GE2025 Mwenyekiti wa TAS Mollel: Tunaomba Rais Samia aongezewe muda

GE2025 Mwenyekiti wa TAS Mollel: Tunaomba Rais Samia aongezewe muda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS), Godson Mollel, amemsifu mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna alivyowajali watu wenye ulemavu katika kipindi cha karibu miaka mitano akiwa madarakani.

Akizungumza Alhamisi, Oktoba 2, 2025, katika mkutano wa kampeni unaofanyika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mollel amesema kundi la watu wenye ulemavu litampigia kura Dkt. Samia katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

"Kwa sababu wewe ni mama na una dhamira njema kwa Watanzania wako, hutaki kundi lolote libaki nyuma. Ukatujali, tunalazimika kukufia, tunalazimika kukutetea usiku na mchana," amesema Mollel.

Ameongeza kuwa dhamira ya Dkt. Samia imejidhihirisha kupitia utekelezaji wa sera na miradi iliyoangazia kundi la watu wenye ulemavu, na kwamba anaamini dhamira hiyo itaendelezwa endapo atapewa ridhaa ya kuunda serikali kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

"Mimi ningekuwa na mamlaka ya kuivunja katiba ya Chama Cha Mapinduzi, miaka mitano ijayo haikutoshi kwa ajili ya Watanzania. Una dhamira nzuri kwa Watanzania, hao waropokaji wanaoropoka Mungu awasamehe", ameeleza

 

Attachments

  • VIDEO-Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS), Godson Mollel, amemsifu mgombea.mp4
    9.8 MB
Back
Top Bottom