambo mwenyekiti wa CHADEMA usariver, wauaji walikamatwa lakini eti walitoroka mikononi mwa polisi wakiwa mahakamani. Sisi tushtaki kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi, yeye atajua namna njema ya kuwaadhibu hawa wauaji. Inauma sana
 
Kwa jinsi ninavyowajua ndugu zangu wa kanda ya ziwa, hii issue haitaisha. Mungu uturehemu ... Pole kwa ndugu na jamaa.
 
Rip kamanda Mawazo.

Hivi Tanzania kuna amani kweli? Au amani kwa wenye dola pekee?
 
Inauma sana!pumzika kwa amani kamanda Mawazo!historia haitakutupa!
 
Watanzania mwenzangu hii ni taarifa ya huzuni sana kwetu wote.

Ndg:Alfonce Mawazo ameuawa Kwa kupigwa Mapanga na watu wasiojulikana alipokuwa Katoro ktk harakati za kuratibu na kampeni za udiwani Katoro jimbo la Busanda-Geita.

Kifo chake kimethibitishwa ktk Hospitali ya Mkoa wa Geita baada ya Juhudi za Kuokoa Maisha yake ilishindikana.

Marehemu pia alikuwa mgombea Ubunge ktk uchaguzi iliyopita akiwakilisha Chadema na UKAWA Kwa ujumla.

Kitendo hiki cha kinyama na cha kishenzi kimetuuzi sana Kwa kweli
 
tanzania tuwashukuru sana viongozi wetu wa upinzani ni wavumilivu sana ndo siri ya amani yetu. mfano tazama kilichotokea zanzibar...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom